Michelle akiri kuvuta bangi na 'boyfriend' wa ujanani kabla ya kukutana na Barack Obama

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,512
2,730
Michelle Obama ametoa siri zake nyingi katika kusanyiko la matukio katika maisha yake kwenye kitabu chake cha "Becoming"
Kwenye kitabu hicho, Michelle anasimulia mambo mengi kuhusu maisha yake ikiwemo jinsi alivyovuta bangi akiwa na umri wa miaka 16.
Hata hivyo, Michelle hakuzamia suala hilo kwa undani na huenda ndiyo sababu iliyomsukuma mtangazaji wa ABC News Robin Roberts kumuuliza sababu yake kujumuisha ujumbe huo katika kitabu chake.

Akimjibu Roberts, Michelle alisema hakuona haya kwa kuwa ujumbe huo ni sehemu ya kisa chake hadi leo na hivyo hakuona umuhimu wa kuuficha.
Anamtaja mpenzi wake wa shule ya upili aliyeitwa David na kusimulia jinsi walivyovuta bangi pamoja wakati "wakirusha roho"

"Hivyo ndivyo nilivyofanya ," alisema Michelle.
"Hiyo ni sehemu ya kisa kizima cha maisha yangu. Kila mtu ana jambo alilotamani kuelewa. Kwa nini nilifiche langu kwa kizazi kijacho? ," aliongeza.

Kura ya maoni ya hivi majuzi ilionyesha kuwa zaidi ya nusu ya raia wa Marekani wametumia bangi wakati mmoja maishani mwao.
Mumewe Michelle, Barack Obama, alihudumu kama Rais wa 44 wa Marekani kati ya mwaka 2008-2016.
Kwenye kitabu chake cha Dreams from my Father , Obama anasimulia jinsi alivyotumia bangi na dawa zingine za kulevya alipokuwa kijana.
 
Michelle amesoma na kuhitimu Havard university tena kwa wastani mzuri best kitivo cha sheria lkn alikuwa mvuta bangi

Obama kasoma havard ila naye kakiri alikuwa mvuta bangi mzuri kipindi yupo college

Halafu kuna watu wana criticize bangi inasababisha ukichaa,haifai wakati imezalisha marais.
 
Michelle amesoma na kuhitimu Havard university tena kwa wastani mzuri best kitivo cha sheria lkn alikuwa mvuta bangi

Obama kasoma havard ila naye kakiri alikuwa mvuta bangi mzuri kipindi yupo college

Halafu kuna watu wana criticize bangi inasababisha ukichaa,haifai..
Mkuu unataka kusema nini hapa kuhusu matumizi ya bangi? Ila yapo majimbo kadhaa ndani ya Marekani yameruhusu wananchi wake kutumia bangi, huwa najiuliza nasema yenyewe sio kali kama kitu cha arusha nini?
 
Dah unajaribu kusema unachojua au unataka kupingana na maelezo yangu? Nazungumzia usmart siyo kilimo cha kutegemea moshi wa bangi.
Mkuu mimi sijapingana na maelezo yako, nimejaribu kujazia nyama hoja yako kwa mfano wa eneo tofauti, yani bangi inaweza kuifanya akili ikawa sharp zaidi au ku stimulate misuli mtu akafanya kazi za kutumia nguvu zaidi.
 
Tatizo la wabongo wanataka kufananisha high class ya bangi wanayovuta Obama, na makushabu ya hapa!....aaah wapi lazima bangi ikubangue!
Hiyo high class inakuwa imeongezewa ingredients zozote zile tangu itoke shambani au ndio inakuwa natural kama kitu kutoka meru hapa nchini.
 
Sawa sawa.
Mkuu mimi sijapingana na maelezo yako, nimejaribu kujazia nyama hoja yako kwa mfano wa eneo tofauti, yani bangi inaweza kuifanya akili ikawa sharp zaidi au ku stimulate misuli mtu akafanya kazi za kutumia nguvu zaidi.
 
Huku Afrika watu wanaficha historia zao "mbaya" tunaambiwa alijisomea sana kemia, kwenye harusi yake alikula matango na mihogo ya kuchoma, blah.....mara huyu hapa kawa kaka mkuu!.....
Inawezekana watu wanachoma mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom