Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

Huyu mzee anakaribia kupigwa na kiharusi. Baada ya serikali kikata ile mirija yake ya unyonyaji anaelekea kuwa mwendawazimu.
Mpeni pole na mwambieni."""CCM HAIWEZI KUFA KWA MATAKWA YAKE BALI ATAKUFA YEYE HUKU AKITAKA KUENDELEA KUISHI""""
Nilijua tu kuwa watu kama wewe mtajitokeza badala ya kuzungumza hoja aliyoleta mnamshambulia mtoa hoja. Tunawajua.
 
By BekaNurdin Yangu macho kuona hayo wakati ukifika kama Mungu atanijalia uzima.
LAKINI:
1) Wananchi mmewaandaa kiasi gani kuwezesha mabadiliko wanasiasa mnayoota?
2) CCM ndiyo wanaoandaa na kusimamia uchaguzi, kuhesabu kura na kutangaza matokeo; ni mwendawazimu yupi anayeweza kujinyonga ilhali anapenda kuendelea kuishi? Inaonesha mmeshindwa kujifunza kupitia chaguzi zilizopita. Hebu basi mjifunze kupitia rasimu ya katiba ya SITA/CHENGE enyi wapinzani.

Siasa ni unafiki sipendi kuwa mnafiki!

Hata kama wewe hujakata tamaa kama mimi, bila ku-address key issues tajwa hapo juu kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura ni ndoto!

Haiwezi kuwa ndoto mbona kuna wabunge wa upinzani hao walipatikanaje? Hatua moja huanzisha nyingine hata wao sasa hawaaminiani na ndio mtaji kwa upinzani, haba na haba hujaza kibaba. Ipo siku watamwaga ugali na mboga.
 
Huyu mzee anakaribia kupigwa na kiharusi. Baada ya serikali kikata ile mirija yake ya unyonyaji anaelekea kuwa mwendawazimu.
Mpeni pole na mwambieni."""CCM HAIWEZI KUFA KWA MATAKWA YAKE BALI ATAKUFA YEYE HUKU AKITAKA KUENDELEA KUISHI""""

Na kiharusi kikupige wewe.... wewe mbinafsi unayejali tumbo lako huku maelfu ya maskini wakiangamia kwa ulafi wako. Mungu hadhihakiwi kama unavyofanya!
 
Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.

Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.

"
Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa."

"Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama.
Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?" alihoji.

Butiku alisema: "CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa."

"Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu," alisema.

...Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.

"Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali."

Kusema tu haitoshi mzee Butiku; fanya kweli tukuone wa maana. Kwa maelezo uliyotoa, kuna sababu ya wewe kuendelea kuwa mwanachama wa CCM?
Tekeleza ulichokiongea hapo juu kwamba, "kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa!". Jivue uanachama kwani kwa maelezo yako, CCM haipo!

Au ni mpaka CCM ifanye kosa kubwa kiasi kipi cha kukufanya hata uone aibu kuendelea kuwa mwanaCCM?
Pamoja na kwamba Warioba tunamheshimu sana sasa, hata hivyo, nikimwona amevaa liguo la kijani sitampa mkono wa salamu. NDIO, Tumekereheka kiasi hicho!
 
Mzee Butiku Amekiri kuwa CCM ya leo ni tofauti na ile enzi za Mwalimu.Sioni kama watapenda ushauri wake.Azimio la Arusha lishaondoka kitambo kuna Azimio la Zanzibar.Ipo tofauti kubwa ya maazimio hayo.Mzee Butiku kama uhafiki na CCM ya leo bora ukajiondoa na kuangalia mambo ukiwa nje ya Chama.
 
Inasikitisha sana vizee ambavyo hata miaka miwili ijayo hawatokuwepo kwenye sura ya duniani,mapovu yanawatoka kwa katiba yenye muelekeo wa miaka 50 ijayo.

Huna adabu, yaani Mbunge awe ameishia la Saba ndo unataka itumike kwa miaka hamsini?

Lets say 2014+50=2064

kwa hiyo hadi 2064 Mbunge ajue kusoma na kuandika tu......

Mirembe waimarishe ulinzi la sivyo hali itakuja kuwa mbaya sana
 
Huyu mzee anakaribia kupigwa na kiharusi. Baada ya serikali kikata ile mirija yake ya unyonyaji anaelekea kuwa mwendawazimu.
Mpeni pole na mwambieni."""CCM HAIWEZI KUFA KWA MATAKWA YAKE BALI ATAKUFA YEYE HUKU AKITAKA KUENDELEA KUISHI""""

Nenda kakae na wapumbavu wenzio kule Lumumba usituharibie mada hapa!!
 
