Sidhani kama ni jambo baya CHADEMA kupewa fedha na wahisani. Nchi hizi ni wafadhili na wanatupa misaada mingi, hivyo ni lazima wahakikishe kuwa kunakuwa na demokrasia na utawala bora. Nothing new.
Hii hoja ilishakua takataka kitambo sana, kwani kufadhiliwa dhambi?
Nchi inafadhiliwa, yeye anafadhiliwa, kigoda cha mwalimu kinafadhiliwa, mama abduli anafadhiliwa na kina GSM, Habith Singh, Rostam, na mafisadi wengine lukuki tena hadharani tu, abduli pia anafadhiliwa, sisiemu inafadhiliwa, jekee anafadhiliwa, mwigulu anafadhiliwa pia, napi anafadhiliwa, nchi nzima makanisa, misikiti, mahospitali, mikoa na wilaya, halmashauri, masoko taasisi mbalimbali hata watu mmojamoja wanafadhiliwa kwa njia mbalimbali au wanajiona wao wana hatimiliki ya kufadhiliwa!
Na hizo fweza chadema wanaletewa na mabeberu kwa mifuko ya sandarusi kama jekee na timu yake walivyochota za Escrow ya IPTL kule Stanbic? Na wakati wanazipitisha chawa wa mama wanakua wapi? Wanapitisha airport? Bandarini kama kago? Au kwa ungo wa kalumanzila? na kina wambura na kingaye na kina Muliroo wanatazama tu?
Wakifadhiliwa wengine wanaumwa? Maumivu yakizidi si wakawaone wachawi wao? Tunguli si zipo?
Hebu watupumzishe sasa, watanzania sio wajinga tena