Bush mdogo akaamuru kahaba anyongwe……………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bush mdogo akaamuru kahaba anyongwe……………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 13, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  PHO-10Sep23-254489.jpg
  Karla Faye Tucker akiwa gerezani
  1927731521_5aafea6d87_z.jpg

  thumb.png

  todd_232087_14[355356].jpg

  tuckerkarlafayebio.jpg

  0877887756.jpg 0877887756.jpg

  Picture 9.png


  karlafayetucker.jpg
  Mlo wake wa mwisho kabla ya kunyongwa

  Kati ya saa 8:30 na 10:30 za usiku ya Jumatatu Juni 13, 1983 Karla Faye Tucker, Danny Garrett na James Leibrant waliondoka nyumbani kwa Karla. Walikuwa na sherehe ndogo, ambapo walitumia madawa ya kulevya aina ya Methadone, Heroin, Dilaudid, Valium, Placidyls, Somas, Wygesics, Percodan, Mandrax na Bangi, pia walichanganya na pombe kali aina ya Rum na Tequila kwa wingi. Karla binti wa miaka 23, kahaba wa mtaa alionekana kupata nishai kutokana na pombe na madawa ya kulevya aliyotumia, lakini alimudu kutembea, kuongea na pia kushiriki katika mazungumzo yao kwa usahihi kabisa pamoja na kuonekana kuzidiwa na uraibu huo.

  Alimweleza Leibrant kwamba anataka kwenda nyumbani kwa Jerry Lynn Dean kuchukuwa fedha zake na kumtisha kidogo. Walikuwa wanazungumzia kuhusu kuchukuwa vitu iwapo Dean hatamlipa fedha zake, walizungumzia kuchukuwa Pikipiki, TV na seti ya mziki. Karla alikuwa amechukua kwa siri funguo kutoka kwa mke wa Dean aitwae Shawn lakini akamdanganya kwamba zimepotea. Wiki mbili zilizopita Karla alikuwa anazungumzia kuhusu kumfanyia jambo Dean.
  Walipofika kwa Dean, waliingia moja kwa moja hadi chumbani ambapo Karla alimkalia Dean na kumuwekea sururu (Pickaxe) shingoni na kumuamuru, "Usije ukasogea hata hatua moja mshenzi wewe, na ukikaidi umekufa." Dean alimuomba asije akamdhuru.

  Hata hivyo katika kujitetea Dean alimshika Karla ambapo Garrett aliingilia kwa kumpiga mapigo kadhaa kisogoni na nyundo aliyoipata hapo ndani. Baada ya kumpiga, Garrett alitoka kwenda kuchukua vipuli vya pikipiki vilivyokuwepo hapo ndani na kuvitoa nje ya nyumba hiyo na kuvipakia kwenye gari la Dean aina ya El Camino. Alimuacha Karla pale ndani.

  Kitendo cha kupigwa nyundo kichwani kilisababisha Dean awe anakoroma kwa sauti. Karla alitaka kumnyamazisha asiendelee kukoroma hivyo akaamua kumpiga Dean na ile sururu kama mara 28 hivi, na kwa mujibu wa maelezo yake alidai kwamba kila alipokuwa akimpiga Dean na ile sururu alikuwa anajisikia kufika kileleni kama vile anajamiiana.

  Leibrant alisema kwamba, baada ya kuitwa na Garrett pale chumbani kwa Dean alisikia sauti ya mtu akikoroma kama vile pampu ya kwenye aquarium ya kufugia samaki. Alipoingia ndani ndipo aliposhuhudia Karla akichomoa sururu (Pickaxe) kutoka mwilini mwa Dean huku akitabasamu na kisha kupiga tena pigo lingine. Leibrant aliondoka katike eneo la tukio na baada ya kutembea mwendo wa saa nzima alimpigia simu rafikiye aitwae Ronnie Burrell ili aje kumchukuwa na gari.
  Garrett na Karla walichukia kwa kitendo chake cha kuondoka katika eneo la tukio, lakini ili kujenga mazingira mazuri ya urafiki wao baadae Leibrant aliamua kumsaidia Garrett kwenda kutelekeza gari la Dean aina ya El Camino jioni ya siku ile katika eneo moja la kuegeshea magari.

  Garrett alitoka pale chumbani na kwenda kuendelea kupakia vile vipuli vya pikipiki kwenye gari lake aina ya Ranchero.

  Kulikuwa na mwanamke aliyekuwa amejificha kitandani akiwa amejifunika na shuka kwenye kona ya kitanda. Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Deborah Thornton, 32, mfanyakazi wa ofisini, alikuwa amegombana na mumewe siku hiyo na kuondoka hapo nyumbani kwao kwa hasira, aliamua kupitisha siku ile akiwa nje ya nyumbani kwake ambapo alikutana na Dean kwenye sherehe moja mchana wa siku ile na ndipo walipoamua kuondoka pamoja. Kwa sababu taa ilikuwa inawaka pale chumbani wakati Karla alipokuwa akimshambulia Dean na ile sururu ambapo Dean alikuwa akimtaja jina lake mara kwa mara, Karla aliamua kumuua mwanamke yule. Alimkabili na ile sururu lakini alimparuza begani hivyo yule mwanamke akamshika Karla na kuanza kukabiliana naye. Garrett alirejea pale chumbani na kuwakuta Karla na yule mwanamke wakikabiliana. Aliwatenganisha, lakini Karla aliendelea kumpiga yule mwanamke na ile sururu mara kadhaa kabla hajamalizia kwa kumpiga nayo moyoni na kumuua pale pale.

  Asubuhi ya siku ile baada ya tukio lile la mauaji, Karla alifika nyumbani kwa Douglas McAndrew Garrett, kaka yake Danny Garrett. Ilikuwa ni majira ya saa 12:30 hivi za alfajiri, akiwa na gari la Dean aina ya El Camino ya bluu. Baada ya kuteremsha vile vipuli vya pikipiki, alimsimulia Douglas jinsi alivyomuua Dean kwa kumpiga na sururu mara kadhaa na kila pigo moja alilokuwa akimpiga, alikuwa anafika kileleni kama vile anajamiiana. Alimpa Douglas pochi ya Dean, lakini Douglas aliichoma moto kwenye kizimio cha sigara. Ingawa aliwaambia waondoe vile vipuri vyao haraka sana hapo kwake, lakini baadae aliamua kumruhusu mdogo wake yaani Danny Garrett kuhifadhi baadhi ya vipuli hivyo pale kwake. Hata hivyo wiki tano baada ya tukio lile alikwenda kuvitelekeza mtoni kabla hajakwenda polisi kuripoti juu ya tulio hilo.

  Miili ya wahanga wale iligunduliwa na mfanyakazi mwenzie Dean aitwae Gregory Scott Traver siku hiyo ya June 13. Hiyo ilikuwa ni baada ya Dean kutompitia yeye Gregory wakati wa kwenda kazini kama ilivyo kawaida yake, Gregory aliamua kumfuata rafikie nyumbani kwake ili kujua kulikoni. Alipofika aliukuta mwili wa Dean ukiwa chumbani pamoja mwili wa Deborah Thornton ukiwa bado uko na ile sururu iliyokitwa moyoni.

  Gregory pia aligundua kuwa gari la Dean aina ya El Camino pamoja na pikipiki vilikuwa havipo na TV pia ilikuwa haipo. Jioni ya June 13, Karla na Garrett walikuwa wanaangalia TV wakati habari ya mauaji hayo ya kikatili yaliyotikisa jimbo hilo la Texas ikitangazwa. Karla na Garrett walicheka kwa kebehi kwamba sasa wamekuwa maarufu. Walimuita Leibrant ili na yeye aone habari hiyo.

  Taarifa ya uchunguzi wa madaktari ilibainisha kwamba marehemu Dean alikuwa ameshambuliwa zaidi maeneo ya kichwani, alikuwa na majeraha yapatayo 28 kichwani na 20 kati ya hayo yalikuwa ni mabaya sana kiasi cha kuvunja fuvu la kichwa. Deborah Thornton, kifo chake kilitokana na majeraha yaliyokutwa kifuani mwake na jeraha lingine la kupigwa na kitu kizito lilikutwa mgongoni. Sururu iliyokutwa katika eneo la tukio ndiyo iliyotumika katika kutekeleza mauaji hayo.

  Polisi walikuwa na taarifa zinazoweza kuwapata wauaji, lakini iliwachukua hadi wiki ya tano ndipo Douglas Garrett alipompigia mpelelezi wa Polisi aliyejulikana kwa jina la J. C. Mosier wa kituo cha Polisi cha Houston ambaye ni rafiki wa familia yao, na kumweleza juu ya wahusika wa mauaji hayo.
  Mosier alikutana na Douglas akiwa na mpenzi wake Kari Burell dada yake Karla Faye siku iliyofuata. (Kari Burrell na Douglas McAndrew Garrett walioana baadae). Walimweleza kwamba mdogo wake yeye Douglas aitwae Danny Garrett na mdogo wa mpenzi wake yaani Kari Burrell aitwae Karla Faye Tucker ndio waliohusika na mauaji hayo ya kutisha. Pia walimpa jina la James Leibrant kwa maelezo kwamba alishuhudia mauaji hayo. Baada ya kuzungumza na maafisa wa upelelezi waliokuwa wakipeleleza kesi hiyo Douglas alikubali kuvaa kifaa maalum cha kurekodia ili aweze kuwasaidia kukusanya ushahidi wa kile alichokisema kwao.

  Siku chache baadae Douglas aliendesha pikipiki yake hadi nyumbani kwa Karla mtaa wa McKean Houston. Alipofika aliwakuta Danny Garrett na Karla Faye na baada ya mazungumzo fulani fulani, ndipo walipozungumzia kuhusu mauaji hayo waliyoyafanya huku wakijisifu kwamba wamekuwa maarufu kwa kufanya mauaji kwa kutumia Sururu (Pickax Murderer). Mazungumzo hayo yalirekodiwa kwenye kifaa cha kurekodia alichokuwa amekibeba Douglas.

  Siku hiyo hiyo baada ya Douglas kuondoka nyumbani kwa Karla, aliupeleka mkanda uliorekodi mazungumzo hayo ambayo ndio yaliyopelekea kukamatwa kwao. Garret na Karla walikamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo na ambapo waliwekwa ndani wakisubiri kufikishwa mahakani kusomewa mashtaka. Hata hivyo James Liebert na Ronnie Burrell nao walikamatwa ili kuisaidia Polisi katika upelelezi wakesi hiyo.

  Hivi huyu Karla Tucker Faye ni nani hasa?

  Kwa nini kesi yake ilivuta hisia za watu wengi, si nchini Marekani tu bali pia duniani kote?

  Naomba ufuatane na mimi katika simulizi hii nyenye kusisimua.

  Karla Faye Tucker mwanamke mrembo na kahaba, mcheza show wa bendi za Rock, mtumiaji madawa ya kulevya na aliyekuwa akifurahia kuendesha pikipiki kwa fujo na mbwembwe alizaliwa na kukulia katika mji wa Houston jimboni Texas nchini Marekani hapo mnamo Novemba 18, 1956. Alikuwa ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti watatu katika familia yao. Baba yake Larrry alikuwa akifanya kazi huko Ghuba ya Mexico. Kutokana na matatizo ya ndoa yaliyoikumba familia hiyo, Karla alianza kuvuta bangi akiwa na umri wa miaka nane. Alipofikisha umri wa miaka kumi, wazazi wake waliachana. Wakati wazazi wake wakiwa kwenye mchakato wa kuachana, ndipo alipogundua kwamba yeye sio mtoto wa ndani ya ndoa ya wazazi wake na ndio chanzo cha kutengena kwa wazazi wake.

  Alipofikisha umri wa miaka 12, alianza tabia ya kutumia madawa ya kulevya pamoja na ukahaba. Akiwa na umri wa miaka 14 alishindwa kuendelea na masomo na kuungana na mama yake katika kundi la muziki la Rock na pia akijiuza kwa wanaume.
  Alianza kusafiri huku na huko na makundi ya muziki wa Rock kama Allman Brothers, The Marshall Tucker na The Eagle. Akiwa na umri wa miaka 16 aliolewa na mtu aliyejulikana kwa jina la Stephen Griffith fundi makanika ambapo alidumu katika ndoa hiyo kwa miaka 6 tu.

  Akiwa ndio anatimiza miaka 20, alikutana na mwanamke mmoja aitwae Shawn Dean mkewe Jerry Lynn Dean ambao walimtambulisha kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Danny Garrett mwaka 1981.Mnamo Septemba 1983 Karla na Garrett walishitakiwa kila mtu kivyake kwa kosa la mauaji. Karla alikana mashtaka na waliwekwa ndani wakisubiri kesi yao kusikilizwa.

  Akiwa jela, siku moja alichukua Biblia kutoka katika kitengo cha dini hapo jela na alikwenda moja kwa moja kwenye selo yake na kuanza kusoma. Baadae aliwaambia marafiki zake, "Sikujua ni kitu gani nilikuwa ninasoma na nilipojua nilijikuta nikipiga magoti na kumuomba mungu anisamehe"
  Karla alijiunga rasmi na ukristo hapo mnamo Octoba 1983, baadae aliolewa na mchungaji ambaye alikuwa ni mfungwa mwenzie aliyejulikana kwa jina la Dana Lane Brown ambapo walifunga ndoa na kufuatiwa na sherehe hapo hapo jela.

  Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake, siri nyingi kuhusu maisha yake zilifichuliwa pale mahakamani. Ilielezwa kwamba Karla alikuwa na vitendo vya kikatili hata alipokuwa shuleni. Alikuwa na tabia ya kupenda shari na ugomvi usio na sababu na mara nyingi alikuwa anapigana na wanaume na hiyo ilitokana na tabia yake ya kutumia Bangi na madawa ya kulevya.

  Kuhusu maisha yake ya ndoa, ilielezwa kwamba, ndoa yake haikupata kuwa na amani tangu alipooana na mumewe Stephen Griffith, kwani mara nyingi walikuwa na ugomvi usioisha na mara zote Karla ndiye aliyekuwa akianzisha ugomvi huo na ndio sababu ndoa yake haikudumu.
  Kwa upande wake Karla alidai kwamba kilichopelekea yeye kumuua Dean siku hiyo ilitokana na chuki aliyokuwa nayo dhidi yake siku nyingi. Karla alikasirishwa na kitendo cha Dean kuegesha pikipiki yake iliyokuwa ikivuja oil sebuleni kwake ambapo oil hiyo iliiharibu picha pekee aliyopiga na mama yake. Kitendo hicho kilisababisha yeye Karla kujenga chuki dhidi ya Dean.

  Akitoa ushahidi hapo mahakamani dhidi ya mdogo wake. Kari ambaye ni dada yake Karla alisema kwamba, kuna siku aliwasikia Garrett na Karla wakisema kwamba watawauwa Leibrant na Ronnie kwa sababu ya kuwazuia wasije wakawataja wao kuhusu kuhusika kwao na mauaji hayo. Pia Karla mwenyewe aliwahi kukiri hapo mahakamani kwamba walikuwa na mkakati wa kuvamia maabara moja haramu inayotumika kuzalisha madawa ya kulevya na kuwauwa wahusika na kupora mali zao.
  Pamoja na hukumu ya kunyonga kuwa ni vigumu kutolewa kwa wanawake katika jimbo hilo la Texas, lakini mwishoni mwa mwaka 1984, Karla na Garrett walihukumiwa kunyongwa (Garrett alifariki hapo mnamo mwaka 1993 wakati akisubiri kunyongwa kwake. Alikufa kwa ugonjwa wa ini).

  Karla alishirikiana selo moja na mfungwa mwenzie waliokuwa wakisubiri kunyongwa aitwae Pam Perillo, ambaye hata hivyo hukumu yake ilitenguliwa na kufungwa kifungo cha maisha.Kati ya mwaka 1984 na 1992 majaribio kadhaa ya kutata kesi hiyo isikilizwe upya yalikataliwa. Lakini ilipofika Juni 22, Karla alidai kwamba maisha yake yalitawaliwa na matumizi ya madawa ya kulevya na siku ya tukio hilo la mauaji alikuwa kwenye ushawishi wa madawa ya kulevya.

  Karla alituma maombi katika Bodi ya msamaha na vifungo vya nje mara kadhaa akiitaka imuonee huruma na kumpunguzia adhabu, lakini maombi yake yalikataliwa. Maombi yake yalivuka mipaka nje ya Marekani na ndani ya Marekani kwenyewe. Miongoni mwa waliomuombea apunguziwe adhabu walikuwa ni aliyekuwa Kamishna wa Umoja wa Mataifa Waly Bacre Ndiaye, Hayati Papa John Paul II wa Kanisa Katoliki Vatikan, Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi, aliyekuwa Spika wa Bunge la nchini Marekani Newt Gingrich, Mhubiri wa kwenye Luninga Pat Robertson, pamoja na Ron Carlson kaka yake marehemu Deborah Thornton aliyeuawa na Karla.

  Mkuu wa Gereza la Texas Huntsvile alisema kwamba Karla alikuwa ni mfano mzuri kwa wafungwa pale gerezani na kwa miaka 14 aliyokaa gerezani akisubiri kutekelezwa kwa hukumu yake ya kunyongwa alikuwa amebadilika sana kitabia. Lakini maombi hayo hayakusikilizwa na Bodi hiyo ya msamaha na vifungo vya nje.

  Akiwa hapo gerezani akisubiri kunyongwa, Karla alibadilika sana kitabia na alitumia muda wake mwingi sana kumtumikia Mungu. Wakati fulani akihojiwa katika kipindi kimoja kinachorushwa na TV ya ABCNEWS, Alisema, "kiukweli huwezi kusema kwamba kuuwa kikatili watu wawili wasio na hatia ni jambo jema, si kweli hata kidogo, lakini baada ya hapo, kilichonitokea ni kubadilika na kuwa mtu mwema"

  Kwa mujibu wa sheria za jimbo la Texas, Gavana wa jimbo hilo, ambaye wakati huo alikuwa ni George W Bush (Mdogo) kabla ya kuwa rais wa Marekani kati ya mwaka 2001 mpaka 2009, ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kutengua adhabu hiyo.

  Maelfu ya watu maarufu walimuandikia barua ya kumtaka atengue adhabu ya kunyongwa kwa Karla, miongoni mwa waliomuandikia ni pamoja na Karla mwenyewe, Hayati Papa John Paul II na Cardinal O'Connor.

  Katika barua yake aliyomuandikia Gavana Bush, Karla Faye alisema:-

  Sijaribu kupunguza kiwango cha kosa hili baya nililolifanya, kwa ukweli ni kosa kubwa na la kutisha na ninawajibika kwa kile kilichotokea…… najua pia kwamba haki na sheria zinahitaji uhai wangu kwa ajili ya watu wale wawili wasio na hatia niliokatisha uhai wao kikatili usiku ule. Kama adhabu ya kunyongwa ndiyo njia pekee na ya mwisho ambayo itatimiza madai na kurejesha haki,….nakubaliana nayo…. Nitakubali kuwajibika kwa namna yoyote sheria itakavyotaka.

  Nilishauriwa na wanasheria waliokuwa wakinitetea nikane mashtaka hayo, na nilikuwa nikiwaamini wataalamu hawa wa sheria. Walikuwa wanajua kwamba nimewauwa Jerry na Deborah. Sikuwadanganya kuhusu kuhusika kwangu na mauaji hayo, kiukweli mimi nina hatia, nina hatia kwa kosa hilo. Niliwahi kumlaumu mama yangu kwa sababu yeye ndie aliyekuwa mlezi wangu na nilimuangalia kama mfano, na ndiyo aliyenikuza katika malezi haya mwanzoni kabisa mwa utoto wangu.

  Nikiwa na umri wa miaka 14, alinichukua na kunipeleka kwenye maeneo ambayo yalikuwa na wanaume na alinifundisha na mimi niwe binti wa kujiuza kwa wanaume hao. Nilitaka kumridhisha mama yangu, nilitaka ajivunie kuwa na mtoto mtiifu kwake kama mimi, hivyo badala ya kukataa, nilijaribu kila alichoniambia. Kitu ndani kabisa ya moyo wangu kiliniambia kwamba ninachofanya si sahihi. Haikuwa ni kanuni ya kundi nililokuwemo, ilikuwa ni kanuni ya familia nilimozaliwa.

  Sitaki kuhamisha lawama kwa mama yangu au jamii, wala silaumu madawa ya kulevya. Nilikuwa kwenye nishai ya madawa ya kulevya usiku ule wa mauaji ya kutisha ya watu wawili wasio na hatia. Nasikitika kwamba niliamua kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya. Kama nisingetumia madawa ya kulevya usiku ule naamini wale watu wawili wangekuwa hai leo. Lakini kwa sababu nilichagua kutumia madawa ya kulevya, yalinipoteza na leo hii watu wawili wasio na hatia wamekufa kwa sababu yangu.

  Sikupanga kwenda katika nyumba ile usiku ule, kwenda kuuwa mtu yeyote. Lakini hiyo sio sababu. Ukweli ni kwamba, tulikwenda katika nyumba ile, na tukauwa kikatili watu wawili wasio na hatia. Tuliondoka pale na kwa takriban mwezi mzima tulikuwa tukijisifu kwa mauaji yale. Ilikuwa ni Octoba, miezi mitatu tangu niwekwe ndani, wakati mchungaji aliponijia katika selo yangu na nilikwenda katika huduma ya kiroho. Usiku ule nilikubali kumpokea Yesu moyoni mwangu. Kitendo hicho kilinifanya nihisi uzito wa jambo nililolifanya ……… nilianza kulia kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya kutofanya hivyo.

  Pia nilijaribu kutuma hela kwa mmoja wa watoto wa wahanga wale, mtoto wa kiume wa Deborah kwa ajili ya shule, lakini kaka wa Marehemu Ron alipokuja kuniona mwaka 1992 aliniambia kwamba amenisamehe kwa kile nilichokifanya kukatisha uhai wa dada yake, nilimfahamisha kwamba nilitaka kumtumia fedha mpwa wake. Aliniambia nisifanye hivyo, kwani nitamuumiza zaidi iwapo nitamtumia hizo fedha. Aliniambia kwamba mpwa wake hatapokea fedha kutoka kwangu kwa sababu hana la kufanya juu yangu. Nilielewa maumivu yake na sikulazimisha.

  Miaka 14 iliyopita nilikuwa sehemu ya tatizo. Sasa nimekuwa sehemu ya suluhisho. Niliamua kufanya matendo mema kwa miaka 14 sio kwa sababu niko jela nikisubiri kunyongwa, lakini ni kwa sababu Mungu aliye mbinguni amenitaka nifanye hivyo. Sasa hivi najua mema na mabaya, ni lazima nifanye mema. Nafikiria iwapo ningekuwa sijakamatwa, labda ningekuwa bado naendelea na vitendo vyangu vya kupigana na kuwaumiza wengine na sio kujaribu kufanya matendo mema. Naamini unanichukulia hivyo. Kwa kweli sielewi kwa nini hutaki kuchukulia mabadiliko yangu ya kitabia na kunitendea wema.

  Sijui ni vigezo gani vinaangaliwa wakati wa hukumu ya adhabu ya kifo, lakini nakuhakikishia kwamba, kama utaibadilisha adhabu yangu na kuwa ya kifungo cha maisha, nitaendelea katika kipindi cha maisha yangu katika ulimwengu huu kuwafikia wengine na kuwabadilisha kimtazamo na kuwa wema katika maisha yao. Nawaona watu hapa Gerezani nilipo ambao wengine wapo hapa kwa makosa ya kutisha, na bado wapo wengine huko uraiani ambao bado wanaendelea na vitendo vya kikatili na kuwaumiza wengine. Nakuhakikishia nitawafikia hawa wasichana na kuwabadilisha kitabia kabla hawajawadhuru watu wengine.

  Nakuomba uibadilishe adhabu yangu na kuwa ya kifungo cha maisha ili niilipe jamii kwa kuwasaidia wengine. Siwezi kurudisha uhai wa wale niliowauwa. Lakini naweza iwapo nitaruhusiwa kuokoa nafsi nyingine zilizopotea. Hicho tu ndicho nitakachoweza kurudisha………………..

  Mwisho wa barua hiyo.

  Hebu fikiria, kati ya wajumbe 18 wa bodi hiyo 12 waliteuliwa na Gavana Bush mwenyewe, hakuna aliyetarajia kama Gavana Bush angetengua uamuzi wa Bodi hiyo, na kiukweli hilo halikutokea.
  Gavana Bush akizungumza na waandishi wa habari alisema,

  "wakati nilipoapishwa kama Gavana wa jimbo hili la Texas, niliapa kwamba nitatekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa sheria za jimbo hili ikiwemo sheria ya kunyonga. Jukumu langu ni kuhakikisha sheria zinafuatwa na haki inatendeka bila kuangalia umuhimu wa mtu. Karla Faye Tucker alikutwa na hatia ya mauaji ya kinyama. Alikutwa na hatia ya kosa hilo na alihukumiwa kwa mujibu wa sheria. Mahakama Kuu ya nchi hii iliipitia hukumu hiyo na mimi sitabadili chochote. Namuombea Mungu ambariki Karla Faye Tucker na ninawaombea wahanga wake na familia zao."

