Business dreams...?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Business dreams...??

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tumain, Nov 4, 2009.

 1. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nilipoanza biashara nilikuwa na dreams nyingi???...
  First, Nilianza kufikiria biashara za "estates" that is najenga nyumba za kupanga na kuuza ...nikakutatana na challenges zifuatazo..a)mtaji, na b) expertize...ningeshauri kama una backround ya civil engineering unaweza kufaulu kwenye hii business c) regulation/laws- kupata eneo la kujenga nyumba ni mlolongo mkubwa ajabu hapo bongo..unlike Zambia ambao it is very easy..unaweza kujenga nyumba za kupanga na kuuza kirahisi sana (have some there..nashauri wana JF muangaze na huko panalipa sana kama una uwezo)
  Second, Nilijaribu Retail shops..mini supermarkets..challenges uwizi na udokozo wa wafanyakazi utakupasua kichwa hata kama unawalipa vipi..just habit..pili competition ni kubwa nafikiri ni biashara ya kila mtu hapa bongo..nikaacha au ikanishinda!
  Third, transport...(hiace,daladala taxi) ..mama yangu wategemezi milion pasua kichwa (wafanyakazi wake) lakini inaleta kila siku kitu kidogo nyumbani..si rahisi kuacha kwasababu switching cost yake ni kubwa ..unakomaa nayo..natamani watokee wataalamu wa IT ili tuweke kama kitu fulani kwenye gari ili tuweze kumunita iko wapi na imetembea kilometa ngapi..waiting that to come ..not yet..in BTWN najua naibiwa lakini nafanya...
  Fourth, Kuuza nafaka (agricultural products) outside the country...hii bonge ya biashara..niko nayo kwa sasa...challenges (uwe tayari kukaa kijijini, kwa muda mrefu kulala kwenye magari ya mizigo etc..) ili ilipe ina involve some sort of manual activities..and kusubiri...prices zinabadilika mara kwa mara..uwe na stoo kubwa ya kuhifadhi..
  What have you tried and what are challenges....lets share business dreams???
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kusafirisha Mbuzi toka mikoa ya kusini kuja Dar,inalipa kiasi tatizo ukitumia usafiri wa umma,kama malori ya mizigo ni balaa tupu,likisimamishwa na wewe umelala,mbuzi wana njaa. Mkilala njiani vibaka. Ukituma mtu akakuchukulie sababu nyingi sana za kuongeza gharama,kama kawaida vijana wa Bongo. Lakini kama una usafiri wako,mbuzi wanalipa sana ukienda vijijini,ila uwe na sehemu ya kuwashusha ambapo ni sehemu yako.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nilijaribu kufanya retail business (kny nafaka-mchele, maharage,kunde, njegere etc) maeneo ya Buguruni Sokoni tena nikiwa chuo UDSM.....! Business ya mazao ya chakula/nafaka inalipa sana Dar....inalipa sana tu! margin can go up to 30% (sometimes).

  Challenges;
  1. Inataka kuwa na usimamizi wa karibu sana...yaani ikiwezekana mwenyewe uwe dereva ...ukondoka tu, umeumia!
  2.Unahitaji mtaji mkubwa....kuweza kuwa na constant supply
  3. Vyanzo vya mazao (suppliers) sio wakuaminika sana.....i.e kuna kipindi business ya mchele inachanganya, lkn watu wakusupply hakuna...so km huna mtaji...ni loss kwako!
  4. Unahitaji uwe na eneo lako lakufanyia business (yaani usikodi hiyo sehemu)
  5. Yes, uswahilini...ndiko kuna market kubwa ya nafaka....but wanapenda sana kukopa, ukikubali hilo umeumia!
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Next level,
  Angalia namna ambavyo unaweza kuwa-supply kwenye soko kama la tandale...ukiweza kupenetrate hapo..itakusaidia sana..pale kuna wanunuzi wengi wa mazao/nafaka...
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wale jamaa wanalalia sana sometimes, kila mmoja anayeleta mzigo wanamtreat kama mkulima vile.....labda uwe na store kubwa pale Dar, then ukileta mzigo wako km bei sio nzuri au wanakuletea za kuleta unapiga store......! kwa uzoefu wangu kuretail inalipa sana sana dar, soko ni kubwa mno kama unamtaji mzuri na unasehemu nzuri ya kuuzia!

  Hata na hivyo nishakimbia huko!
   
 6. m

  majogajo JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mhhhhh
   
Loading...