Business idea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Business idea

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kassamali, Jan 27, 2011.

 1. k

  kassamali JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Je una Idea au Business project ambayo inahitaji Mtaji usiozidi Usd 4M ambayo returns yake inaweza ikafikia mpaka USD 20M baaada ya miaka 3 au 5 with very low risk ila masharti yake ni simple lazima mimi niwe Partner katika hiyo na lazima business iwe ndani ya hizi sphere na zingine ambazo hazipo kutoa kilimo manaa kilimo risk kubwa

  1)IT
  2)Renewable energy
  3)Real estate

  Na zingine nyinging ambazo sijazitaja

  Ila Idea au Project lazima iwe origina na mpya na uwe umefanya assessment zote na suala lingine Elimu yako na uzoefu wako hasa katika hiyo Idea unayo taka ku offer

  Kama upo serious ni PM
   
 2. babalao

  babalao Forum Spammer

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee inaonekana unayo mapesa unataka kuwekeza ila hujui ufanye nayo nini huoni kama mtu akija na business idea na wewe ukatoa mtaji itakuwa ngoma droo lakini ukitaka atoe na mtaji kuchangia wewe utampunja. Mimi nakushauri kwamba watz wengi siyo waaminifu watakuingiza mjini na pesa zako njia nzuri ni kununua hilo wazo la biashara na kuanzisha wewe mwenyewe hiyo biashara. Kwa ushauri zaidi tuwasiliane ninayo mawazo mengi naweza kukuuzia. Nipigie simu namba 0755394701
   
 3. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kassamali,
  Parnerships kama unayoitarajia inawezekana.
  Upande wa IT kuna ideas nyingi ambazo kwa nchi yetu development yake bado ni changa sana kwa hivyo itahitaji muda kidogo kabla haujafikia critical mass ili returns unazotarajia zitimie. Hata hivyo, nadhani kwa up coming economies, returns huwa around 30% kwa hivyo kama ume-invest 4Mil USD,basi kwa mwaka gross unaweza kutarajia 5.2Mil, hence returns of around 1.2Mil less Taxes.
  Kwa kuzingatia kuwa IT bado ni changa, my suggestion to you ni kuwa, your invest in these feasible ideas on a longer term basis, create the facility from where these businesses can operate from and in the long term you will have partnered with great minds indeed.
  Kama babalao alivyo suggest, unaweza kuzinunua hizi ideas outright, kama unaweza kuziendeleza mwenyewe au ukawa partner with the bearer of the idea, na kuziendeleza pamoja.
  Unaweza kuulizia hapo UDSM kitengo cha IT, nilisoma kuwa wana incubator of ideas pengine huko kuna ambazo tayari zimeiva, just needing capital to get going.

  For those familiar with "Dragons Den" kipindi cha luninga UK/US/Australia kinacho 'wakutanisha wenye ideas, na wenye pesa in hope of partnership establishment, nadhani will attest kuwa this can be a very fruitful meeting for the two parties. Rations of investments huwa sio kubwa sana, around 250K USD, na percentages ni around 70/30 (in favor of the dragon).

  Kassamali, you need a manager to look after your investments? Give me a shout....
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mzee mimi nina idea nzuri sana kwenye real estate. With 4m USD we can make it, kama kweli uko serious naomba uni-PM tujadiliane zaidi
   
 5. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
   
 6. babalao

  babalao Forum Spammer

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Facts and figures, Mimi ni mjasiriamali niliyebobea Tuliingia Partnership na jamaa Tukaanzisha kampuni ya Contactor inaitwa Shinyanga annex Building contractors. Yule jamaa alifanya kazi za Sh. 300 million na hakunipa mgao wangu mpaka amekufa bila kunipa mgao wangu.
   
 7. misorgenes

  misorgenes JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mi ngoja jifunze kitu hapa, jamani toeni comements bac!
   
 8. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  [QUOTE=Kassamali,
  Mkuu.Kuna watu wengi tu wenye mapesa yao kibao mfukoni km wewe lakini hawajui wayafanyie nini, matokeo yake ni kiungia mkenge.Ndg yangu Kassamali kimsingi wazo lako la kuwekeza pesa zako sio baya ni zuri tu, ila mbinu unayotumia kutafuta huo uwekezaji sio mzuri sana, kwa kama Babalao alivyosema hapa Bongo matapeli ni wengi tena wanajua sana kupanga mipango, wabunifu kweli kweli, waandishi wazuri sana wa michanganuo ya kibiashara, wacheshi,wakarimu mno, wapole, lakini mwisho wa siku wanakuacha pabaya.

  Ndg yangu sauala la kuwa partnership na mtu usiyemjua vizuri kabisa ni hatari sana ktk ulimwengu wa kibiashara, ushirika ktk biashara ni mgumu mno unataka mtu ajitoe kikamilifu,awe muwazi,awe na nidhamu, awe mkweli, mpenda haki, awe muelewa, mwenye maono pia akubari kuwajibika bila kinyongo.sifa hizi watanzania wengi hatuna.
  tumezoea kufanya mambo kiujanja ujanja tu, kiusanii au kwa lugha ya kisasa tumezoea kuchakachua kila jambo.

