Bwana na Bibi Harusi wana kosa gani?

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
amka2.gif
WAKATI serikali ikiwa kwenye harakati za kumkomboa mtoto wa kike kielimu juhudi hizo zinarudishwa nyuma na baadhi ya wapinga maendeleo akiwemo mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Byuna, wilayani Bariadi, mkoani Shinyanga, Deogratias China (29), ambaye ameamua kumuoa mwafunzi wake.

Mwalimu huyo hivi sasa ameshikiliwa na jeshi la polisi wilayani kwa kosa la kufunga ndoa na mwanafunzi wake kwenye ofisi za mkuu wa wilaya hiyo juzi.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi majira ya mchana mara baada ya mtuhumiwa huyo kukamilisha taratibu za kula kiapo na mwanafunzi huyo Amina Idd (22) anayesoma kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kishampanda iliyoko katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambapo polisi walipopata taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo waliandaa mtego.



Kufuatia tukio hilo polisi walimtia mbaroni mtuhumiwa huyo pamoja na mshenga wake Kabala Charles na mshenga wa bibi harusi ambaye ni mama wa kambo wa mwanafunzi huyo Suzana Masubati kutokana na kukiuka taratibu za nchi za kushuhudia ndoa ya mwanafunzi na kukubali kuwa mashahidi.


Ndoa hiyo iliingia dosari mara tu baada ya kufungwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya mbele ya katibu tawala wa wilaya, Jackson Sima, na wahusika kuweka sahihi zao kuthibitisha makubaliano yao ya ndoa ya mke mmoja huku mashahidi nao wakitia saini zao kuthibitisha uharamu huo.



Tanzania Daima Jumapili lilifanya mahojiano na mwanafunzi huyo akiwa kituo cha polisi ambapo alisema kuwa yeye na mpenzi wake huyo walikubaliana kufunga ndoa kwa lengo la kupata cheti wakati yeye akiendelea na masomo na kumuahidi kuwa akimaliza shule wangeishi pamoja.



"Aliniambia kuwa yeye anataka apate cheti mimi sikuelewa cha kazi gani lakini sikuwa na tatizo naye kwani hata nyumbani wanamfahamu kuwa ni mchumba wangu wa siku nyingi ingawa mama aliwahi kumweleza kuwa anisubiri nimalize kwanza masomo ndipo anioe," alisema Amina.



Mwanafunzi huyo alisema kuwa walionana na mwalimu huyo wakati akifundisha katika shule anayosoma yeye, mwalimu huyo akiwa katika mazoezi shuleni hapo na kuanza mahusiano akiwa mwalimu wake ambapo hivi sasa ameajiriwa katika shule nyingine na kwamba walikubaliana kufunga ndoa hiyo kipindi cha likizo.


Mama mzazi wa mwanafunzi huyo alipotakiwa kutoa maelezo, alidai kuwa amechoka sana na hayuko tayari kuzungumza na mtu yeyote juu ya tukio hilo huku mwanaye akisema kuwa walifanya siri na mama yake wa kambo wakati mama yake mzazi hakuwa na taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo.



Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Baraka Konisaga, alikemea vikali kitendo hicho na kusema kuwa mwalimu huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wote wenye tabia za aina hiyo kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike.



Alisema tabia ya baadhi ya walimu wa kiume kuwarubuni na kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike imechangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha elimu katika wilaya hiyo na taifa pamoja na kuwafanya watoto wa kike wawe wanyonge.



Alibainisha kuwa kutokana na vitendo hivyo, baadhi ya watoto wa kike wamekuwa wakipata mimba katika umri mdogo jambo linalowafanya wakose fursa ya kuendelea huku baadhi yao wakifariki wakati wa kujifungua kutokana na viungo vyao kutokomaa kwa ajili ya tendo hilo.
Aliongeza kuwa tabia hiyo imekuwa ikishamiri zaidi maeneo ya vijijini ambako baadhi ya watu wamekuwa wakijifariji kuwa mkono mrefu wa sheria hauwezi kuwafikia na kuwaadhibu kwa yale wanayoyatenda.
"Jamani hii ni aibu na kudhalilisha taaluma ya ualimu, watu wanafanya vitendo hivi wakidhani hawawezi kufikiwa na mkono wa sheria, wanajidanganya tutawasaka kokote waliko ili kukomesha tabia hii," alimalizia Konisaga.


source:freemedia.co.tz

defination ya school child: "school child" means any child who on the effective date has attained the age of seven years and includes any child who is pursuing primary school education. Tangazola serikali namba 280 la 2002.

Sheria ya ndoa, Law of marriage Act inasema nini kuhusu umri wa kuoa: (1) No person shall marry who, being male, has not attained the apparent age of eighteen years or, being female, has not attained the apparent age of fifteen years.

Mwisho, afisa tawala wa wilaya kwa nini asiwajibishwe yeye kama kuna kosa limitokea, kaandikisha ndoa ( amekaa tu hajaona kosa) kama lipo, imetangazwa bomani wiki tatu ( amekaa tu hajaona kosa), mpaka siku ya ndoa kwa nini yeye asiwajibishwe.

Wasimamizi wa ndoa wanakosa gani, maana wao sio wazazi wa msichana ( kama kungekuwa na kosa).

Tulijadili hili
 
Mimi sioni kosa! they meet the age requirement...
kwani kuna kulazimisha hapo?
 
Kwa polisi ya Tz?...wana nguvu kupita kiasi! Ivi hawana limit ya kukushika kwa 24hrs kabla ya kukusomea mashtaka?
 
Back
Top Bottom