Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

kunamambo mawili hajayaweka bayana
  1. CCM haitasubiri miaka kumi, tayari kimeanza kutoka madarakani
  2. CCM haielekei/hainamuelekeo wa kutumia mabavu, ilishaanza kitambo sana
 
Butiku ni mwehu msisikilize

Basi wehu wake una faida kwa taifa. kama ndo hivyo natamani tungekua na wehu wa namna hiyo kama milioni 30 hivi hapa nchini.Nchi hii ingekua na maendeleo sana. Hata hivyo nashangaa wewe umemsikiliza tayari hutaki wengine wamsikilize.
 
Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.

Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.

“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa. Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari, inasimama,” alisema na kuongeza:

“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”

Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa chama.

“Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama. Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?” alihoji.

Butiku alisema: “CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa.”

“Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Hatujawahi kusambaza polisi kila mahali kulinda watu wetu, walikuwa wanajilinda hata wakati wa kudai uhuru. Tulikuwa na maadui wa nje wengi, lakini tulitegemea watu wetu.”

Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa pia mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema alishawahi kueleza kuwa CCM imepoteza mwelekeo, lakini chama kikamkosoa.

Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.

“Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali.”

WANAOTAJWA URAIS CCM

Bila kutaja majina ya watu waliojitangaza kuutaka urais kupitia CCM, Butiku alisema kuwa miongoni mwao haamini kuwa yupo mwenye sifa thabiti za kushika wadhifa huo.

Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa takriban miaka 21 alisema: “Frankly (ukweli), wanaosema wanautaka (urais), wote hawana sifa ya kuwa rais. Nikipata nafasi nitawaambia kwa sababu nawafahamu.”

Alidai kati ya wale waliojitangaza, haoni yeyote kati yao mwenye uwezo wa kutetea kwa dhati maslahi ya wananchi kama utu wao, heshima, ardhi yao na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.

SIFA ZA RAIS

Akizungumzia sifa za rais, Butiku alisema kwa mtazamo wake, anaamini kuwa yeyote anayetaka urais ni lazima awe ni mtu anayetambua majukumu ya taasisi hiyo na kukubali kuyabeba kwa nia ya kulisaidia taifa na siyo kujinufaisha binafsi.

“Nyerere alituambia mtu anayetambua uzito wa urais si mtu anayeshabikia urais kama cheo. Ni mtu anayetambua uzito wake na kusema pamoja na uzito huu, mimi nitabeba (jukumu), nitasaidiana na wenzangu kuona kwamba umaskini unaondoka, afya ni nzuri zaidi na mambo mengine,” alisema Butiku.

Alitaja sifa muhimu ya pili kuwa ni lazima mtu anayekuwa rais awe ni mwadilifu, anayeheshimu watu wote na ambaye anawapenda watu wake kama anavyojipenda mwenyewe
Alisema kuwa kamwe haiwezekani mtu kushika wadhifa huo ikiwa hawapendi watu wake.

Akifafanua, alisema kumheshimu mtu na kusimamia haki na usawa ni masuala yasiyo na mjadala na hivyo, ni mambo ya msingi ambayo kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kuwa nayo.

Sifa ya tatu, kwa mujibu wa Butiku, ni kwamba rais asiwe mtu mwenye kupenda kujilimbikizia utajiri. “Huwezi kuwa rais halafu ukahangaika mno na utajiri wako binafsi. Rais anapaswa amudu presha (shinikizo) ya ndugu zake, marafiki zake, watoto wake na mke wake...ukikaa pale wakuone umekaa rais na siyo baba. Uko wakati wa (kuwa) baba na wakati wa (kuwa) baba wa wote," alisema.

Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”

Akimzungumzia Mwalimu Nyerere ambaye kesho ni kumbukumbu yake ya miaka 15 tangu alipofariki dunia Oktoba 14, 1999, Butiku alisema alikuwa ni kiongozi ambaye Watanzania na dunia nzima, wanaendelea kumsifu kwa sababu alisimamia utu na heshima, usawa na uhuru bila kujali cheo au udogo wa mtu.

CHANZO:NIPASHE

leo kinana kasema ccm wanachukiwa sababu ya rushwa. kasahau ufisadi nk.
 
Basi wehu wake una faida kwa taifa. kama ndo hivyo natamani tungekua na wehu wa namna hiyo kama milioni 30 hivi hapa nchini.Nchi hii ingekua na maendeleo sana. Hata hivyo nashangaa wewe umemsikiliza tayari hutaki wengine wamsikilize
Butiku ni mwehu msisikilize

.
bilashaka umejionea mwenyewe, hahahaha, hao ndo vijana wenyewe kwa majina bandia humu, loh, wapi Chakaza mzee wa kuwachakaza buku 7 Lumumba FC??
 
Last edited by a moderator:
ngoja tusubiri kama kuna kijana wa CCM atanyenyua mdomo wake kumdhihaki huyu mzee baada ya kuwapa za uso.
Mkuu CCM inaanza kuji ISOLATE taratibu. mwisho wa siku itakua sawa na nzi kwenye utando wa buibui. Alianza Warioha, wakaja viongozi wa dini, kaja Butiku, idadi ya uasi inazidi kuongezeka tu na hawa wote CCM inawatukana lakini wana ushawishi mkubwa sana kwa jamii. Hebu fikiria Bitiku na Warioba wanaheshimika kiasi gani mahali kama mkoa wa Mara tu achana na Tanzania. Viongozi wa dini wengine wamejiapiza kufa kutetea katiba yenye maoni ya wananchi. Tunasubiri orodha ya uasi kama huu......Bila kusahau Tume ya haki za binadamu akina Bisimba, Tanganyika Lawa sosiety, jukwaa la katiba, wahanga wa mfumo kama Sumaye. Anguko haliko mbali sana. Tusubiri.
 
CCM ni chama cha mabavu.......nashukuru kupata jina lingine la magamba
 
bilashaka umejionea mwenyewe, hahahaha, hao ndo vijana wenyewe kwa majina bandia humu, loh, wapi Chakaza mzee wa kuwachakaza buku 7 Lumumba FC??
Mkuu hivi vijamaa mnavyoviitaga Lumumba buku saba, akili zao na uwezo wao wa kufikiri mwisho wao huwa ni vyumbani mwao. Hivi vikilipwa vihela wakati wa kampeni wakinunua viji TVs vya flat screen, vikochi, vikapeti, vikabati vya vyombo na nguo, sabufa, kitanda cha 6 kwa 6, halafu vikabandika vioo ukutani vikawa vinajitazama na kutunishatunisha vimisuli vyao basi vinaridhika na maisha na kujiona vimefiiiika. Wakati nchi inaibiwa. Vyenyewe havina habari. Wakati vijana wenzao wengine wao wanawaza hadi nje ya mipaka ya Tanzania kuangalia Mataifa yaliyoendelaea yalifanyaje.
 
Last edited by a moderator:
Butiku ashakuwa batiki hana jipya tena kazeeka mpaka midomo hizo elfu kumi anazolipwa na mbowe kutoa matamko haziwezi kumsaidia.
 
Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”

Ukweli unapaki kuwa ukweli, kwa nchi nyingi za Africa maraisi wanataka familia ziwe na maisha ya peponi kwa kuwa na tamaa bila kujua wao ni baba wa wote. Ni hatari imetokea kwa Ghadafi, H.Mubbaraka kwa tabia kama hizo.
Wote waliojitangaza hatujasikia mwenye kusimamia slogan anayoiamini yeye. wazalendo wa kweli karne hii kama Mandela, Nyerere, Nkuruma wako wapi?

Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.

Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.

“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa. Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari, inasimama,” alisema na kuongeza:

“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”

Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa chama.

“Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama. Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?” alihoji.

Butiku alisema: “CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa.”

“Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Hatujawahi kusambaza polisi kila mahali kulinda watu wetu, walikuwa wanajilinda hata wakati wa kudai uhuru. Tulikuwa na maadui wa nje wengi, lakini tulitegemea watu wetu.”

Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa pia mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema alishawahi kueleza kuwa CCM imepoteza mwelekeo, lakini chama kikamkosoa.

Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.

“Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali.”

WANAOTAJWA URAIS CCM

Bila kutaja majina ya watu waliojitangaza kuutaka urais kupitia CCM, Butiku alisema kuwa miongoni mwao haamini kuwa yupo mwenye sifa thabiti za kushika wadhifa huo.

Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa takriban miaka 21 alisema: “Frankly (ukweli), wanaosema wanautaka (urais), wote hawana sifa ya kuwa rais. Nikipata nafasi nitawaambia kwa sababu nawafahamu.”

Alidai kati ya wale waliojitangaza, haoni yeyote kati yao mwenye uwezo wa kutetea kwa dhati maslahi ya wananchi kama utu wao, heshima, ardhi yao na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.

SIFA ZA RAIS

Akizungumzia sifa za rais, Butiku alisema kwa mtazamo wake, anaamini kuwa yeyote anayetaka urais ni lazima awe ni mtu anayetambua majukumu ya taasisi hiyo na kukubali kuyabeba kwa nia ya kulisaidia taifa na siyo kujinufaisha binafsi.

“Nyerere alituambia mtu anayetambua uzito wa urais si mtu anayeshabikia urais kama cheo. Ni mtu anayetambua uzito wake na kusema pamoja na uzito huu, mimi nitabeba (jukumu), nitasaidiana na wenzangu kuona kwamba umaskini unaondoka, afya ni nzuri zaidi na mambo mengine,” alisema Butiku.

Alitaja sifa muhimu ya pili kuwa ni lazima mtu anayekuwa rais awe ni mwadilifu, anayeheshimu watu wote na ambaye anawapenda watu wake kama anavyojipenda mwenyewe
Alisema kuwa kamwe haiwezekani mtu kushika wadhifa huo ikiwa hawapendi watu wake.

Akifafanua, alisema kumheshimu mtu na kusimamia haki na usawa ni masuala yasiyo na mjadala na hivyo, ni mambo ya msingi ambayo kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kuwa nayo.

Sifa ya tatu, kwa mujibu wa Butiku, ni kwamba rais asiwe mtu mwenye kupenda kujilimbikizia utajiri. “Huwezi kuwa rais halafu ukahangaika mno na utajiri wako binafsi. Rais anapaswa amudu presha (shinikizo) ya ndugu zake, marafiki zake, watoto wake na mke wake...ukikaa pale wakuone umekaa rais na siyo baba. Uko wakati wa (kuwa) baba na wakati wa (kuwa) baba wa wote," alisema.

Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”

Akimzungumzia Mwalimu Nyerere ambaye kesho ni kumbukumbu yake ya miaka 15 tangu alipofariki dunia Oktoba 14, 1999, Butiku alisema alikuwa ni kiongozi ambaye Watanzania na dunia nzima, wanaendelea kumsifu kwa sababu alisimamia utu na heshima, usawa na uhuru bila kujali cheo au udogo wa mtu.

CHANZO:NIPASHE

Wakati mwingine ninapoona jinsi wanachama wa CCM kwa wingi wakitangaza nia ya kuwania urais wazee kwa vijana, wenye uwezo (angalau kidogo) na wale wasio na uwezo kabisaaaaaaa najiuliza ' hivi hawa wanatafuta 'URAIS au URAHISI'
 
Butiku ashakuwa batiki hana jipya tena kazeeka mpaka midomo hizo elfu kumi anazolipwa na mbowe kutoa matamko haziwezi kumsaidia.

Ndio nyie tunaowasema kuwa mnathamini sana Buk 7 kuliko hata maisha yenu. Upo unapost uzuzu wako badala ya kwenda kwenye fungate ya dada mwenzio Shonza aliyeamua kuyaacha maisha ya kuwa kiburudisho cha chama na kuwa "Private property ya jamaa"
Mpelekee salamu kuwa sasa amekuwa ajiheshimu ili watu wasahau ya kale (kumhusu yeye) ili huyo shemeji yenu aishi kwa amani.
ImageUploadedByJamiiForums1413193633.249757.jpg
 
Ndio nyie tunaowasema kuwa mnathamini sana Buk 7 kuliko hata maisha yenu. Upo unapost uzuzu wako badala ya kwenda kwenye fungate ya dada mwenzio Shonza aliyeamua kuyaacha maisha ya kuwa kiburudisho cha chama na kuwa "Private property ya jamaa"
Mpelekee salamu kuwa sasa amekuwa ajiheshimu ili watu wasahau ya kale (kumhusu yeye) ili huyo shemeji yenu aishi kwa amani.
View attachment 192957
du, hiyo picha nilijua ni sherehe za kipaimara
 
Inasikitisha sana vizee ambavyo hata miaka miwili ijayo hawatokuwepo kwenye sura ya duniani,mapovu yanawatoka kwa katiba yenye muelekeo wa miaka 50 ijayo.
 
mzee Butiki angesema kuwa chama hakipo mwenyekiti ka kili hivyo mara nyingi tuu,Katibu mkuu ana hubiri hivyo kila siku naibu katibu mkuu, Katibu mwenezi wajumbe wa kamati wakuu kama akina wassira, Lukuvi Membe yeye anaenda kutukana wenziwe redio, ukweli ni kwamba chama hakimo ila kinaishi kwa kivuri cha TISS na Police period
 
Kweli kabisa wote wanaotajwatajwa, na hata hao walojificha bado, kuwania 'urais' wa Tanzania hawawezi kuwa 'Nyerere'! Na hata Nyerere angekuwa miongoni mwao pia asingekuwa 'Nyerere' maana 'KILA ZAMA INA KITABU CHAKE!'
MZEE WETU BUTIKU usituvunje moyo bali uwe nasi, kama mwana CCM, kutusaidia kumpata aliye bora miongoni mwa hao wachafu wetu kama mgombea wetu wa urais!
KUANZA NA DHANA YA KUPATA MALAIKA NI DALILI NZURI SANA YA KUSHINDWA!

butiku ni aina ya warioba wanadhani wao wajua zaidi kumbe wakati wao walikuwa si chochote si lolote mambo yamebadilika kweli wajiulize kilichomfanya mwalimu nyerere ang'atuke nini alijua wakati wake umepita
 
Back
Top Bottom