  Ndg yangu jaribu kutafuta wazo, kisha fanya wewe mwenyewe,cha mhimu ni kuwa na timu nzuri ya watu wa kukushauri juu ya wazo husika,pia katika kusimamia kazi.Lazima uwe makini sana na suala la Management kwani ndiyo mhimili wa kazi,ukilala hapo ujue imekura kwako.

  Wasiliana na Babalao atakupatia mawazo mazuri tu,mie namjua hana shida ilimradi umuandalie vijisenti vya kupelekea watoto wake nyumbani.Mungu akubariki ndg Yangu.
   
 9. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,306
  Trophy Points: 280
  Kasamali,

  Unawazo zuri lakini approach mmh hata mimi inanitisha kidogo. mimi ni business consultant
  nimefanya hiii kazi mora than 10yrs in Tanzania, Sudan, Kenya na hata Ulaya. Kwanza hakuna nchi nzuri ya kuwekeza kama Tanzania (unaweza usikubaliane nami lakini huo ni ukweli).
  Mimi naweza kukupatia ideas nyingi na nzuri saaaana lakini ethics za business zinasema a good business Idea ni ile unayoidevelop mwenyewe na sio copy na kupaste. Kwa nini usije kwetu na 2 or three business idea then tukusaidie kuidevelop kuliko kutegemea za watu.

  Karibu sana kama utapenda kufanya kazi nasi. tuwasiliane kwenye PM for more info
   
 10. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Mkuu hapo napingana nawewe. Watz ni waaminifu sana. Kwanza mliaminiana ndio maana mliamua kuanzisha kampuni pamoja. Usinge kuwa unamwamini definitely usinge ungana nae. Tatizo liko kwako mkuu both of you mlikua na poor administration plan and you had no forecast na pia hapo lazima communication ilikuwa very poor. Ukichunguza sana chanzo cha kuporomoka katika shughuli yeyote kwa wanao fanya kazi pamoja tatizo linaanzia kwa mawasiliano kati ya two parties. Ungekua mfuatiliaji, mgefika mbali.
  BUT ukifanya kazi na mtu usiomwamini kazi itafanyika tena vizuri bcoz utakua unafuatilia kila cent na kila shughuli. Mimi katika makampuni yangu sipendi kufanya kazi na mtu nae mwamini bcoz i will find my self in Limbo kwa kudhani kwamba mwenzangu anafanya kazi nzuri kumbe anachakachua tu. So please ukitaka kufanya kazi na mtu yeyote na mahalipopote usimwamini mtu kabisa, fuatilia kilakitu ambacho unajua you invested your money.
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Fungua financial institutions kama ilivyo FINCA, PRIDE, SEDA, WEDAC, Bay Port n.k

  kwa mtaji wa USD 4million itatosha sana
   
 12. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kasamali naona bado... hajapata muda kuendeleza mada, au hii ni chemsha bongo?...
  Kwa wale wanaosema kuwa M-TZ haaminiki, napenda kupinga hilo jambo. Wewe kama mwekezaji inabidi ufanye due diligence ya hali ya juu kabla haujatoa hiyo investment yako kwenye hiyo partnership.
  Pia ikumbukwe, hii ni biashara na sio urafiki, kwani communication channels zinabidi ziwe of highest standard kuiimarisha hiyo partnership na biashara yenyewe. Usitegemee tu kuwa mnaaniniana bali every aspect of the business, any change however minor should be communicated.

  You also don't expect that mwenye capital pia awe amebarikiwa pia na kuwa na ideas.
   
 13. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kassamali kabla ya kuenda mbali nikuulize je una uzoefu gani katika mambo ya biashara ama ujasiriamali? Kwa kweli katika suala zima la ujasiriamali sehemu ngumu ni kuzaa wazo ( business ideas) vengine vyote vinafuatia Business plan, funding etc.
  Sidhani kama unaweza kupata mafanikio kwa kupewa ideas na mtu mwengine, ujasiriamali ni kutoa/kuzaa wazo toka kichwani kwako mwenyewe na baadae kuzifanyia kazi.
  Jengine hio return unayoitegemea katika kipindi kifupi kama cha miaka 5 is almost impossible (110% per year), unless uwekeze kwenye biashara haramu ( kuwapeleka vijana kwa Pele)
  Ushauri wangu ni kama wewe huna uzoefu basi jaribu kujiweka kama ni Venture capitalist, tafuta wajasiriamali wenye ideas za nguvu kama wanne u-spread $1M each on this 4 ventures, ila utegemee return ya 30% kwa mwaka ($1.3M) kwenye kila mradi.
   
 14. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi nina idea kwenye tourism tu.
   
 15. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  you sound like a CEO of a hedge fund!!
  Ni wazo zuri na naamini utapata watu hapa jamvini
   
 16. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wa Tz viboko kweli! Hv ni jambo la kuuliza kuh uaminifu wa wa TZ?Ila kama walivyosema wengi,a big part in any business is a right business idea,hayo mengine yote sio muhimu sana. Fuata ushauri wa baba lao.
   
 17. k

  kassamali JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wadau wa Jamvini nashukuru sana kwa michango yenu kila neno la kila mtu nalifanyia kazi na kwa kujibu swali la muheshimiwa hapa mimi kwa uzoefu ni mwanasheria ila naamini kitu kimoja maisha ni kujaribu katika kkona zote na kuona uzuri na ubaya wake.Natanguliza shukrani zangu
   
Loading...