Business ideas (Bure)

Fungua biashara zinazojisimamia huku ukiendelea na kazi...
Mfano wa biashara hizo ni kama bajaji au boda boda. Kama una mil 20 unaweza kununua hata bajaji ndio nzr ukilinganisha na boda ambazo huwa na risk kubwa. Tafuta bajaj used ambazo zimetumika mwaka mmoja na bei zake huwa ni kati ya mil 4/4.5
Hesabu ni elfu 20 kwa siku.
Hii ni biashara nzur kwa mtu anaefanya kazi kwa sbb haihitaji muda wako mwingi kuifuatilia zaidi ya kuzipeleka service kila mwisho wa wiki. Kwa mtaji wako unaweza kupata bajaj nne na chenchi ikabaki kwa ajili ya service na vibali. Unazitumia mwaka mmoja halafu unaziuza na kununua nyingine.
N.B kama utaamua kufanya biashara hii siku ya kununua ni lazima uwe na fundi.
 
Endelea na kazi Kwani kuajiriwa sio dhambi.

Kwa tafsiri lahisi biashara/ujasiriamali ni sawa na mbio za "Nyika". Kadri unavyofanya mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa na pumzi. Nakushauri ufungue biashara yako iwe ni sehemu ya kukuongezea kipato kwa kazi unayofanya.

Huu sio muda muafaka wa kuacha kazi na kufanya biashara sababu.
1. Uwezo wa watu kufanya manunuzi umepungua
2. Uhaba wa chakula umesababisha mfumko wa bei (Labda uanze na biashara ya nafasi).
3. Serikali haitabiriki. Serikali imekuwa ni ya matamko badala ya sheria, kanuni na taratibu kutamalaki. Mfano wazi ni wafanyabiashara wa "viroba" jinsi walivyotendewa.
Binafsi nakushauri ujiwekee malengo ya muda mrefu kidogo.kama pesa ulioipata imetokana na kazi.nakushauri ujenge guest house, jiwekee malengo ndani ya miaka mitatu au minne iwe tayari kwani guest hata usimamizi wake ni rahisi.
 
mkuu guest gani ya m 20 nami niijenge
 
Fungua biashara zinazojisimamia huku ukiendelea na kazi...
Mfano wa biashara hizo ni kama bajaji au boda boda. Kama una mil 20 unaweza kununua hata bajaji ndio nzr ukilinganisha na boda ambazo huwa na risk kubwa. Tafuta bajaj used ambazo zimetumika mwaka mmoja na bei zake huwa ni kati ya mil 4/4.5
Hesabu ni elfu 20 kwa siku.
Hii ni biashara nzur kwa mtu anaefanya kazi kwa sbb haihitaji muda wako mwingi kuifuatilia zaidi ya kuzipeleka service kila mwisho wa wiki. Kwa mtaji wako unaweza kupata bajaj nne na chenchi ikabaki kwa ajili ya service na vibali. Unazitumia mwaka mmoja halafu unaziuza na kununua nyingine.
N.B kama utaamua kufanya biashara hii siku ya kununua ni lazima uwe na fundi.
Ushauri mzuri sana ,nashukuru sana ndugu yangu
 
Usisikilize watu wanaokukataza usiache kazi
kama una mtaji fikiria biashara ya kufanya
Mkuu kuacha kazi sio tatizo ila tunafikia unapo acha kazi unaenda kufanya nini ndo maana tunashauri kabla hajaacha kazi anapaswa kufanya biashara amabayo ataweka mtaji kidogo baada ya mda atakuwa amepata uzoefu na anapo acha kazi anajua anaenda kufanya kitu Fulani na maslahi yake anayajua
 
Binafsi nakushauri ujiwekee malengo ya muda mrefu kidogo.kama pesa ulioipata imetokana na kazi.nakushauri ujenge guest house, jiwekee malengo ndani ya miaka mitatu au minne iwe tayari kwani guest hata usimamizi wake ni rahisi.
Hebu nijuze hyo biashara Mimi sijui vzuri
 
Nimeona hapo biashara ya gesti ni kwel inalipa sana ukipata oneo husika mfano mpakani kama tunduma ila viwanja havikamatiki,kifupi kma kiwanja unacho sehemu inayoeleweka sio mbaya kwa kuanzia
 
UPANDE WA KILIMO
@ufugaji samaki
@ufugaji kuku wa mayai na nyama
@ufugaji wa nguruwe
@uzalishaji mbwa na kuwauza
Kilimo mbogamboga
@utengenezaji chakula cha mifugo
@utengenezaji wa unga na kuuuza
@kununua nafaka na kuuza kama mchele
@ulimaji wa mazao ya chakula na biashara
@ulimaji wa matunda

UPANDE WA ELIMU
@ufundishaji tuition,au shule binafsi
Huduma ya chakula mashuleni na ofisini
@utunzaji wa watoto/day care centre
@Uuzaji wa past papers na solution zake
@kufundisha kompyuta
@uuzaji wa vifaa vya stationery
UPANDE WA ICT
@uuzaji wa simu,vifaa vya simu na kurekebisha/repair
@uuzaji wa Pc na vifaa vyake
@kuwatengenezea web watu
GRAPHICS DESIGN
Huduma ya kurudisha namba zilizopotea
Huduma ya simu pesa(aitel money,tigo pesa na m pesa)
@uchezeshaji wa magemu
Huduma ya banda la kuangalia mechi Uefa,vpl,epl na world cup
BIASHARA NYINGINE
@upakaji rangi
@utengenezaji sabuni na cream body
@utengenezaji batiki
@utengenezaji dawa za chooni
anzisha blog yako
@ tengeneza app yyt katika google play store
Andika kitabu cha kuelimisha mambo ya dini
@Fanya research na tafuta wafadhili ktk hy mada yako na fanya presentation
@usafirishaji mizigo
@mtengenezaji cake za harusi na mpambaji
mkufunzi wa mazoezi ya viungo( body fitness trainer)
ahsante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom