Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

Butiku: Mwisho wa CCM miaka 10

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.

Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.

“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa. Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari, inasimama,” alisema na kuongeza:

“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”

Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa chama.

“Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama. Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?” alihoji.

Butiku alisema: “CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa.”

“Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Hatujawahi kusambaza polisi kila mahali kulinda watu wetu, walikuwa wanajilinda hata wakati wa kudai uhuru. Tulikuwa na maadui wa nje wengi, lakini tulitegemea watu wetu.”

Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa pia mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema alishawahi kueleza kuwa CCM imepoteza mwelekeo, lakini chama kikamkosoa.

Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.

“Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali.”

WANAOTAJWA URAIS CCM

Bila kutaja majina ya watu waliojitangaza kuutaka urais kupitia CCM, Butiku alisema kuwa miongoni mwao haamini kuwa yupo mwenye sifa thabiti za kushika wadhifa huo.

Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa takriban miaka 21 alisema: “Frankly (ukweli), wanaosema wanautaka (urais), wote hawana sifa ya kuwa rais. Nikipata nafasi nitawaambia kwa sababu nawafahamu.”

Alidai kati ya wale waliojitangaza, haoni yeyote kati yao mwenye uwezo wa kutetea kwa dhati maslahi ya wananchi kama utu wao, heshima, ardhi yao na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.

SIFA ZA RAIS

Akizungumzia sifa za rais, Butiku alisema kwa mtazamo wake, anaamini kuwa yeyote anayetaka urais ni lazima awe ni mtu anayetambua majukumu ya taasisi hiyo na kukubali kuyabeba kwa nia ya kulisaidia taifa na siyo kujinufaisha binafsi.

“Nyerere alituambia mtu anayetambua uzito wa urais si mtu anayeshabikia urais kama cheo. Ni mtu anayetambua uzito wake na kusema pamoja na uzito huu, mimi nitabeba (jukumu), nitasaidiana na wenzangu kuona kwamba umaskini unaondoka, afya ni nzuri zaidi na mambo mengine,” alisema Butiku.

Alitaja sifa muhimu ya pili kuwa ni lazima mtu anayekuwa rais awe ni mwadilifu, anayeheshimu watu wote na ambaye anawapenda watu wake kama anavyojipenda mwenyewe
Alisema kuwa kamwe haiwezekani mtu kushika wadhifa huo ikiwa hawapendi watu wake.

Akifafanua, alisema kumheshimu mtu na kusimamia haki na usawa ni masuala yasiyo na mjadala na hivyo, ni mambo ya msingi ambayo kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kuwa nayo.

Sifa ya tatu, kwa mujibu wa Butiku, ni kwamba rais asiwe mtu mwenye kupenda kujilimbikizia utajiri. “Huwezi kuwa rais halafu ukahangaika mno na utajiri wako binafsi. Rais anapaswa amudu presha (shinikizo) ya ndugu zake, marafiki zake, watoto wake na mke wake...ukikaa pale wakuone umekaa rais na siyo baba. Uko wakati wa (kuwa) baba na wakati wa (kuwa) baba wa wote," alisema.

Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”

Akimzungumzia Mwalimu Nyerere ambaye kesho ni kumbukumbu yake ya miaka 15 tangu alipofariki dunia Oktoba 14, 1999, Butiku alisema alikuwa ni kiongozi ambaye Watanzania na dunia nzima, wanaendelea kumsifu kwa sababu alisimamia utu na heshima, usawa na uhuru bila kujali cheo au udogo wa mtu.

CHANZO:NIPASHE

 
......"CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa."


Ni vema umesema wewe mzee wetu, huo ni ukweli mtupu - ila kuwapa miaka kumi ni mingi - wameshaparaganyika tayari - wamepotea uelekeo (njia) ila wanasema "twende tu". Wanaliendesha taifa bila dira, ni hatari.
 
Hata Kinana amekiri CCM ni wapuuzi, kwa mantiki hiyo mwanachi gani mwenye akili timamu atakubali kuongozwa na viongozi kutoka chama cha wapuuzi? Wananchi gani wenye akili timamamu watakubali kupigia kura rasimu ya katiba iliyopendekezwa na wapuuzi? Ni ajabu sana kuendesha bunge la mchakato wa katiba mpya kumuweka mwenyekiti mpuuzi ndio maana akaamua maamuzi ya kipuuzi. Miaka 10 mingi sana mkuu butiku, mingi sana tegemea lolote ndani ya kipindi kifupi sana. Tumechoka kodi zetu kutumiwa kipuuzi na wapuuzi.
 
Kina Butiku wanapaswa kwenda hatua ya juu zaidi, kuwaelimisha wananchi ubaya wa CCM tangu aliposadikiwa kuacha zaidi ya robo tatu ya msingi yake. HISTORIA ITAWATAJA KWA MAJINA YENU ama mkiisaidia nchi au mkiaangalia nchi inakufaa
 
Hata Kinana amekiri CCM ni wapuuzi, kwa mantiki hiyo mwanachi gani mwenye akili timamu atakubali kuongozwa na viongozi kutoka chama cha wapuuzi? Wananchi gani wenye akili timamamu watakubali kupigia kura rasimu ya katiba iliyopendekezwa na wapuuzi? Ni ajabu sana kuendesha bunge la mchakato wa katiba mpya kumuweka mwenyekiti mpuuzi ndio maana akaamua maamuzi ya kipuuzi. Miaka 10 mingi sana mkuu butiku, mingi sana tegemea lolote ndani ya kipindi kifupi sana. Tumechoka kodi zetu kutumiwa kipuuzi na wapuuzi.
Huyu jamaa anayejiita MwanaDiwani huwa hapendi thread kama hizi
 
Last edited by a moderator:
Huyu mzee anakaribia kupigwa na kiharusi. Baada ya serikali kikata ile mirija yake ya unyonyaji anaelekea kuwa mwendawazimu.
Mpeni pole na mwambieni."""CCM HAIWEZI KUFA KWA MATAKWA YAKE BALI ATAKUFA YEYE HUKU AKITAKA KUENDELEA KUISHI""""
 
Kweli kabisa wote wanaotajwatajwa, na hata hao walojificha bado, kuwania 'urais' wa Tanzania hawawezi kuwa 'Nyerere'! Na hata Nyerere angekuwa miongoni mwao pia asingekuwa 'Nyerere' maana 'KILA ZAMA INA KITABU CHAKE!'
MZEE WETU BUTIKU usituvunje moyo bali uwe nasi, kama mwana CCM, kutusaidia kumpata aliye bora miongoni mwa hao wachafu wetu kama mgombea wetu wa urais!
KUANZA NA DHANA YA KUPATA MALAIKA NI DALILI NZURI SANA YA KUSHINDWA!
 
korumbeta na kinana aliyoyasema jana naye ana kiharusi…?? Huo ndio kwel jomba kinana jana kachanika kwel kama vip zama youtube za itv utakutana nayo
 
Last edited by a moderator:
Huyu mzee anakaribia kupigwa na kiharusi. Baada ya serikali kikata ile mirija yake ya unyonyaji anaelekea kuwa mwendawazimu.
Mpeni pole na mwambieni."""CCM HAIWEZI KUFA KWA MATAKWA YAKE BALI ATAKUFA YEYE HUKU AKITAKA KUENDELEA KUISHI""""

Hata kwetu wapo kama wewe ila tunajuwa namna ya kuishi nao..

1. Suala la rushwa hilo lipo wazi JK alisema mara kadhaa lakini kasema huyu leo ndo mnaona kama jipya vile
2. Hivi zile hati chafu za halmashauri mbalimbali huwa inakuwaje..??
3. Na wafanyakazi hewa je..??
 
ccm imezeeka na wazee wake, nashangaa vijana wajuzi akina mwigulu na January na akina ridhiwani wanaweza kudhihaki maneno ya wazee kama hao.
 
Huyu jamaa anayejiita MwanaDiwani huwa hapendi thread kama hizi
Huyo mtu ulomtaja anaishi maiya ya kiujnjaujanja. Wewe huwezi kuwa unakisifia chama kinachopingwa kila mahali.Makanisani, misikitini, vyuoni, magengeni, makongamanoni, mashuleni, mabarabarani angani na majini. Ukiona mtu wa hivyo hawezi kuwa anaishi kihalali.Huyu ni wale watumikia kafiri ili apate mradi wake.
 
Last edited by a moderator:
ccm imezeeka na wazee wake, nashangaa vijana wajuzi akina mwigulu na January na akina ridhiwani wanaweza kudhihaki maneno ya wazee kama hao.
ngoja tusubiri kama kuna kijana wa CCM atanyenyua mdomo wake kumdhihaki huyu mzee baada ya kuwapa za uso.
 
Hata kwetu wapo kama wewe ila tunajuwa namna ya kuishi nao..

1. Suala la rushwa hilo lipo wazi JK alisema mara kadhaa lakini kasema huyu leo ndo mnaona kama jipya vile
2. Hivi zile hati chafu za halmashauri mbalimbali huwa inakuwaje..??
3. Na wafanyakazi hewa je..??

Mkuu wewe kweli una roho ngumu. Yaani Umeenda kwe kilabu cha pombe unamkuta mlevi chakali alieshindwa hata kumalizia pombe yake halafu unampeleka darasani unaanza kumfundisha ataelewa kweli.Mkuu hiyo hekima yako usiipoteze bure.
 
bandiko hili lisiondilewe hadi nnape alisome uone atakuja na jb gani.....hataacha kusema" hawa wazee wanasubiri kufa' utadhani yeye ataishi milele. hongera nnape.
 
ngoja tusubiri kama kuna kijana wa CCM atanyenyua mdomo wake kumdhihaki huyu mzee baada ya kuwapa za uso.
Wewee, we unaongea nini wewe. Ulishawahi ona wapi mtoto wa jambazi, malaya au mchawi akamkana mzazi wake?
hahaha, nyie watu wasahaulifu kweli, ni juzi tu hapa mmesahau warioba na team yake walivyotukanwa na hao hao vijana akina nape, January na Ridhiwani?? mkuu Nguruvi3 njoo unisaidie kuwakumbusha hawa,
vijana wa CCM hawana soni yakutukana wazazi wao, narudia tena soni hawana ng'oooo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom