Labda ni misunderstanding.
Mzee Butiku yeye binafsi ana msimamo gani kuhusu muundo wa serikali ya muungano? Maoni ya wananchi siyo lazima yawe maoni ya wanatume kwa binafsi yao.
Nadhani ndiyo alichomaanisha, kwa sababu aliulizwa kama yeye anataka serikali tatu.
Vilevile siyo kama Warioba anataka serikali tatu, ila kwa maoni yake ni kuwa wananchi wanataka serikali 3.
Mimi ningependa kuwe na refferrendum kwanza, na kama muungano utatakiwa na pande zote basi tuwe na serikali moja. Zanzibar nayo ife.
"Not to decide is to decide" kutotoa maoni, ni uamuzi na una uzito wake sawa na kutoa maoni. Kwa hiyo kama asilimia themanini ya waliotoa maoni hawakuzungumzia kabisa muungano, hii inamaanisha hawajali muungano utakuwa wa aina gani.
Bunge la katiba linaweza likachukulia hiyo kama ni mandate ya kuamua mfumo wa muungano. Na baadae kuuleta kwa wananchi ambao, chini ya tume huru ya uchaguzi wataamua kukubali au kukataa.
Halafu tuache unafiki, jeshi kutwaa madaraka ni mfano uliotolewa kama mojawapo ya kutokuwa na serikali inayoweza kukusanya mapato, au kuwa na vyanzo vya mapato. Ila nashangaa watanzania tumeutwist ujumbe huo.