Business ideas (Bure)

Wazo la Biashara - SUPERMARKET NDOGO (AKA MINI SUPERMARKET)
Enzi hizo biashara za supermarket wanunuzi wake walikuwa wachache wenye kipato cha ziada ila kwa sasa supermarket zimekuwa zikipata wateja wa kila aina. Tafiti zinaonesha kuwa katika kila watu kumi wa mijini watu watano hupendelea kununua bidhaa katika supermarket (ama angalau mini supermarket).

Mabadiliko haya yametokana na kuzagaa kwa supermarket kila kona na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata kipato cha kati.
d4b926c603f9be96db0a71a22aca36d5.jpg

Hivyo basi, kuazisha mini supermarket kwaweza kuwa wazo zuri sana la kibiashara endapo una mtaji wa kutosha kuweka kila kitu ndani yake.

Acha leo niongelee jinsi unavyoweza kuanzisha mini supermarket yako mwenyewe. Sitoongelea supermarket kubwa bali zile ndogo ndogo.

ENEO:
Ndani ya Dar es Salaam, mwanza ama arusha, kupata eneo linalotosha kuweka supermarket ndogo unahitaji kati ya Tshs 800,000 hadi 3,000,000 kutegemea na ukubwa wa chumba cha biashara na wingi wa watu katika eneo husika.

Kuna msemo huwa naupenda sana. Msemo huo si mwingine bali ni ule usemao "Vidogo Vyavutia". Tuchukue hiki kiwango cha chini cha Tshs 800,000. Tunalipa miezi sita inakuwa Tshs 4,800,000. Mh, acha kuguna. Usije ukaogopa mpaka ukaacha kuwaza kuanzisha biashara hiyo. Jua kuwa asilimia kubwa ya pesa utayolipa kwenye mini supermarket ni kodi ya upangaji.
52ac95c14c52a1000e10ddeec4595541.jpg

LESENI NA VIBALI:
Ili kufanya biashara ya mini supermarket unahitaji vibali mbali mbali na leseni. Usiumize kichwa juu ya hili maana hata uendapo ugenini unahitaji kujua nauli za daladala za kule japo hakuna anaejishuhulisha kuulizia. Unachotakiwa kujua ni bajet ya kuandaa kwa nauli za daladala ama texi kule uendako. Ili usisumbuke na suala la vibali na leseni weka bajet ya Tshs 600,000 itamaliza kila kitu.

BIDHAA:
Wapo wasambazaji kadhaa walio tayari kusambaza bidhaa mbali mbali kwenye mini supermarkets. Hawa husambaza mlango hadi mlango. Unahitaji kujiandaa na kati ya Tshs 10,000,000 na 20,000,000 kujaza bidhaa ndani ya supermarket. Kwakuwa "Vidogo Vyavutia" acha tuanze na Tshs 10,000,000.

WATUMISHI:
Kwa supermarket ya bidhaa za milioni 10, hapo wapaswa uwe na watu wasiozidi 5 watakaofanya kwa shift ya watatu watatu. Hawa watakugarimu kama Tshs 2,000,000 kwa mwezi.

FAIDA:
Mini supermarkets hutoa faida kati ya Tshs 2,000,000 na 3,000,000 kwa mwezi. Kwakuwa tumeamua kuanza kile "Kidogo Kinachovutia" faida yetu itakuwa Tshs 2,000,000 kwa mwezi.
9fb07e33f6f8a49cca96da3b639af816.jpg

CHANGAMOTO:
Huwa hakuna biashara isiyo na changamoto. Changamoto ya kwanza kwa supermarket ndogo ni wizi. Wamiliki wengi wa supermarket ndogo ndogo hulalamikia suala la wizi kutoka kwa wateja na watumishi wao. Ni rahisi mtumishi wako kukwepa wizi wake na kusingizia wateja. Wapaswa kuweka mitego mbali mbali ya kupunguza suala la wizi ili unufaike na faida itokanayo na biashara yako. Moja ya mitego hiyo ni cctv camera. Kwa kawaida ukiweka camera hata mbili tu zitasaidia sana. Hii hugarimu wastani wa Tshs 1,200,000. Changamoto nyingine ni bidhaa kufikia mwisho wa matumizi (yaani kuexpire). Wasambazaji kadhaa wapo tayari kuchukua bidhaa zinazoisha muda wake japo sio wote. Kupunguza uwezekano wa kupata hasara kutokana na bidhaa kuisha muda wake wa matumiz kabla hazijanunuliwa, jaribu kununua bidhaa zako nyingi kwa wasambazaji walio tayari kuchukua bidhaa zilizokweisha muda wake. Pia jitahidi kununua bidhaa ambazo zimetengenezwa muda mchache ulipita ikiwezakana hata kuwapa masharti wasambazaji kuwa bidhaa zinazozidi mwezi wasikuletee.

Pia kuna bidhaa ambazo hazitouzika kabisa na wapo wateja watakaohitaji bidhaa ambazo wewe hauna. Hii ni changamoto ila isije kukuvunja moyo kwani itakusumbua mwanzoni tu na baadae utakuwa mzoefu.

Biashara ya mini supermarket ni biashara yenye faida sana ila huhitaji mtaji usiopungua Tshs 17,000,000 na uangalizi wa karibu ili kushamiri.

ZINGATIO: NIMEONA WATU WENGI WANASHINDWA KUELEWA KUWA FAIDA = MAPATO - MATUMIZI WANAULIZA FAIDA YA 2,000,000 AFU KUNA MISHAHARA NA BILI NYENGINEZO. JAMANI FAIDA HUPATIKANA BAADA YA KUTOA GARAMA ZOTE. KWAIYO MIL2 NI BAADA YA KUTOA GARAMA ZOTE.
_________________________________________________
Jifunze zaidi biashara mbali mbali unazoweza kuzifanya kupunguza ukali wa maisha.
 
Wabongo tunakosea sana tunaposema Mini Supermarket. Supermarket haiwezi kuwa mini tena, yaani Soko kuuuubwa lenye karibia kila kitu liwe kasoko kadogo tena muda huo huo.
Nachojua kuna Super market na Mini market, na Hakuna Mini super market.
Naweza kuelimishwa kama huwa naelewa ndivyo sivyo.
 
Jamani mimi sijamlazimisha mtu afanyie kazi au la ila nimesema ni ideas kwa anayehitaji atafute kujua zaidi na ukitaka kufaulu jambo lolote lazima ukajifunze sasa wewe unayesema nimeorodhesha sasa ulitaka nikufafanulie kila moja? Na wewe kazi yako golkeeper tu kupokea na sio mchezaji wa ndani.Life is a game tafuta mpira
Shukrani sana mkuu
 
Salaam kwenu wana JF.
Alhamdulillah! Mwenyezi Mungu ameniwezesha kufikisha kiasi hicho cha fedha baada ya kujichanga kwa muda mrefu kutoka katika kipato cha kazi nizifanyazo.
Kutokana na misukosuko mingi niliopitia ya kuajiriwa nafikiria muda umefika kusimama mwenyewe.
Naomba ushauri wenu juu ya nini nifanye sababu sina uzoefu sana ktk biashara na kuna wakati nilijaribu ikashindikana nikarudi kujipa mda na kujipanga kimtaji.

Naomba mawazo yenu ndugu zangu kwa moyo mmoja.
Natanguliza shukrani zangu nyingi kwenu.
 
Hongera kwa kufikisha mtaji huo. Kabla ya kuwaza kuacha kazi ungewekeza kwanza uangalie biashara inaendaje kwa walau miezi sita, ukiona inakwenda vyema ndio uanze kufikiria kusimama mwenyewe.
 
Njoo nikuuzie nyumba yangu yenye actual values ya 36 million kwa bei ya mil 25 then kwa mwaka mmoja baadae kulingana na location iliyopo utapiga good money kwa kuiza bila kuwa na haraka.

Invest in a more safe and secured project. Real estate.
 
Njoo nikuuzie nyumba yangu yenye actual values ya 36 million kwa bei ya mil 25 then kwa mwaka mmoja baadae kulingana na location iliyopo utapiga good money kwa kuiza bila kuwa na haraka.

Invest in a more safe and secured project. Real estate.
Nyumba Ipo wapi mkuu funguka si vibaya ukiweka tukaiona gapa
 
Njoo nikuuzie nyumba yangu yenye actual values ya 36 million kwa bei ya mil 25 then kwa mwaka mmoja baadae kulingana na location iliyopo utapiga good money kwa kuiza bila kuwa na haraka.

Invest in a more safe and secured project. Real estate.
Nyumba iko wapi embu Funguka tu faidike wote
 
Njoo nikuuzie nyumba yangu yenye actual values ya 36 million kwa bei ya mil 25 then kwa mwaka mmoja baadae kulingana na location iliyopo utapiga good money kwa kuiza bila kuwa na haraka.

Invest in a more safe and secured project. Real estate.
Kwann hilo wazo ulilompa jamaa usilitumie wewe kupiga pesa. Au mwenzetu umeshiba mapesa?
 
Peleka shamba kias..peleka kwenye mifugo kias(CLOSE SUPERVISION MUHIMU) inayobaki nunulia kiwanja/viwanja..
FANYA RESEARCH YA KUTOSHA KABLA KUFANYA BIASHARA YOYOTE

Kwa kifupi afanye portfolio Investments.

N.B
Don't put all eggs Into one Basket.
 
Kwann hilo wazo ulilompa jamaa usilitumie wewe kupiga pesa. Au mwenzetu umeshiba mapesa?
Hii business inataka mtaji mkubwa sometimes huge capital kwa hela yangu ya mshahara wa mwl hata kuwa mpambe wa kampuni ya real estate sistahiki.

Matter of fact, hii ni stress free business na idadi kubwa ya watu wanahamia mjini ilhali idadi ya nyumba za kisasa haziongezeki. Hivyo anahitajika MTU mwenye mtaji kukaa kati na kupiga hela zake zile easy money!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom