Butiku, Kitine, Kaduma, Salim, Warioba, wana nguvu?

kama kweli ccm ni mbaya na inakufa warudishe kadi wazee hao wakipata posho hawakosekani vikao vya ccm pia tuliona Sura zao siku jk alipozungumza na wazee wa dar es salaam wakiwa miongoni mwa wazee wakitikisa vichwa kuonyesha kuguswa na hotuba ya jk unafiki mkubwa huu.
 
Jibu hoja usituletee matusi ya kikwere hapa; kama baba yenu kazi imemshinda ndio maana kila mtu anataka kuwa Rais kwanini asiambiwe?


kitine hawezi kusimama mbele za watanzania kusemea maovu wakati yeye mwenyewe ni mchafu aliepituka.kwa nini alighushi vyeti ili mke wake akatibiwe india mwizi yule
 
hawa hawa ndio waliomkwamisha Mwl Nyerere katika utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya watanzania.
 
Mlisubiri nini siku zote kuweka udhaifu wao hadharani? Au ndo ugali chali mnakimbilia kumwaga bakuli la mboga????humu tunahitaji hoja kwa hoja!!
 
Bunge liliamua kwamba Kitine arudishe fedha zetu milioni 60 alizotudanganya katika matibabu hewa ya mke wake ambaye alikuwa haumwi na wala hakumpeleka canada kwa matibabu. Je, Kitine alirudisha fedha hizo hajawahi kutuambia wala kuomba radhi kwa kutuibia lakini pia hajawahi kujutia kitendo hicho cha kifisadi na kama mzee huyu asingelazimishwa kujiuzulu uwaziri angekuwa amekomaa kwenye nafasi ya ufisadi
 
kwa nini wasiende kuyasemea mawazo yao haya kwenye vikao,naamini kwa nafasi walizowahi kushika hawangeshindwa kuomba apointment kwa curent leaders
 
inasikitisha kwa mzee kama Kitine ambaye alishika ukurugenzi wa taasisi nyeti hapa nchini kuropoka majukwaani badala ya kutumia vikao kutoa maoni yake.
 
Naskia Kitine ni mzee wa totoz mbaya kabisa,ametelekeza mtoto wake mmoja sasa analelewa na bibi yake huko Tanga.alimzaa akiwa mkuu wa mkoa huo.
 
ukitaka kujua taarifa chafu za kitine kamuulize membe ndiye alimlipua bungeni baada ya kugushi matibabu hewa ya mkewe ni kitine alikuwa boss wa membe TISS na pia kitine alipokuwa balozi canada membe alikuwa afisa ubalozi canada bila membe madudu ya huyu mzee tusingejua kila mtu aliogopa eti kwa sababu alikuwa mkurugenzi wa TISS
Mama Porojo kama jina lako! Wakati wa sakata la mke wa Kitine,balozi wetu Canada alikua Fadhil Mbagga! Naona hizi stori umesimuliwa,yawezekana ulikua bado mdogo ama haujafika mjini!
 
salaam wakuu.

Kitine Akiwa mkuu wa mkoa wa Tanga alitumia madaraka yake vibaya kwa kuandaa nyaraka feki ili mke wake asafirishwe kwenda Canada na alipiwe gharama za matibabu na serikali ya Tanzania.

taarifa za wadadisi wa mambo zinasema kuwa Alifukuzwa Ukurugenzi Mkuu wa usalama wa taifa (UWT) baada ya miaka miwili tu, na kwamba ni yeye pekee aliekaa madakarakani ktk nafasi hiyo kwa kipindi kifupi sana kuliko wakurugenzi wote waliowahi kushika nafasi hiyo nyeti hapa nchini.chanzo cha kufukuzwa inaelezwa ni Ufisadi na alitaka kulisaliti Taifa kwa maadui.
KITINE ni mwizi wa mali za watanzania na ni mtu mwenye gubu katika roho yake.

My take:Je ni kweli huyu jamaa ana ujasiri wa kutosha kujitpokeza na kuwaambia watanzania kuwa chama cha magamba kinakufa kufa? ni mzalendo wa kweli?

Hapana,
Kitine hakuondolewa ukuu peke yake. Aliondolewa pia Augustine Mahiga na Nimrodi Lugoe. Kilichowaondoa pale kwa hivi sasa sikumbuki lakini Kitine hakuondolewa peke yake. Kuhusu mke wake Kitine hakuandaa nyaraka feki. Kitine alipomaliza masomo yake Canada aliamua kurudi nyumbani na mke wake akabaki Canada. Kulikuwa na tetesi wakati huo kuwa huenda wakaachana kwa sababu Kitine alirudi nyumbani na watoto wote. Mkewe alikuwa na tatizo la migraine kwa muda mrefu na alilitumia hilo kumwomba mumewe amtafutie hela za matibabu. Kitine was as much a victim kwa sababu hakujua kuwa mke wake alikuwa na mipango ya kutumia hela hizo kwa malengo tofauti.
 
ukitaka kujua taarifa chafu za kitine kamuulize membe ndiye alimlipua bungeni baada ya kugushi matibabu hewa ya mkewe ni kitine alikuwa boss wa membe TISS na pia kitine alipokuwa balozi canada membe alikuwa afisa ubalozi canada bila membe madudu ya huyu mzee tusingejua kila mtu aliogopa eti kwa sababu alikuwa mkurugenzi wa TISS
Kitine hajawahi kufanya kazi ubalozi Canada. Alikuwa masomoni Vancouver na ubalozi uko Ottawa. Membe amepelekwa ubalozi Canada wakati Kitine amesharejea Tanzania baada ya kumaliza Phd yake.
 
enzi za butiku alikuwa anashika fuko la fedha za mwalimu ikulu. nyerere hakuwahi kutembea na fedha ya ofisini ktk shughuli zote za kikazi ni butika alitoa fedha kwa maelekezo ya nyerere. fuko hilo lilimpa kiburi akatumia nafasi hiyo ya kutoweza kumfikia mwalimu bila butiku kutembea kizembe na akina dada wa ikulu kwa idadi kubwa hadi ndoa yake ikavunjika mke wake akambilia nje ya nchi hadi leo kwa kashfa hizo. kwa sababu ya kukosa uaminifu ktk mambo ya fedha na uzinzi mwalimu akasikia habari zake akamwondoa ikulu akampeleka kuwa mkuu wa mkoa wa mara.
Mama Porojo,
Punguza porojo zako. Butiku alikuwa Private Secretary wa Mwalimu mpaka Mwalimu anaondoka mamlakani. Mwinyi akamwomba amsaidie pale Ikulu wakati alipoingia na Butiku amekaa na Mwinyi kwa miaka miwili kama Private Secretary wake. Baadaa ya hapo kwa sababu Mwalimu alikuwa anapata wageni wengi pale Butiama akamwomba Mwinyi amruhusu Butiku kuwa mkuu wa mkoa wa Mara pale Musoma ili aweze kumsaidia Mwalimu na wageni wake wanapokwenda kumtembelea Butiama. Butiku alikuwa mkuu wa mkoa mpaka pale Mwalimu alipoanzisha Nyerere Foundation akamchukua kumsaidia pale. Aliyemteua Butiku kuwa mkuu wa mkoa Mara ni Mwinyi na wala si Mwalimu.
 
wazee hawa ni majeruhi kelele zao si za uzalendo ni kelele za kusahauliwa kwenye maamuzi na kuwekwa pembezoni.wakirudishwa watakaa kimya mathalan warioba si yule wa mwaka juzi kasogezwa jikoni. warioba anaandamwa na kashfa ya kampuni ya madini ya mwananchi bado tunahitaji maelezo kwa kina anatuhumiwa kuchota mamilioni. warioba aliondolewa na mwinyi ktk nafasi ya waziri kwa sababu alikuwa hatoshi na kumweka john malecela. akiwa waziri mkuu wetu ni nini tunachokumbuka alifanya kwa ajili ya kukumbuka utumishi wake huo mkubwa?
Kuhusu kampuni ya Mwananchi mbona Kikwete ameogopa kumfungulia Warioba mashtaka? Utakapojua ukweli wa jambo hili utatambua jinsi Kikwete alivyo janga kuu kwa taifa.
 
Back
Top Bottom