Bwanaharusi aliyetambulika kwa jina moja la RAHIM (miaka 30) ameshindwa kutokea ktk tukio linalomuhusu la kufunga kati yake na BI HUSNA (miaka 16)
Bwanaharusi huyo aliamua kuingia mitini baada ya kuhisi kwamba huenda aliandaliwa mtego wa kukatwa na kufunguliwa kesi ya ubakaji kwa kumuoa binti wa miaka 16 ambapo kwa mujibu wa sheria za Tanzania binti wa miaka 16 anahesabiw kuwa bado ni mtoto asiyeweza kufanya maamuzi makubwa kama hayo.
Hongereni sana watu wa kutetea haki za kinamama na watoto kwa kuandaa mtego huo.