Business ideas (Bure)

Habari wadau,

Naombeni msaada wa wazo nimechoka kuumiza kichwa mwenyewe..

Ni biashara gani nzuri kwa dar es salaam ya kuuza na kununua (trading) kwa sasa. Biashara ambayo naweza zungusha walau sh milioni 2 au 3 kama "working capital" na nikapata walau sh 30,000 mpaka sh 50,000 kwa siku kama faida.

Ofisi ninayo tayari, leseni na vitu vingine vyote vya kuniwezesha kufanya ila sijajua biashara ya kufanya. Pombe siwezi uza sababu ya kiimani, maji ya jumla maduka kila kona, gesi za nyumani nazo mpaka maduka ya Mangi.

Msaada tutani!
 
Ha ha unajua kwann watu hawajakujibu uzi huu tangu juzi? Ushapanga na faida unayotaka
Hahaha,hili moja
La pili ana leseni tayari,sasa leseni alienda kuomba ya biashara gani
i?
La Ziada ni kwamba kwa mtaji huo na faida hiyo haviendani kabisaa,Inamaana baada ya Miezi miwili uwe umerejesha pesa yako?
Aisee kizazi cha sasa ni sheeeeda,yaani kila anaeishi mjini atakaka faida kubwaaa,ukimuambia faida ya buku tano anakuambia bora niache,wa bush anakuja anakomaa na Biashara ya karanga,anatusua
Asha sina la kukushauri ,maana jibu unalo mwenyewe
 
Habari wadau,

Naombeni msaada wa wazo nimechoka kuumiza kichwa mwenyewe..

Ni biashara gani nzuri kwa dar es salaam ya kuuza na kununua (trading) kwa sasa. Biashara ambayo naweza zungusha walau sh milioni 2 au 3 kama "working capital" na nikapata walau sh 30,000 mpaka sh 50,000 kwa siku kama faida.

Ofisi ninayo tayari, leseni na vitu vingine vyote vya kuniwezesha kufanya ila sijajua biashara ya kufanya. Pombe siwezi uza sababu ya kiimani, maji ya jumla maduka kila kona, gesi za nyumani nazo mpaka maduka ya Mangi.

Msaada tutani!


Mradi huu mpya utakufaa sana. Kwa milioni tatu utapata si chini ya Sh 25,000 kila siku.


Uwekezaji mbadala usio na stress, wa uhakika na wenye kipato kikubwa zaidi umeingizwa sokoni

Maendeleo katika nyanja za mawasiliano (Internet) yameleta mabadiliko makubwa mno na yenye tija mno kwa wanadamu popote pale walipo duniani katika karne hii ya mawasiliano (Information Age).

Kwa kutumia teknologia ya mawasiliano, kampuni inaweza kusajiliwa popote pale duniani na ikafanya biashara na kila mtu ama ndani au nje ya mipaka ya nchi ambamo kampuni imesajiliwa kwa kuuza bidhaa au huduma zake katika mfumo wa mawasiliano (internet) kwa kutumia tovuti.

Mfano ni bidhaa ya Cashback Marketing (CBM) inayoletwa kwetu na kampuni inayomilikiwa na wanachama waliotapakaa duniani kote inayoitwa We Share Success Inc. yenye makao yake makuu Las Vegas, USA.

Hii ni bidhaa ya kutangazia biashara yako lakini ina muundo na motisha ndani yake ambavyo hata kama huna biashara kwa sasa ya kuitangaza bado unaweza ukainunua na ikakuingizia kipato cha mpaka 1% cha kila siku kutokana na pesa ulizolipa kununulia hii bidhaa.

Kila uniti moja ya CBM inauzwa USD 30.

Unaponunua bidhaa hii basi unaamua kama unataka kuitumia mara moja kwa kutangazia biashara yako na hivyo utainunulia kwenye sehemu inayoitwa Personal Marketing Pool ambapo hutalipwa daily cashback au unainunulia kwenye sehemu inayoitwa Global Marketing Pool ambapo unakuwa unaiazima CBM izitumie uniti zako ulizonunua kwa sasa kutangazia biashara za mtandao wa Unicorn Network zilizotapakaa dunia nzima mpaka pale utakapoamua kuanza kuzitumia mwenyewe kutangazia biashara yako. Katika kipindi chote utakachokuwa umeiazima CBM kutumia uniti zako kutangazia biashara zake basi utalipwa daily cashback rate ya mpaka 1%.

Tunatumia lugha ya kusema mpaka 1% kwa sababu daily cashback rate inaweza kuwa kuanzia 0% (yaani hakuna daily cashback rate inayolipwa kwa siku hiyo mpaka 1% ambayo ndio rate ya juu unayoweza kuipata kwa siku.

Kama kampuni, hatutarajii daily cashback rate kushuka chini ya 1% kutokana na fursa zilizopo za kupata mauzo ya zaidi ya 1% kwa siku tutakapotumia hela zilizowekwa ndani ya Global Marketing Pool kutangazia biashara zetu zilizotapakaa dunia nzima lakini kwa sababu biashara yoyote ile inaweza kukutana na changamoto zilizopo nje ya uwezo wake hivyo kuna wakati hali inaweza kuwa ngumu kwa kampuni kuweza kupata mauzo zaidi ya 1% au kukosa kabisa itakapotumia hela zilizopo kwenye Global Marketing Pool kutangazia biashara zake ndio maana kuwa kwenye upande wa uhakika zaidi tunasema daily cashback rate itakuwa kuanzia 0% mpaka 1%.

Wengi wetu tumejaribu biashara na zimetushinda kuzifanya na kuishia kupata hasara kwa sababu nyingi tu zikiwemo:

  • ·Kuwajiri watu watufanyie na kutokuwa na muda wa kuzifuatilia matokeo yake waajiriwa wanatumia mwanya huo kukuibia au kuweka maslahi yao binafsi juu ya maslahi ya biashara yako;
  • ·Kukosa ujuzi wa kuendesha biashara husika
  • ·Gharama nyingi za kuendeshea biashara yako kama vile kulipa pango la ofisi, umeme, maji, usafi, wafanyakazi, ulinzi, n.k.
  • ·Uwezo finyu wa kuuza vya kutosha na hivyo kuweza kutengeneza faida ya kutosha kutokana idadi ndogo ya watu unaowategemea kuja kwenye biashara yako kutokana na umbali. Kwa mfano ukiwa na duka basi utauza kwa watu wa eneo hilo tu linalolizunguka duka lako!
  • ·Umasikini wa watu unaofanya nao biashara unasababisha biashara kuwa ngumu.


Unaponunua bidhaa hii na ukaitumia kwa ajili ya kupata cashback ya kila siku basi unakuwa huna stress ya kuisimamia biashara uliyoianzisha wewe mwenyewe au kutakiwa kuwa na ujuzi wa kuiendesha au kumwajiri mtu ili akusimamie biashara yako au kulipia gharama nilizozitaja hapo juu au kuwa na wasiwasi wa ufinyu wa soko kwani biashara inaendeshwa na kusimamiwa na kampuni ya kimataifa inayofanya biashara dunia nzima na yenye wataalam waliobobea katika kila fani wanayoshughulika nayo.

Hivyo nawashauri wafanyabiashara na wale ambao wanataka kufanya biashara kufikiria kutenga angalau sehemu ya mapato yao kununua bidhaa hii ama kwa ajili ya kutangaza biashara yako na wakati huo huo unapata pesa za kila siku au kwa ajili ya kupata pesa za kila siku kwanza na kutangaza biashara baadaye wakati utakapoamua au kuwa na biashara yako.

Mapato ya siku utakayoyapata ukinunua uniti za CBM ni makubwa ukilinganisha na biashara zako unazofanya sasa hivi kwa sababu biashara hii ni ya kimataifa hivyo ina ufanisi mkubwa katika mfumo wake wa biashara kuliko biashara yako iliyoishia kwenye ngazi ya eneo unaloishi au wilaya au mkoa au taifa lako tu au kikanda tu kama vile Africa Mashariki.

Kwa mfano tuchukulie umenunua uniti za CBM kwa ajili ya kupata kipato cha daily cashback katika mazingira yafuatayo:

·Kiwango cha cashback cha kila siku bado kiko 1% kama kilivyo kwa sasa
·Ukiwa na shilingi unataka kuibadilisha kwenda kwenye dola basi itakughalimu sh 2,200
·Ukiwa na dola unataka kuibadilisha kwenda kwenye shilingi basi utaiuza dola hiyo kwa sh 2,000.
·Kiasi cha fedha ulichonacho kuwekeza kwenye mradi huu ni TZS millioni 1.

Kwa mfano huo hapo juu basi utakuwa unapata USD 4.5 (TZS 9,000 ) kila siku.


Kwa hiyo kama una biashara unayoifanya au ulishawahi kuifanya ambayo sasa hivi huifanyi tena kwa sababu hailipi au kwa sababu nyingine yoyote ile basi angalia mtaji ulioutumia pamoja na gharama za kila siku za kuundeshea mradi wako na linganisha na pesa ambazo ungetarajia kuzipata kwa siku kama ungeamua kununua CBMs zenye thamani ya mtaji wako ili upate mapato ya kila siku badala ya kuziwekeza kwenye mradi wako.

Kwa mfano kama biashara yako ni bajaji basi mtaji wa kununua bajaji ni TZS milioni 5 na mapato ya kila siku ukimpa dereva akuletee marejesho basi ni TZS 15,000. Lakini ukitumia hela hizohizo (TZS milioni 5) kununua uniti za CBM ili zikupatie mapato ya daily cashback basi utapata kiasi cha USD 22.5 (TZS 45,000 kwa siku!!!

Kwa watakaokuwa tayari kuanza kuitumia CBM kama chanzo chao cha kupata mapato kupitia motisha wa Cashback unaotolewa kila siku basi tuwasiliane ili niwaelekeze cha kufanya kuweza kuitumia bidhaa hii kama uwekezaji mbadala kwa ajili ya kupata daily cashback.
Kumbuka kwamba Cashback Marketing ni bidhaa na sio hati ya uwekezaji hivyo ukishainunua umeinunua kwa ajili ya kutangaza biashara yako na hela hairudishwi. Ndio maana nauita uwekezaji mbadala kwa kuwekeza kwa ajili ya kupata mapato ya daily cashback yanayotolewa kama motisha wa kununua bidhaa hii ambayo ni makubwa zaidi na ya uhakika ukilinganisha na mapato utakayoyapata kwenye biashara yako kutokana na sababu mbalimbali nilizozielezea hapo juu.


Nipigie simu kwa namba hizi 0772 977 330 au 0658 977 330 au tupange tuonane ofisini kwangu kama upo Dar. Ofisi yangu iko Makumbusho Bus Terminal & Shopping Complex, Block A, Ghorofa ya kwanza, Chumba No. FF-04.

Bonyeza kiungo cha CASHBACK MARKETITNG hapo chini kwenda kwenye tovuti ya Cashback Marketing ambapo unaweza kuzinunua hizi uniti moja kwa moja online.
 
Ameomba msaada wa mawazo na kuanisha capital na matarajio yake,sikutegemea angejibiwa kama mnavyo mjibu. Sidhani kama kuna ulazima wa kuchangia kama huna mawazo . Kama huna mawazo kaa kimya,sio kumkatisha mtu tamaa
 
Wakuu, mambo yanakwendaje, nadhani wote mpo safi na kila mmoja anaangalia Magu anavyo kimbiza. Wengi wetu sasa tumerudi nyuma mwili umekuwa na hofu tunaogopa kuanza biashara sababu hatujui kesho, hilo ni kosa namba moja kwa mtu ambae anataka kuvuna mapema.

Muda kama huu ndio muwafaka kuweka mikakati madhubuti, sababu wale wajanjawanja wote lazima wazame tuu, lakini kama umeweka strategy zako sawa huu ndio muda maana Mh. anasafisha barabara wewe kama strategy zipo sawa ni mwendo wa Mwendo Kasi tuu.
 
Mkuu mtanganyika shukran kwa idea zako nzuri..... Lakini mimi nipo interested sana na kilimo.... Je kwa uzoefu wako ni kilimo gan ambacho kwanza kinalipa, pili hakitegemei sana mvua, tatu sitahitaji mtaji mkubwa sana..... Shukran!!
 
Mkuu mtanganyika shukran kwa idea zako nzuri..... Lakini mimi nipo interested sana na kilimo.... Je kwa uzoefu wako ni kilimo gan ambacho kwanza kinalipa, pili hakitegemei sana mvua, tatu sitahitaji mtaji mkubwa sana..... Shukran!!
Kilimo kizuri ni cha viazi mviringo km upo njombe au iringa. Ni kilimo rahisi sana na chenye gharama nafuu ndani ya muda mfupi km uko wellfocused unatoka haraka mno
 
Wakuu, mambo yanakwendaje, nadhani wote mpo safi na kila mmoja anaangalia Magu anavyo kimbiza. Wengi wetu sasa tumerudi nyuma mwili umekuwa na hofu tunaogopa kuanza biashara sababu hatujui kesho, hilo ni kosa namba moja kwa mtu ambae anataka kuvuna mapema.

Muda kama huu ndio muwafaka kuweka mikakati madhubuti, sababu wale wajanjawanja wote lazima wazame tuu, lakini kama umeweka strategy zako sawa huu ndio muda maana Mh. anasafisha barabara wewe kama strategy zipo sawa ni mwendo wa Mwendo Kasi tuu.
Mkuu asante kwa uchambuzi mzuri hakika wengi tutanufaika.Mimi nilikuwa nahitaji kufahamu je kuna uwezekano wa kufanya packaging ya dagaa wa mwanza na wakabaki na rangi yao ileile(nyeupe) kwa mda mrefu bila kubadilika rangi?Maana kwa kawaida wanabadilika rangi within a week.Pili je naweza pata mashine ambayo inakausha dagaa bila kuanika.I mean baada ya kuwavua wanakaushwa na mashine badala ya jua?
 
Kijana13 Finance kwa any start up ni uphill battle, lakini guess what it is winnable. Kuna mambo lazima uzingatie kabla ujaanza kuzunguka kutafuta mtaji. Najua umeshasikia hili kwamba kati ya start-up kumi zinazoanzishwa saba zinakufa ndani ya miezi michache. What does this mean for an investor/bank? Start-up are too risky. Na hii ni kwanini start-up too risky, mara nyingi start up nyingi zinaanzishwa na watu wasio na ulewo wa biashara, mbili start up nyingi are just a single product.

Nimejaribu kufikiria jee ni nini entrepreneur angalie kabla hajaanza kuzunguka kutafuta mtaji wa kwa start up. Kwa uchache here is the roadmap.
  1. Know the numbers behind your business. Ukweli kwamba kama unataka kutengeneza business ambayo utaajiri watu na wewe kupata mafanikio basi lazima ujue namba. Mambo kama lini biashara itakuwa cash positive, Jee kiasi gani cha mtaji unaitaji? Jee Gross Margin zako zitakuwaje? Lini biashara ita break even, Jee ikifika sehemu fulani utaitaji tena mtaji kiasi gani? Jee mauzo kwa mwezi yawe kiasi gani ili uweze kujiendesha mwenyewe. Haya yote ni maswali ambayo lazima ujiulize na uprove majibu yako. Kama utajidanganya mwenyewe kwa kusema aaah nitauza KG 200 kwa mwezi za unga bila hata kujua Bakheresa anauza ngapi, hapo utakuwa unajiingiza chaka.
  2. Test and Prove your idea. Hapa ndio kikomo cha start up, idea yako itakuwa idea mpaka utakapo ijaribu na kuona inafanya kazi. Mfano mimi nimekuwa nikiwaza sana biashara ya kusindika vyakula, sababu it is not capital intensive, the market is BIG and the process is not complicated. However, nimekuwa muwazi nikitambua kwamba Waatanzania sio walaji wa process food, it's a new product machoni kwa watu so it can be mix results. So, i decide kutest the market, hivyo nitatengeneza prototype (za majaribio) na naanza na maharage kwanza, nita process 100 jars za 1/2KG Mbeya beans, kisha 20 nitagawa for different people from different background, kisha baada ya muda nitachukua survey kuona wameonaje. Kama watapenda then i know this idea can be product to the mass, kama hawa 20 wakisema NO then am ending this nonsese and think about something else. Hivyo ni muhimu sana kutest market before anything.