  Mnamo Februari 2, 1998 Karla alisafirishwa kwa ndege kutoka jela ya Gateville hadi jela ya Huntsville akisubiri utekelezaji wa hukumu yake ya kunyongwa kwa kuchomwa sindano ya sumu.
  Siku ya Jumanne ya tarehe 4 Februari 1998 ndiyo siku ambayo Karla alikuwa anyongwe, umati mkubwa wa watu walikusanyika nje ya jela hiyo pamoja na kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakilaani kitendo hicho cha kunyongwa kwake lakini wengine wakishangilia kwa nguvu na wengine walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "Karla lazima afe."

  Akizungumzia kuhusu hukumu hiyo aliyewahi kuwa mumewe na Karla Faye Stephen Griffith alisema kwamba, Karla atakuwa sasa ametimiza ndoto zake za kuwa maarufu. "mara nyingi alikuwa akinimbia kwamba siku moja atakuja kuwa maarufu" Griffith alinukuliwa na gazeti moja la mji huo wa Houston. Griffith alioana na Karla Faye na kudumu katika ndoa yao kwa muda wa miaka 6, hata hivyo hakuhudhuria kunyongwa kwake.

  Karla aliwaambia marfiki zake kwamba imani yake kwa Mungu haitetereki. Ilipofika saa 11:30 jioni alikula chakula chake cha mwisho. Na ilipofika saa 12:00 alipelekwa umbali wa mita 15 kwenda chini kwenye chumba cha kunyongewa akiwa amevaa mavazi meupe.

  Karla alichagua watu wa kushuhudia kunyongwa kwake, watu hao walikuwa ni mume wa marehemu Deborah Thornton aitwae Richard "Tony" Thornton ambaye aliridhia kunyongwa kwa Karla Faye, pamoja na yeye aliandamana na binti yake Katheryn Thornton na William Joseph Davis mtoto wa Deborah aliyempata katika ndoa yake ya kwanza, hawa nao pia waliridhia hukumu yake ya kunyongwa, kaka yake Deborah aitwae Ronald Carlson, huyu alipinga adhabu hiyo ya kunyongwa, pia alibadilika kiimani na kuwa mtu wa dini.

  Hii ndiyo ilikuwa kauli yake ya mwisho kwa familia hiyo ya wahanga:-

  "Ningependa kuwaambia wote, familia ya Deborah Thornton na familia ya Jerry Dean, kwamba naomba mnisamehe sana. Naamini Mungu atawapa amani kwa hili. Mwanangu, nakupenda sana Ron, naomba umkumbatie Peggy kwa niaba yangu. Kila mtu alikuwa mwema kwangu. nawapenda sana nyote. Nakwenda kukutana uso kwam uso na Yesu Kristo sasa. Askari Magereza Bagget, nakushukuru sana, ulikuwa mwema sana kwangu, nawapenda wote. Nitaonana nanyi mnakapokuaja huko mbinguni. Nitawasubiri."

  Baada ya kumaliza kuongea alilazwa kwenye kitanda cha kinyongewa na kufungwa na mikanda, baada ya amri kutolewa, mtu asiyefahamika alikwenda kumchoma sindano iliyokuwa na mchanganyiko wa Sodium Thiopental, Pancuronium Bromide na Potassium Chloride kwenye mshipa wa damu, muda mfupi Karla alivuta pumzi mara mbili kisha akakakoroma kidogo kisha kimya. Muda mfupi baadae Daktari alifika kwenye chumba hicho na kumulika machoni mwa Karla, na kisha akapumua kwa sauti. "Amekwisha kufa" alisema daktari yule. Ilikuwa ni saa 12:45 za jioni.
  Alizikwa katika makaburi ya Forest Park Lawndale katika mji wa Houston.

  Mnamo mwaka 2004 ilitolewa sinema ya maisha yake ikiwa na jina la "Forevermore" na aliyecheza sinema hiyo ni mwigizaji Karen Jezek.

  Sinema yenyewe nimeiambatanisha na simulizi hii, hapa chini:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Gustavo bravo! Ngoja nisome
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah story ndefu hii ngoja nibusti koka na chungwa.
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida leo siku ya Ijumaa, nimeweka simulizi hii ambayo kwa kweli inasikitisha, kuhuzunisha na pia inafundisha.
  Ningependa kumshukuru NATA kwa kuniomba niweke simulizi hii ambayo kwa kweli baada ya kumaliza kuiandika na kuisoma, nilijikuta mwili mzima ukinisisimka. lakini kilichonihuzunisha zaidi na kunipa simanzi ni filamu niliyoiambatanisha na habari hii.

  Simulizi hii inafundisha mambo mengi tu, lakini binafsi nimeona mambo matatu.
  1. Kwanza malezi ya watoto wetu ni jambo la kuzingatiwa sana, je wanandoa wanaishi maisha ya aina gani? Je kuna kuamainiana? Je watoto wanajifunza nini kwa wazazi? Je wanajua athari za Pombe na madawa ya kulevya?
  2. Pili inafundisha kuhusu imani, Je tumewaweka watoto wetu karibu na Mungu kwa kiasi gani? Je wanajua mema na mabaya?
  3. Ni kuhusu Vipaji na ndoto za watoto wetu. watoto wetu wanaposema wangependa kuwa maarufu, inabidi wawe na uhakika wanazungumzia umaarufu wa aina gani (specific) kwani kinachokwenda katika fikra zetu au mawazo yetu ya kina (Subconscious Mind) ambayo yenyewe hayajui kuchagua kwamba unataka umaarufu gani. kuna uwezekano wa kuwa maarufu kwa kubaka au kwa kufanya mauaji..............Kwani kama ukitangazwa kwenye vyombo vya habari kama umefanya mauaji ya kutisha, si ni umaarufu pia? Kama tulivyoona kwa Karla Faye Tucker, yeye alisema anataka kuwa maarufu na kweli kawa maarufu, lakini Je ni umaarufu gani alioupata?

  Niishie hapa, niwachie na wengine wachangie.
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asante sana Mtambuzi yaani inasikitisha sana!

  Niliona watu walivyokuwa wakimtetea jamani .

  Huyu Bush angemuulumia bado wale wamabango na ndugu wa marehemu wangeweza kutomkubali kwenye jamii
  na wangeweza mfanyizia chochote.
   
 6. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh wangemhurumia kwani alisha tubu,
  it is very painful!
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Duh mkuu inasikitisha sana
  Ni funzo kubwa sana kwa wazazi wote wajue namna ya kuwalea watoto
  Asante sana mkuu
   
 8. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  duh sina la kusema.
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du nakupa Big Up hasa na nimeiweka ktk Bookmark nitaisoma kila siku na kuangalia YouTube
  Tatizo heading ilinitatiza
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka watu wengi walijaribu kumtetea kwa kuamini kuwa ametubu na ameokoka.

  Lakini wengine wakakataa wakidai kuwa watu hawaachi kabisa uovu wao na kuokoka si permanent
  so huyu dada anaweza kurudi mtaani na kurudia maisha yake yale nakuweza kuua zaidi au kuleta madhara makubwa zaidi.

  Kwa kweli inasikitisha jinsi anavyokufa kwa matumaini makubwa akiamini kuwa amesamehewa na amewafurahisha wale walioumizwa na vifo alivyosababisha!
   
 11. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Duh........Inasikitisha sana na naomba nikiri imenitoa machozi ya uchungu.

  Watoto wetu tunaposhindwa kuwasimamia vema na kuwaongoza/funza kuwa watu wenye matendo mema na kuuchukia uovu ni sisi wenyewe tunatengeneza bomu litakalotulipukia, tujitahidi kuwapa malezi mema ya elimu dunia na akhera.

  Najaribu kuilinganisha kesi hii na tuhuma zinazomtuhumu Lulu kwa sasa kwani tayari kesha tugawa watanzania ktk makundi mawili ya wenye kutaka aachiwe kwani hana hatia na wale wenye kutaka ahukumiwe kwani ana hatia, ni funzo kubwa kwetu tulio na watoto.
   
 12. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Very interesting. Mtambuzi, you are really a great thinker brother! Thanks very much for your time, making sure you post suck kind of educating threads. Big up!!
   
 13. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Angeanza yeye kwanza kuwahurumia aliowaua.
   
 14. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi, umeshawahi kumsikia Jeffrey Dahmer?
   
 15. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye red nimesikitika sana mkuu
  hiki nacho ni kipande kilichonisikitisha
  dah jamaa ana roho ngumu
  kwani ukimnyonga mtu ndio wale waliokufa wanarudi?
   
 16. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  why do we kill people, to show people that killing people is wrong?
   
 17. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani ukimuacha aishi wale aliowaua wanarudi?

  Na huyo mwanamke muuaji yeye hana "roho ngumu"?
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Habari MH

   
 19. a

  ammah JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  another great strory from Mtambuzi...very interesting...
   
 20. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unataka kung'atwa wewe?
   
Loading...