'Busu' lamtia mashakani Obama

'Busu' lamtia mashakani Obama

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,105
Reaction score
34,926
ko
141022103303_obama_kiss_512x288_bbc_nocredit.jpg

Obama akibusu Cooper

Rais wa Marekani, Barack Obama, ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu.

"rais tafadhali usimguse mpenzi wangu," alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones.
Yote hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper.
''Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo,'' alisema Rais Obama , huku akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko.
Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake.
Obama alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa ,''hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu,''
Baada ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuongea.Chanzo.http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/…/141022_obama_busu

Rais Obama afuata Mkondo wa njia ya Rais wa Zamani wa Marekani MR Bill Clinton haahahahah kazi kweli ipo Amerika.

 
Back
Top Bottom