Butiku, Kitine, Kaduma, Salim, Warioba, wana nguvu?

Mama Porojo,
Punguza porojo zako. Butiku alikuwa Private Secretary wa Mwalimu mpaka Mwalimu anaondoka mamlakani. Mwinyi akamwomba amsaidie pale Ikulu wakati alipoingia na Butiku amekaa na Mwinyi kwa miaka miwili kama Private Secretary wake. Baadaa ya hapo kwa sababu Mwalimu alikuwa anapata wageni wengi pale Butiama akamwomba Mwinyi amruhusu Butiku kuwa mkuu wa mkoa wa Mara pale Musoma ili aweze kumsaidia Mwalimu na wageni wake wanapokwenda kumtembelea Butiama. Butiku alikuwa mkuu wa mkoa mpaka pale Mwalimu alipoanzisha Nyerere Foundation akamchukua kumsaidia pale. Aliyemteua Butiku kuwa mkuu wa mkoa Mara ni Mwinyi na wala si Mwalimu.

Ni Butiku ndio aliefilisi mfuko wa mwalim Nyerere Foundation,amekula pesa za wafadhili waliokuwa wanatoa kuuendeleza mfuko huo sasa anatafuta huruma ya watanzania.kama kweli alikuwa mzalendo sana,ameifanyia nini tanzania kwa nafasi alizowahi kushika ikiwamo hiyo ya ukuu wa mkoa.mwizi tu huyo.
 
Hiyo ni issue nyingine. Kama unataka kuzungumzia Nyerere foundation anzisha thread yake tutachangia huko. Hapa tunazungumzia uhalali wa wazee hawa kuikosoa CCM.
 
Hapana,
Kitine hakuondolewa ukuu peke yake. Aliondolewa pia Augustine Mahiga na Nimrodi Lugoe. Kilichowaondoa pale kwa hivi sasa sikumbuki lakini Kitine hakuondolewa peke yake. Kuhusu mke wake Kitine hakuandaa nyaraka feki. Kitine alipomaliza masomo yake Canada aliamua kurudi nyumbani na mke wake akabaki Canada. Kulikuwa na tetesi wakati huo kuwa huenda wakaachana kwa sababu Kitine alirudi nyumbani na watoto wote. Mkewe alikuwa na tatizo la migraine kwa muda mrefu na alilitumia hilo kumwomba mumewe amtafutie hela za matibabu. Kitine was as much a victim kwa sababu hakujua kuwa mke wake alikuwa na mipango ya kutumia hela hizo kwa malengo tofauti.

kwa hiyo unataka kueleza nini mbona naona umachi know lakini unaruka ruka,kama hakuondolewa peke ake ina maana alikuwa pamoja na wenzake kitu ambacho hakiondoi ufisadi wake.naona unaongeza maelezo bila kujua mkuu
 
By Jasusi Hapana,
Kuhusu mke wake Kitine hakuandaa nyaraka feki

mkuu,upo dunia ipi wewe,hukumbuki kuwa ni kitine ndio aliyeomba huruma kwa wabunge wakubali serikali imlipie deni mke wake baada ya kubainika alidanganya?hebu kumbuka vizuri mkuu.huyu ni adui mkubwa wa taifa hili ila amejificha kwenye ngozi ya kondoo,kwa wasiomfahamu watadanganyika na porojo zake za mfa maji.
 
Tamachungu,
Uchunguzi ulifanywa na bunge na Kitine alilazimika kuzilipa zile $60,000. Alikatwa kwenye mshahara wake. Hakuandaa nyaraka feki. Mkewe alimdanganya na huo ndio ukweli. Kitine has paid the price na kama hujawahi kuoa basi huwezi kuelewa majanga ambayo wake zetu wanaweza kutuingiza.
 
Hiyo ni issue nyingine. Kama unataka kuzungumzia Nyerere foundation anzisha thread yake tutachangia huko. Hapa tunazungumzia uhalali wa wazee hawa kuikosoa CCM.

jasusi,wewe unafikiria kwa kutumia tumbo lako wakati taifa linaangamizwa na hawa wazee,butiku hadi leo hana mahusiano mazuri na familia ya mwalim kwa ufirauni wake..
amekuwa katibu wa mda mrefu wa nyerere lakini historia inaeleza kuwa alinyanyasa sana wafanyakazi waliokuwa chini yake,alikuwa mungu mtu,mbabe asiependa kuwashirikisha sub ordinate wake.labda umevaa miwani ya mbao ndio maana hukupata kuyaona haya
 
Huwezi kuniambia lolote ambalo sijui kuhusu familia ya Mwalimu na Butiku. Lakini usituondoe kwenye mada. That is all I am saying. Tunazungumzia haki ya hawa wazee kuikosoa CCM. Tujukite huko kwa sasa.
 
Tamachungu,
Uchunguzi ulifanywa na bunge na Kitine alilazimika kuzilipa zile $60,000. Alikatwa kwenye mshahara wake. Hakuandaa nyaraka feki. Mkewe alimdanganya na huo ndio ukweli. Kitine has paid the price na kama hujawahi kuoa basi huwezi kuelewa majanga ambayo wake zetu wanaweza kutuingiza.

bro mimi nina mke na nina watoto,kudanganywa na mkeo hakuwezi kutufanya sisi tukuone we ni msafi kiasi hicho,hiyo ni failure kubwa sana kwa kiongozi kama yeye.kama mke wake amemshinda,atawaeleza watanzania kipi kizuri uzeeni mwake wamwamini?????isingekuwa membe si angetuibia?????kama mke wake ni muongo,atakuwa ametudanganya mangapi ambayo hatujayaona na kuyajua mkuu,tuwe critical kidogo.
 
Tamachungu,
Huwezi kuniambia lolote ambalo sijui kuhusu familia ya Mwalimu na Butiku. Lakini usituondoe kwenye mada. That is all I am saying. Tunazungumzia haki ya hawa wazee kuikosoa CCM. Tujukite huko kwa sasa.

kama sio waropokaji kwa nyadhifa zao walizowahi kushika kwanini wasizitumie kukaa na watawala watoe maoni yao.

kuna msemo kichaa akiokota nguo zako,nawe ukamfukuza ukiwa uchi,ina maana wewe ndio kichaa zaidi,sasa hawa wazee wana tofauti gani na huyu aliemkimbiza kichaa akiwa uchi?????
 
Kitine hajawahi kufanya kazi ubalozi Canada. Alikuwa masomoni Vancouver na ubalozi uko Ottawa. Membe amepelekwa ubalozi Canada wakati Kitine amesharejea Tanzania baada ya kumaliza Phd yake.

tueleze kwa nini alifukuzwa kurugenzi mkuu wa usalama wa taifa.kwanini aliondolewa ubalozini.yule ni mwizi lakini kwa kuwa wewe ni ndugu yake huwezi kuona mapungufu yake.
 
Tamachungu,
Huwezi kuniambia lolote ambalo sijui kuhusu familia ya Mwalimu na Butiku. Lakini usituondoe kwenye mada. That is all I am saying. Tunazungumzia haki ya hawa wazee kuikosoa CCM. Tujukite huko kwa sasa.

kama kweli yeye ni mzalendo na ana uchungu na nchi hii kwanini ameinyanyasa familia ya mwalim?kwanini amefilisi mfuko wa mwalim Nyerere foundation,kabla ya kumnyoshea mwenzako kidole hakikisha wewe ni msafi
 
kama sio waropokaji kwa nyadhifa zao walizowahi kushika kwanini wasizitumie kukaa na watawala watoe maoni yao.

kuna msemo kichaa akiokota nguo zako,nawe ukamfukuza ukiwa uchi,ina maana wewe ndio kichaa zaidi,sasa hawa wazee wana tofauti gani na huyu aliemkimbiza kichaa akiwa uchi?????
Kama unafuatilia mada hapa JF, Butiku amewahi kuwaandikia wote Mkapa na Kikwete juu ya matatizo ndani ya CCM. Mpaka leo hajajibiwa. Sasa watakaaje na watawala watoe maoni yao kama watawala hata hawataki kuwasikia sembuse kuwaona? Actually unachotetea hapa ni kitu gani? CCM haina matatizo? CCM haijakosa mwelekeo? Wameropoka kitu gani? Hebu tujikite kwenye message yao badala ya ku shoot the messenger.
 
Mnapotoshwa!

wewe tunakujua ni kibaraka wa kitine ndio mfanyakazi wake wa ndani lazima umtetee boss wako lakini ipo siku ukiujua ukweli lazima utoke huko kwa mayowe.

hili ni jukwaa huru,hakuna mtu anyepotosha,kama wewe una facts weka hapa tupime ukweli ni upi kati yako na huyo mwingine,ukisema mnapotoshwa wakati wewe unakula posho zinazotokana na kodi zetu lazima tukutilie shaka
 
tueleze kwa nini alifukuzwa kurugenzi mkuu wa usalama wa taifa.kwanini aliondolewa ubalozini.yule ni mwizi lakini kwa kuwa wewe ni ndugu yake huwezi kuona mapungufu yake.
Nimeshasema kuwa sijui kwa nini Kitine, Mahiga na Lugoe waliondolewa pale usalama wa taifa. Nimesema pia kuwa Kitine hajawahi kufanya kazi ubalozini. Na kuna mwingine hapa jukwaani ameniunga mkono akataja na balozi aliyekuwa Canada wakati huo. Nimesema Kitine alikwenda Canada, Vancouver, kwa masomo ambako alipata Phd. Mimi si ndugu yake. Mimi natoka Mara na Kitine nadhani anatoka Iringa. Tujikite zaidi kwenye issue badala ya personalities.
 
wewe tunakujua ni kibaraka wa kitine ndio mfanyakazi wake wa ndani lazima umtetee boss wako lakini ipo siku ukiujua ukweli lazima utoke huko kwa mayowe.

hili ni jukwaa huru,hakuna mtu anyepotosha,kama wewe una facts weka hapa tupime ukweli ni upi kati yako na huyo mwingine,ukisema mnapotoshwa wakati wewe unakula posho zinazotokana na kodi zetu lazima tukutilie shaka

Ndugu yangu haya ya kuitana majina hapa JF hayana tija. Siwezi kuwa kibaraka wa Kitine kwa sababu hata yeye hatufahamiani kiasi hicho. Huenda tumekutana mara moja mara mbili maisha yetu yote. Nimekuwekea facts wewe unarejea matusi. Na posho ninayokula ni kwa jasho langu mwenyewe hata wale wanaonifahamu hapa JF watakuwa mashahidi wangu wa kwanza.
 
Kama unafuatilia mada hapa JF, Butiku amewahi kuwaandikia wote Mkapa na Kikwete juu ya matatizo ndani ya CCM. Mpaka leo hajajibiwa. Sasa watakaaje na watawala watoe maoni yao kama watawala hata hawataki kuwasikia sembuse kuwaona? Actually unachotetea hapa ni kitu gani? CCM haina matatizo? CCM haijakosa mwelekeo? Wameropoka kitu gani? Hebu tujikite kwenye message yao badala ya ku shoot the messenger.

kwanza kabisa tukubaliane kwamba ni waropokaji then tukae chini kujadili walichokisema.

1.ukitoa ushauri mara moja haukufuatwa ndio uchague kuwa mropokaji???
2.kwa nini kitine alifukuzwa usalama wa taifa kama DG
3.kwanini kitine alidanganya bunge kuwa mke wake alikuwa anatibiwa ili aibe kodi zetu.
4.kwanini familia ya Nyerere inamuona butiku ni mbwa
b.kwanini butiku ameitelekeza familia ya Nyerere wakati ameishi na mwalim maisha yake yote kama private secretary wake na istoshe wanatoka sehem moja.
5.kwanini kama viongozi wakuu wastaafu wa serikali wameshindwa kutumia vikao kufikisha ujumbe wao.
hata kama ni mabwana zako lazima tuwe objective ili tujenge taifa la watu wawajibikaji.
 
Ngoja nikujibu moja baada ya jingine.
1. Nini maana ya mropokaji kwa mtazamo wako.
2. Nimeshakwambia kuwa sikumbuki kwa nini "walifukuzwa" kutoka usalama wa taifa. Point hapa ni kwamba Kitine hakuwa peke yake. Alikufuzwa pamoja na wenzake wawili.
3. Kitine hakudanganya bunge kwa sababu fedha zilitolewa na wizara ya afya na si bunge.
4. Sijawahi kusikia popote pale kwamba familia ya Nyerere inamwona Butiku ni mbwa. Kama wewe umesikia tueleze unachojua juu ya hilo.
b. umesema Butiku ameitelekeza familia ya Nyerere. Hujasema ameitelekeza kwa vipi. Makongoro, Madaraka, Magige, Rose, Anna na Andrew wote ni watu wazima. Sasa ulitaka Butiku awafanyie nini? Mama Maria is well and healthy akiwa Msasani au Butiama. Unataka Butiku afanye nini kuonyesha kuwa wako karibu. Eleza wewe.
5. Nimeshakujibu kwamba wameandikiwa barua Mkapa na Kikwete wakachunia. Sasa unataka hawa wazee wakae kimya tu wakati wanaona mambo ndani ya chama chao si shwari?
Naongezea namba 6. Punguza matusi ukumbini. Tujikite kwenye hoja badala ya viroja.
 
Hivi hao wazee hakuna utaratibu wa kichama wa kuisaidia chama badala ya kwenda direct kwenye vyombo vya habari?

Hivi wamenyimwa fursa za kuonana na Mwenyekiti, katibu wa chama chao?

JK ambaye anaweza kuonana na kila mtu atashindwa kuonana na hao wazee (NAY)..

Nafikiri wana agenda zao kibindoni..
 
Topical,
Nimewahi kuzungumza na Butiku na alisema alishawaandikia wote Mkapa na Kikwete barua. Wote hawakumjibu. Aliwahi kuomba akutane na Mkapa alipokuwa mamlakani, akamchenga. Ameomba kukutana na Kikwete, yale yale. Sasa ajabu, juzi baada ya Vincent Nyerere kumvua nguo Mkapa hadharani, ndipo Mkapa kwa mara ya kwanza amemtafuta Butiku, eti asaidie kumpatanisha na Vincent. Lakini kama ni suala la kukutana, Butiku ametumia kila njia bila kufanikiwa.
 
Back
Top Bottom