Kama hayo mawili hapo juu yote ni provable then unaweza kusema kwamba wewe sasa una biashara. Ileweke kwamba kuna tofauti ya biashara na idea. Financing ziko za aina kadhaa lakini kwa start-up i will only focus on two: Angles Investors ( Mama mdogo, uncle, mjomba, jirani, kaka yako, someone you know), hawa ni jamaa zako ambao wanakuamini wewe, take your idea to this folks and ask for a certain capital with a Promise of percentage ownership katika biashara yako. Kumbuka to own 70% of a business is better than own 100% of an idea with no capital. Second is debt finance (Bank, Vikoba, Saccoss, private equity, n.k). These are the folks who doesnt know you, and they don't care about your product they only care for ROI of their money. Nakupa 1,000,000 prove utairudisha in 6 month with 20% interest rate. How to face this mean people? Below is 1,2,3
  1. Have a some revenue, hawa jamaa wanataka kuona jee umeshatengeneza hela. Means your business is not an idea any more. So, make sure biashara ishasimama hata kwa mguu moja kabla ya kwenda Bank kukopa.
  2. Be prepared: Kumbuka hawa jamaa only thing they care is their money, so lijue soko, jua forecast zako, zijue namba zako vilivyo na hapa kama uliandikiwa Business Plan be ready kutoka jasho la kwapa.
  3. Get use to the word "NO", jiandae kabisa kwamba wapo watakao kukwambia No lakini don't give up.

I hope this point chache zinaweza kutoa mwanga kidogo, lakini kumbuka ya kwamba wewe ndio unaijua biashara yako kushinda mtu yoyote, hivyo no one can stop you to make it happen.

Kaza msuli haya mambo yanawezekana, 80% ya kuendelea ni kujiandaa kimawazo, kama umejipanga kimawazo unakwenda. Jamani hawa kina Manji, MO, Mengi, Azam waliwezaje? If you have a tough skin kama kenge, then this is your field. Lakini kama ukipoteza 10,000Tsh unakosa usingizi, basi please kaa huko huko kwa muajiri. Failure is not permanent.
Will work with it.
 
Wakuu, mambo yanakwendaje, nadhani wote mpo safi na kila mmoja anaangalia Magu anavyo kimbiza. Wengi wetu sasa tumerudi nyuma mwili umekuwa na hofu tunaogopa kuanza biashara sababu hatujui kesho, hilo ni kosa namba moja kwa mtu ambae anataka kuvuna mapema.

Muda kama huu ndio muwafaka kuweka mikakati madhubuti, sababu wale wajanjawanja wote lazima wazame tuu, lakini kama umeweka strategy zako sawa huu ndio muda maana Mh. anasafisha barabara wewe kama strategy zipo sawa ni mwendo wa Mwendo Kasi tuu.
upo right mkuu wangu. Naona sasa hivi ni perfect opportunity ya kujipanga
 
THANKS FOR THE BUSINESS IDEAS THAT YOU SHOWED OR LISTED
STILL SO NOT UNDERSTAND MOBILE ENTERTAINMENT HOW IT WORK.
COULD YOU EXPLAIN ABOUT ON HOW IT WORKS ??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom