Kwa kweli ningependa sana kusikia msimamo wa mwanaharakati Mzee Mohammed Said hasa kufuatia haya yanayoendelea leo hii nchini na hasa kitendo cha serikali kumkamata Shehe Ponda Issa Ponda na kundi la vijana wa Kiislamu? Je inamkumbusha ile kamatakamata ya miaka ya sitini ambapo baadhi ya mashehe na wanasiasa wengine walikamatwa na aliyekuwa Shehe Mkuu kurudishwa Zanzibar?
Baadhi yetu tunatarajia kumsoma tena kwa makini akitupatia busara zake katika mlolongo wa matukio haya ambayo yanaonekana kuzidi kutugawa.
Mnajua ndugu zangu mnaoandika kama ulivyoandika na wengine wenye mtazamo wako, huwa nawashangaa sana. Tatizo sio Shehe Ponda na vijana hao wakiislam waliokamatwa, tatizo ni waislam kutoridhika na utaratibu uliopo ndani ya nchi yetu katika sekta mbali mbali ikiwa pamoja na elimu, ajira, utawala na kadhalika.
Ndugu zangu wakristo kweli miminawashangaa sana kwa tabia ya kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu sana. Kwa mfano, wewe unazungumzia kushikwa kwa Sheh Ponda, lakini hata siku moja hujajadili Barua ya Ponda aliyomuandikia Mh Benjamini Mkapa akiwa madarakani, ihusuyo uwiano usiolingana kati ya waislam na wakristo katika ajira za serikali. Mkapa alikubali kuwepo kwa tatizo hilo, kwahilo nilimsifu sana kwa vile hiyo ni hatua moja muhimu sana kama Rais wa nchi.
Baada ya hapo hakuna kilichofanyika. Lakini kibaya zaidi hoja zilizokuwa na ambazo zinaendelea kutolewa ni kuwa nyie waislam mlikimbia shule za Mission kwa kuogopa kulishwa Nguruwe. Ndio, hata mimi nisingeenda kusoma shule ambayo inabidi niiuze imani yangu kwa mbadala wa kitu fulani. Hii ni sawa na miaka ya hivi karibuni, kwa wahisani vijijini kutumia chakula kama njia ya kuwabadilisha watu dini. Kwa vile una njaa nitakupa mahindi lakini kwanza kuwa mkristo. Lazima wote tukubali kuwa haya yalikuwa makosa na kuwasifu wale waliokataa kwenda shule kwa ajili ya kulinda imani zao.
Ninachofahamu mimi Serikali yeyote makini huwekeza zaidi pale penye maendeleo hafifu ili napo pafikie level ya sehemu nyingine. Hata kwa sasa hivi Serikali huwekeza sana vijijini kwa vile huko maendeleo ni duni, kwa mfano miundo mbinu n.k Kwa hiyo huwa nawashangaa wote wasemao eti kwa vile mlichelewa basi iwe hivyo Tanzania yetu mpaka milele. Ukweli ni kwamba wote wenye mawazo hayo bado hawajafahamu kwanini au ni nini chanzo cha mauaji ya Halaiki kule Rwanda. Tatizo lile kwa wengi wanaliona kama Tatizo la kikabila, kumbe hali halisi ni Tatizo la kundi moja (watusi) kuwa juu sana kielimu, ajira na hivyo kuwa na awezo wa kumiliki rasilimali nyingi nchini humo.
Waisla hawadai matatizo hayo yatatuliwe leo au kesho, tunachotaka ni kuwepo utaratibu na mpango makini endelevu utaohakikisha kuwa hata kama kuna ajira chache tugawane sawa kwa kila makundi. Na mpango huu uanzie katika elimu na kuendelea. Mfumo huu wa elimu hatukuwa nao, ulipofika wote tumehamasishwa mpaka tukauelewa na wengine wakatangulia kuupenda kabla ya wengine. Sasa hatuwezi tukasema eti mmasai hauelewi huu utaratibu basi serikali imtose na waendelee na mchaga aliyeielewa shule mapema. Kweli hii si kazi ya serikali, serikali makini itawekeza zaidi kwa wamasai ili nao waonekane ofisini.
Leo hii mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari 252, ni mkoa unaoongoza Tanzania nzima, ndio ni vizuri lakini changamoto kubwa kwa serikali ni kujiuliza wafanye nini ili na Mtwara, Lindi, Pwani n.k nao wapate shule 252? Hii ndio changamoto kubwa na ningependa kuwaona wenzetu wakristo wanatoa ufumbuzi wa maswali haya magumu, kuliko kutoa hoja kuwa sisi tumeshaelimika ndio basi. Nyie wengine hamtatupata maana mliogopa nguruwe na hoja nyingine nyepesi.
Ndugu zangu wakristo tatizo si Ponda au Sheikh Farid bali ni vijana wote wa kiislam waliochoshwa na utaratibu uliopo. Panueni wigo wa kufikiri, ili tuwe pamoja katika kutatua matatizo haya.