Kusafisha CCM ni kazi rahisi sana kama wanachama waadilifu wataamua. CCM ASILI itakuwa na wanachama wengi kuliko CCM mafisadi. Changamoto ni moja tu kuwa CCM ASILI ni wengi lakini waoga kuchukua hatua na wanalalamika tu ingawa masikini wote watawaunga mkono, CCM MAFISADI ni wachache, wenye kuchukua maamuzi bila wasiwasi, wanafuatwa na masikini kwa sababu ya njaa na ujinga tu!
 
By BekaNurdin Yangu macho kuona hayo wakati ukifika kama Mungu atanijalia uzima.
LAKINI:
1) Wananchi mmewaandaa kiasi gani kuwezesha mabadiliko wanasiasa mnayoota?
2) CCM ndiyo wanaoandaa na kusimamia uchaguzi, kuhesabu kura na kutangaza matokeo; ni mwendawazimu yupi anayeweza kujinyonga ilhali anapenda kuendelea kuishi? Inaonesha mmeshindwa kujifunza kupitia chaguzi zilizopita. Hebu basi mjifunze kupitia rasimu ya katiba ya SITA/CHENGE enyi wapinzani.

Siasa ni unafiki sipendi kuwa mnafiki!

Hata kama wewe hujakata tamaa kama mimi, bila ku-address key issues tajwa hapo juu kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura ni ndoto!

BekaNurdin,
Kuna Wilaya ambazo zilikataa uongozi wa CCM hapa nchini tangu kuanza kwa vyama vingi. Mimi pia pale mwanzoni nilipata mashaka kama wewe. Lakini hizo sehemu kwa kuwa wananchi waliamua kusimama imara na kwa wingi hata wizi wa kura ulishindikana, ccm ikabidi ikubali na mpaka leo wameshindwa kabisa kuyarudisha hayo majimbo CCM. Kwahiyo kusema eti haiwezekani siyo sahihi. Inawezekana sana ila kazi inabidi ifanyike kuwafungua macho watanzania wengi. Wapo ambao hata hawaamini kama vyama vingine ni vya kweli.
Na kama kuna yeyote Tanzania kwa sasa anayedhania kuwa nchi yetu haihitaji kubadilisha chama kwa ajili ya kuandaa misingi ya kweli ya Kidemokrasia na yenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Taifa zima kwa ujumla wake, atakuwa amejiunga na kundi lisilokuwa na upeo wa fikra sahihi, akili imesimama na/au kudumaa. Tunachoomba Mungu ni kundi hilo lizidi kupungua mpaka Taifa lipate nafasi ya kusonga mbele kwa kasi nzuri ya kimaendeleo. Ndiyo maana Mzee Butiku ametabiri kuwa miaka kumi litakuwa limeshatokea. Hakumaanisha kuwa haiwezi kutokea mapema zaidi, ila uwezekano wa
kudumu zaidi ya miaka kumi ni mdogo sana.
 
BUTIKU is among of those Tanzanians who r remaining in ccm party as a residual intelligent person, the rest are blighted ovum! wakifa na hao, ndo basi chama kinaondoka, hiki chama hakina kitu!
 
RIP Mwalimu, kiongozi ambaye ulijali siku zote ulijali maslahi ya Tanzania na Watanzania.

Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.

Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.

“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa. Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari, inasimama,” alisema na kuongeza:

“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”

Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa chama.

“Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama. Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?” alihoji.

Butiku alisema: “CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa.”

“Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Hatujawahi kusambaza polisi kila mahali kulinda watu wetu, walikuwa wanajilinda hata wakati wa kudai uhuru. Tulikuwa na maadui wa nje wengi, lakini tulitegemea watu wetu.”

Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa pia mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema alishawahi kueleza kuwa CCM imepoteza mwelekeo, lakini chama kikamkosoa.

Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.

“Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali.”

WANAOTAJWA URAIS CCM

Bila kutaja majina ya watu waliojitangaza kuutaka urais kupitia CCM, Butiku alisema kuwa miongoni mwao haamini kuwa yupo mwenye sifa thabiti za kushika wadhifa huo.

Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa takriban miaka 21 alisema: “Frankly (ukweli), wanaosema wanautaka (urais), wote hawana sifa ya kuwa rais. Nikipata nafasi nitawaambia kwa sababu nawafahamu.”

Alidai kati ya wale waliojitangaza, haoni yeyote kati yao mwenye uwezo wa kutetea kwa dhati maslahi ya wananchi kama utu wao, heshima, ardhi yao na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.

SIFA ZA RAIS

Akizungumzia sifa za rais, Butiku alisema kwa mtazamo wake, anaamini kuwa yeyote anayetaka urais ni lazima awe ni mtu anayetambua majukumu ya taasisi hiyo na kukubali kuyabeba kwa nia ya kulisaidia taifa na siyo kujinufaisha binafsi.

“Nyerere alituambia mtu anayetambua uzito wa urais si mtu anayeshabikia urais kama cheo. Ni mtu anayetambua uzito wake na kusema pamoja na uzito huu, mimi nitabeba (jukumu), nitasaidiana na wenzangu kuona kwamba umaskini unaondoka, afya ni nzuri zaidi na mambo mengine,” alisema Butiku.

Alitaja sifa muhimu ya pili kuwa ni lazima mtu anayekuwa rais awe ni mwadilifu, anayeheshimu watu wote na ambaye anawapenda watu wake kama anavyojipenda mwenyewe
Alisema kuwa kamwe haiwezekani mtu kushika wadhifa huo ikiwa hawapendi watu wake.

Akifafanua, alisema kumheshimu mtu na kusimamia haki na usawa ni masuala yasiyo na mjadala na hivyo, ni mambo ya msingi ambayo kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kuwa nayo.

Sifa ya tatu, kwa mujibu wa Butiku, ni kwamba rais asiwe mtu mwenye kupenda kujilimbikizia utajiri. “Huwezi kuwa rais halafu ukahangaika mno na utajiri wako binafsi. Rais anapaswa amudu presha (shinikizo) ya ndugu zake, marafiki zake, watoto wake na mke wake...ukikaa pale wakuone umekaa rais na siyo baba. Uko wakati wa (kuwa) baba na wakati wa (kuwa) baba wa wote," alisema.

Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”

Akimzungumzia Mwalimu Nyerere ambaye kesho ni kumbukumbu yake ya miaka 15 tangu alipofariki dunia Oktoba 14, 1999, Butiku alisema alikuwa ni kiongozi ambaye Watanzania na dunia nzima, wanaendelea kumsifu kwa sababu alisimamia utu na heshima, usawa na uhuru bila kujali cheo au udogo wa mtu.

CHANZO:NIPASHE

BekaNurdin,
Kuna Wilaya ambazo zilikataa uongozi wa CCM hapa nchini tangu kuanza kwa vyama vingi. Mimi pia pale mwanzoni nilipata mashaka kama wewe. Lakini hizo sehemu kwa kuwa wananchi waliamua kusimama imara na kwa wingi hata wizi wa kura ulishindikana, ccm ikabidi ikubali na mpaka leo wameshindwa kabisa kuyarudisha hayo majimbo CCM. Kwahiyo kusema eti haiwezekani siyo sahihi. Inawezekana sana ila kazi inabidi ifanyike kuwafungua macho watanzania wengi. Wapo ambao hata hawaamini kama vyama vingine ni vya kweli.
Na kama kuna yeyote Tanzania kwa sasa anayedhania kuwa nchi yetu haihitaji kubadilisha chama kwa ajili ya kuandaa misingi ya kweli ya Kidemokrasia na yenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Taifa zima kwa ujumla wake, atakuwa amejiunga na kundi lisilokuwa na upeo wa fikra sahihi, akili imesimama na/au kudumaa. Tunachoomba Mungu ni kundi hilo lizidi kupungua mpaka Taifa lipate nafasi ya kusonga mbele kwa kasi nzuri ya kimaendeleo. Ndiyo maana Mzee Butiku ametabiri kuwa miaka kumi litakuwa limeshatokea. Hakumaanisha kuwa haiwezi kutokea mapema zaidi, ila uwezekano wa
kudumu zaidi ya miaka kumi ni mdogo sana.

Ndugu,
Maelezo yako hayana tofauti na key issues hizo nilizotaja kabla. Niliimaanisha kwamba msingi mkuu wa mabadiliko ya mfumo wa utawala ni wananchi na tume huru ya uchaguzi. Ndipo nikauuliza, wananchi mnawaandaaje kufanikisha hayo? Tume huru ya uchaguzi?
Wakati mwingine wanasiasa mnachangia sana sisi wananchi tusio na vyama kukata tamaa. Harakati zenu huisha baada ya uchaguzi na kufufuka mara uchaguzi mwingine unapokaribia.
 
Back
Top Bottom