STIDE: Nikupe pole sana kwa changamoto hiyo uliyokutana nayo. Katika utafutaji wako wewe hukuangalia swala la imani, lakini wazazi wa huyo binti kwao ni muhimu sana. Swali la muhimu kwako, je uko tayari kubadilisha imani ili uweze kukubaliwa kupewa huyo binti??. Nafikiri huu ni uamuzi wa muhimu sana kwako. Kama huwezi, basi nafikiri anza mchakato upya, na ukimshirikisha Mungu ili akupe wa kufanana na wewe. All the best!