Business ideas (Bure)

Safi.
Aise, mimi nimependa idea ya No 3 Car wash.
1. Nafahamu nahitaji kwanza eneo
2. maji (kisima, maji ya bomba) ....... (sijapata bei ya uchimbaji kisima)
3. Vijana wa kuosha magari (hawa watalipwa kulingana na kazi)
4,. .....motor na pump ile wanatumia ku- fasten maji - jina sahihi sijafahamu (sijui bei yake)
5. generator kwa ajili ya umeme (best, cheap and efficient generator sijazifahamu
6. kujenga eneo la kuoshea gari
7. Variable costs (hizi nafikiri si kubwa soap, vitambaa vya kuoshea, ving'arishi.......)

Nimetaja vile ambavyo nimekuwa naviona kwa waoshaji, ndio maana hata majina ni kama nimeyataja bila usahihi sana.

Tafadhali, kama unafahamu vya kutosha biashara hii nimeipenda na ninapenda kuifanya licha ya kuwa sina fedha kwa sasa ila najipanga.






Wakuu nimekuwa nikifuatilia JF kwa muda mrefu sana, tangu enzi hizo inaitwa JamboForums mpaka JamiiForums. Nimeona watu wengi walivyo na muamko wa biashara ili kuongeza kipato sababu mishara ya kazini haitoshi. Lakini kikubwa nimeona watu wanavyoumiza kichwa kujua nini wafanye, wengi wamekuwa waigizaji au copycat. Kwenye biashara kuna watu wa aina tatu Innovator, imitator and ------, hivyo try to be innovator.

Ok enough of blah blah. Mpango wangu katika post hii ni kuainisha biashara 6 ambazo mtaji wake ni less than 10,000USD exclude a working capital.

1. Food Processing and Packaging: (The truth ni kwamba agro product zetu hazipo kwenye mashelf ya supermarket za dar sababu the packaging sucks. Nilinunua bottle ya mbilimbi pickles, yaani product is taste lakini the package ni aibu. Biashara yoyote inayohusu chakula una potential ya kuikuza at least by 15% annual. Food ambazo unaweza process includes Maharage, mahindi mabichi, samaki, njegere, mchicha na nyingine nyingi. Sio lazima kutengeneza pilipili everybody is doing it.


2. Maize and Rice Milling: Najua hapa wote mtasema oooh Azam na Jogoo wameshika soko, guess what kuna at least 20% ya market share ambayo ni nobody territory. Unachotakiwa ni kujitofautisha (Differentiation Strategy) na Azam na Jogoo.

Here is how:

(a) Kiwango (Quality), hakuna atake nunua unga wako kama ukikaa ndani unaoza,

(b) Urahisishaji (convenience) hapa sio kwenye price bali kwenye packaging, funga katika ujazo wa 1/2KG, 1KG, 2KG, 5KG na 10KG. Zama za mizani zimekwisha.

(c) Bei shindani (competitive price), kumbuka zama za kulopoka kwamba kilo 1,000 zimekwisha. Have all the facts behind your numbers, jua gharama za uzalishaji (Direct Cost & Indirect Cost), pricing is an art sio kulopokwa tuu sababu everybody is selling 1,000 basi na wewe 1,000.


3. Quick Car Wash,Tire Repair, Oil and Lubes: Kila mtu anaona magari yanavyongezeka Tanzania, the good news ni kwamba this is nothing in the next 10 years idadi will double. Means kwamba opportunity and opportunity for entrepreneur. Nimeita quick sababu quickness ndio inakutofautisha na wachaga walio na sehemu hizi.

Kumbuka we are not trying to bring new business into the market we're either changing the process or improve the service that's it. So, hapa unaitaji air compressor ya mid size, hydraulics car jack za ukweli sio vile vijeki mshenzi ambavyo lazima utumie msuli. Remember quickness here at least 10 minutes mtu hayupo.


4. Bakery, fast food restaurant and Pizza Place: Tanzania sasa imeamka jamani sio miaka ya 1980s ambapo watu walikuwa wananua maandazi ya kufunga na gazeti, watu sasa wanataka good product, well packed and delicious. Cha muhimu hapa ni location, ukienda kufungua hii venture kigogo huko au kwetu kimanga am sorry no one will recognize it.

Angalia location and target "middle income consumer" wanaojifunga tai na michuchumio ( facebook/twitter generation). Hapa pia kumbuka quickness is a key, watu wanajaribu kuishinda foleni, so no one will give you 20mins umfungie maandazi.


5. Mobile entertainment: Hapa kama una ujuzi wa kuwaza unaweza kutengeneza pesa mpaka basi. Over 20% ya Watanzania ni watoto 12years and younger. Means kwa dar tuu wapo watoto zaidi ya laki 6. Kila mdada anajaribu biashara ya kuleta bounce house kwenye birthday za watoto, that is so 1960s. Watoto wa siku hizi wapo 9 hours ahead, fikiria outside the box. Kumbuka hi St. Majanga zote zilizojaa dar ukiwa na good mobile entertainment idea you will partner with all of them. This is pure money...

6. Mobile Fast Food Restaurant: Wenyewe mnaona jinsi KFC au subway zinavyojaza au container pale morocco, lakini hawa wote ni "brick and mortar" hawewezi kuwafata wateja posta, coco beach. Wewe unafanya mapinduzi, kumbuka business is always about revolution if you evolve yatakupata ya Blackberry.

Kama una idea nyingine weka hapa, zama za kuamini kwamba idea yako watu wataichukua is nonsense, sababu wewe unaijua idea yako kushinda mtu mwingine. Kama mimi all those 6 are my ideas. Let soko liwe jaji.

Mungu akijalia wakati mwingine nitaandika tumia social media to make miracle in your business. Na hapa you will see how facebook, twitter, blogs can make revolution for your business. Remember we do not bring anything new in the market, we are either change, process au improve service.
 
Ndugu zanguni nimefarajika kwa elimu yenu juu ya masuala ya biashara,naombeni mnisaidie ninae rafiki yangu ana kiwanda cha kutengeneza mifuko ya magunia ya cotton,kikubwa ama changamoto ni masoko nawaombeni msaada wenu kwa huko.
Ahsanteni
 
Ndugu zanguni nimefarajika kwa elimu yenu juu ya masuala ya biashara,naombeni mnisaidie ninae rafiki yangu ana kiwanda cha kutengeneza mifuko ya magunia ya cotton,kikubwa ama changamoto ni masoko nawaombeni msaada wenu kwa huko.
Ahsanteni

Mkuu jee mmeshafanya mchanganuo (analysis) ya kwamba mmnamlenga nani kwenye masoko? Pili jee mnamchakato gani wa kuyafikia haya malengo? Mnataka kwenda kwa wateja wadogo wadoho moja kwa moja au mnataka kwenda kwenye wasambazaji moja kwa moja.
 
THANKS FOR THE BUSINESS IDEAS THAT YOU SHOWED OR LISTED
STILL SO NOT UNDERSTAND MOBILE ENTERTAINMENT HOW IT WORK.
COULD YOU EXPLAIN ABOUT ON HOW IT WORKS ??
Mkuu hii inabidi uchonge trailer ambalo unaweza kuvuta, kisha ndani weka Big screen mbili TV nununua PS3 au Xbox, weka ndani sound system na viti. Unakuwa una peleka trela kwenye event za watoto kama birthday, wazazi wanakodi for hour. Weekday fanya partnership na shule hizi za St. Fulani na chekechea
 
Safi.
Aise, mimi nimependa idea ya No 3 Car wash.
1. Nafahamu nahitaji kwanza eneo
2. maji (kisima, maji ya bomba) ....... (sijapata bei ya uchimbaji kisima)
3. Vijana wa kuosha magari (hawa watalipwa kulingana na kazi)
4,. .....motor na pump ile wanatumia ku- fasten maji - jina sahihi sijafahamu (sijui bei yake)
5. generator kwa ajili ya umeme (best, cheap and efficient generator sijazifahamu
6. kujenga eneo la kuoshea gari
7. Variable costs (hizi nafikiri si kubwa soap, vitambaa vya kuoshea, ving'arishi.......)

Nimetaja vile ambavyo nimekuwa naviona kwa waoshaji, ndio maana hata majina ni kama nimeyataja bila usahihi sana.

Tafadhali, kama unafahamu vya kutosha biashara hii nimeipenda na ninapenda kuifanya licha ya kuwa sina fedha kwa sasa ila najipanga.

Upo sawa mkuu, nibora kujipanga kabla huna mtaji kuliko kuwa na mtaji bila kujipanga. Unafanya vyema kabisa mkuu
 
Asalam aleykum naomba nisaidie tuseme una million ishirini unataka kufanya biashara zanzibar to dar au dar to zanzibar utafanya biashara gani na italipa ?
 
Nunua Vifaa Used kutoka Zenj leta Dar

Ni vzr zaid kama utakuwa unachukuwa Tenda mbali mbali za mahitaji ya watu

Zen unazamia Zenj unachukua mahitaji yako

Unawapelekea mahitaji yao

Ila usije Dumbukiza iyo pesa yote kwa Biashara Mdogo mdogo tuu
 
bado na amini kwa biashara ya buubaa, ng'ombe wanaouzwa karagwe bei ya kutupa sbb ya ukame inalipa hela nyingi kwa kipindi kifupi sana ila watz nadhan hatujaona kama ni fursa japo kwa wenzetu wanaKaragwe ni janga.
 
Mubarikiwe wote mnaochangia na kutoa elimu jinsi ya watu wanavyoweza kujikwamua. Ombi langu kwa vijana ni kuwa na idea kwanza kabla hujawa na mtaji na siyo kuwa na mtaji ndiyo utafute idea. Kwani pindi unapokuwa na wazo inakupa muda mzuri wa wewe kulifanyia upembuzi zaidi na kwa undani kuliko kuwa na mtaji kwanza kwani utajikuta unawekeza katika kitu ambacho hujakifanyia upembuzi vizuri
 
Mawazo mazuri sana nimependa namna wachangiaji walivyojitoa. Ila kiukweli mtaji ni changamoto.
 
Delivery

Bado tz tupo nyuma,hasa kwa vya kula, unaweza kuwa na scooter mbili tatu special kwa delivery, kwa wateja wa online pengine spending 30,000 ya cha kula deliver free.

24 hours

Kufanya biashara wakati wowote, hii utapiga bao sana, kwa biashara za usiku.

Usalama

Lazima uwangalie usalama wa biashara yako, hasa nyakati wa usiku, kwa mfano unauza chakula ukifika muda kuazia saa sita ya usiku unafunga na kuwacha window Maalum yakuhumia wateja fast take away food. Badala ya wateja kuingia ndani ya eneo lako, wengine sio wateja.

Kila baada ya muda pesa ku ondoa kwenye biashara yako na kupeleka bank or safe place.

Camera kugunga sehemu za biashara, cctv, hii ni kwa ajili ya kuwatambua wanao ingia na kutoka, ikiwezekana weka chumba Maalum cha cctv, kuwa na mawasiliano ya vituo vya polisi.
 
Nimefaidika na huu uzi, mke wangu amesomea ujasiria mali, hapa nilikuwa na fikiria jinsi ya kumsaidia na zaidi ni kuwa na machine za kutengeza package iwe plastic bag na chupa.

Nipo katika kufanya research ya mashine ninayo hitaji na uwezo wangu, nimefuatilia kwa mfano chupa za kutia shampoo na shower gel mpaka niende Kenya kununua.

Jengine nimefikiria kujenga eneo Maalum la kufanyia kazi. Kwa sasa biashara zetu tunatengeneza nyumbani.

Nime taget kununua, milk cream separate na mashine yatoa maganda ya tomato na kokwa kwa ajili ya kutengeza tomato paste. ..n.k kwa kuanzia.
 
Ivi naombeni ushauri, kw sasa nawez nkanzisha mradi gani ambao utaniletea maendeleo au nifanye biashar gan itakayowez kunpa faida kubwa,?
 
Habari wakuu natumaini mtakuwa poa,

Nataka kuanza kufanya biashara ya nafaka mf. mchele, maharage kunde n.k lakini ni kuchukua mkoani na kuuza Dar kwa reja reja lakini sijui wapi pa kuanzia na mikoa gani naweza kupata kwa bei rahisi na mimi nikapata faida. Nina mtaji wa ml2.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom