Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wakuu
Wananchi wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara wamejikuta wakinusuru fedha zao kwaajili ya bajeti ya kitoweo cha sherehe ya sikukuu ya kuchinja ‘Eid al-Adha’ baada ya Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini kuchinja Ng’ombe zaidi 500 na kuwagawia.
Tukio hilo limetokea mapema leo Juni 7, 2025 hatua inayotajwa kuwawezesha wananchi hao bila kujali dini zao wanaungana na wenzao ulimwenguni kusherehekea Eid.
Akizungumzia tukio hilo lililoandaliwa nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Butiama kwa niaba ya mbunge huyo, Ofesa Mahusiano kutoka ofisi ya Mbunge, Japheth Changalawe amesema Ng’ombe hao 500 wametolewa na marafiki zake kutoka nchini Uturuki.
Amesema hatua hiyo ni ishara ya mshikamano baina yake na marafiki wa nje, viongozi na wananchi na kunaonesha namna tunavyothamini ibada, amani na undugu katika jamii.
Aidha, amesema Ng’ombe hao wamegawanywa kwenye vitongoji 370 na taasisi zote za umma na binafsi zilizopo katika jimbo hilo, kwa ajili ya kitoweo kwa wananchi kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Eid Al-Adha.
Ugawaji wa sadaka hiyo umefanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia jana na leo, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuonesha moyo
wa upendo na mshikamano wa Mbunge Sagini kwa wananchi wa jimbo hilo.