Busara za Mbowe zaonekana

Nafikiri Rufani ni muhimu kuangalia pia uwezekano wa kukwepa gharama za chaguzi ndogo japo CHADEMA wana uhakika wa kushinda hilo jimbo iwapo Mahakama itaamua uchaguzi urudiwe! Nafikiri pia kufanya hivyo kutasaidia kuanika uozo wa baadhi ya majaji kutumiwa na chama tawala kwa manufaa ya watawala. Na hili ni tatizo la kikatiba maana hao jamaa wanasubiri presidential appointments. Inabidi tufike mahali hawa watu wawe wanaomba hizo nafasi kupitia kwa wananchi na siyo kwa kujipendekeza kwa watawala! GO Goo Gooo CHADEMA! This is what leadership is all about! Ndiyo ukomavu wa kisiasa huo..
 
Huyu ana Hekima, Busara, Ushawishi, Uwazi, Ukweli na Ubunifu wa hali ya juu. Ni mara ya 2 nahudhulia mikutano yake. Sikumjua. Anaweza
 
Busara gani zinazotokana na kula ndumu na viroba!yaone Kombati kama wamepuuu
 
Wakati wote nakubali kuwa mbowe ni kiongozi mkuu, lakini nikiri kuwa binafsi sina imani na mahakama kwa hiyo siamini kama rufaa ni uamuzi wa maana. Wote ni mashahidi kwamba ktk siku za hivi karibuni mahakama imeonesha kupoteza mwelekeo, namshangaa kwa mara ya kwanza mbowe kwamba amesahau kuwa mashetani walishaweza kucorrupt mpaka rufaa iliyoamriwa na judge mkuu Ramadhan, ni ile ya mgombea binafsi. Mbowe kwa msisitizo amesema kuwa hukumu ile sio ya mahakama ni ya judge mmoja binafsi na kwamba ameambiwa na majaji wengi wastaafu kuwa akate rufaa, lakini mbona hajiulizi kuwa hao walikuwa wapi wakati maamuzi ya rufaa ya mgombea binafsi yanapindishwa. Mie naona kuwa huo ni mpango wa ccm kutimiza mpango wao wa kuipooza CDM ktk Arusha ikiwa ni pamoja na kumkomoa Lema. Na wanajua kuwa CDM isipokata rufaa basi uchaguzi utafanywa haraka na hawawezi kushinda hivyo watakuwa wamevuna mabua. Lakini rufaa ikikatwa basi hukumu itatolewa kuaanzia 2014 na muda wote huo jimbo litakuwa wazi bila mbunge, hapa tuangalie swala la madiwani waliotimuliwa na chadema linavyoendeshwa na hiyo hiyo mahakama. Hao anaosema majaji wanaosema akate rufaa ni ccm wa kutupwa.
 
kisheria CDM wanatakiwa kufanya yafuatayo-
1. kuiomba mahakama ya rufaaa kusitisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu hadi pale mahakama ya rufaa itakapotoa hukumu yake, hiki kikifanyika Mhe. Lema ataendelea kuwa mbunge wa Arusha Mjini hadi pale uamuzi wa mahakama ya rufaa utakapotolewa ; na

2. kuhusu gharama za kesi yule atakayeshindwa katika kesi itakayofunguliwa mahakama ya rufaa ndiye atakayelipa gharama zote za kesi kuanzia za mahakama kuu

huo ndio ufafanuzi wa ksiheria GT

Tunaomba magamba wajue CDM ni chama makini chenye watu na viongozi makini na kinachopendwa na watanzania,

napiata
 
Ningependa mnijuze endapo mh. lema ataruhusiwa kuhudhuria vikao vya bunge kama kawaida!
 
nimeshuhudia mbowe na lema wakijaribu kuwatuliza watu wa arusha.wamejaribu sana kuwzeleza wakazi wa arusha umuhimu wa kutulia
 
Nami pia naona uamuzi Wa kukata rufaa ni jambo lenye maslahi kwa rasilimali zetu. Kwanza kutamuondolea kikwazo ndugu Lema ili haki hake ya kuwa kiongozi isipokonywe bila sababu za msingi(ikumbukwe kwa jinsi judge alivyoamua kuchanganya vifungu makusudi, lema hataweza kugombea mwaka 2015 Kama judgement haitakuwa reviewed). Pili haki ya ya wananchi itakuwa imechukuliwa pasipo uhalali Kama judgement hiyo ikibaki
kwenye records. Ila wasiwasi nilionao ni je mahakama ya rufani irascible mda
 
Nami pia naona uamuzi Wa kukata rufaa ni jambo lenye maslahi kwa rasilimali zetu. Kwanza kutamuondolea kikwazo ndugu Lema ili haki hake ya kuwa kiongozi isipokonywe bila sababu za msingi(ikumbukwe kwa jinsi judge alivyoamua kuchanganya vifungu makusudi, lema hataweza kugombea mwaka 2015 Kama judgement haitakuwa reviewed). Pili haki ya ya wananchi itakuwa imechukuliwa pasipo uhalali Kama judgement hiyo ikibaki
kwenye records. Ila wasiwasi nilionao ni je mahakama ya rufani irascible mda gani kutoa uamuzi wa rufaa?
 
kwanza napenda kumpongeza sana mh. mbowe kwa dhati kabisa na leo mimi nilikuwa na ofu kubwa sana hule umati wa watu pale NMC. Ni busara ya hali ya juu sana, kwa sababu kama amri yoyote hile ingelitoka,na kwa umati hule na POLISI wale basi ungelikuwa tunaongea mengine.

MY TAKE
Naunga mkono sana CHADEMA kwa uamuzi wa busara wa kukata RUFAA na mtashinda tu kwa sababu JAJI RWAKIBARILA alijichanganya sana na CCM wanajua hilo.
Sababu za CHADEMA kushinda RUFAA ni hizi hapa:-

  1. Jaji hakukamilisha amri ktk uamuzi wake na kuacha baadhi ya mambo yakielea.
  2. Kifungu cha 114 cha sheria ya uchaguzi,jaji alipashwa kwenda mbali zaidi kwa kutamka adhabu zinazoambatana na makosa hayo badala ya kutangaza kutengua matokeo pekee.
  3. Anayetiwa hatiani kwa kifungu hicho anakabiliwa na adhabu ya kupigwa marufuku kushiriki chaguzi kwa miaka isiyozidi 5,lakini ktk hukumu yake hakutamka hivyo.
  4. Kosa la kashfa alilosema ili lithibitike ni lazima maneno yalitamkwa lazima yadhihilike kuwa ya uongo kwa sababu iwapo yaliotamkwa yana ukweli,haiwezi kuwa kashfa.
  5. Kama lema alitamka na kudhihilika km ni kashfa,basi shauri la kukashifiwa lingelifunguliwa na Dr. Burian mwenyewe na si mtu mwingine.
  6. Shauri la kashfa haliwezi kufunguliwa na mtu mwingine isipokuwa yule aliekashifiwa. Shauri la kashfa haliwezi kuwa na uwakilishi ndio maana ikitokea mlalamikaji ktk kesi ya kashfa anafariki dunia,basi shauri lenyewe nalo huishia hapo kwa sababu haliwezi kurithiwa.
  7. Dr. burian aliedaiwa kukashifiwa na lema hakuwai kufungua kesi ya kashfa wala kufika mahakamani kutoa ushaidi wa madai hayo licha ya jaji RWEKIBARILA kisisitiza umuhimu wa ushaidi wake kutokana na kutajwa na mashaidi wote 14
  8. Wadai hawakuwasilsha nakala za CD zinazomuonyesha lema akiutubia na kutoa maneno ya kashfa,udhalilishaji na ubaguzi kidini na kijinsia walizodai kuwa nazo.
  9. Dr. burian aliedaiwa kukashifiwa,hakuwahi kulalamika kwenye kamati ya Maadili ya Jimbo wala CCM hakikuwai kulalamika licha ya kupewa fursa hiyo kisheria.

Ni mengi sana na wanasheria wa CHADEMA nawajua sana walivyobobea ktk sheria na wameyaona mengi zaidi na ni uakika mh lema ataludishiwa ubunge wake.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi.
 
Jimbo liko wazi mpaka hapo uamuzi wa jaji Rwakibarila utakapotenguliwa! Lakini rufani itaamuliwa mapema zaidi kwani mahakama zimepewa muda wa kushughulikia kesi za uchguzi.
 
Kwa mara nyingine tena busara imetumika baada ya kutumia maneno ya kuwatuliza wanachama wa Chadema.

"Mahakama si mtu mmoja bado tuna majaji wengine wenye uelewa, tutakwenda huko kudai haki".

"Vijana tulieni tusionekane chama cha vurugu acheni wao waanzishe vurugu, lakini tuwe tayari kwa vurugu..dah!"

Hizi ni busara za hali ya juu tukubali tusikubali kama si kutuliza hasira kwa busara saa hizi tungekuwa tunasema mengine.

Kama serikali, Usalama wa Taifa, Polisi haioni umuhimu wa mtu huyu basi haitapata mwingine.

Absolutely! Frankly speaking kukosekana hiyo kitu (hekima na busara) miongoni mwa viongozi na wananchama wa CUF ndiko kulikochangia kwa zaidi ya 90% kuimaliza CUF pamoja na nafasi kubwa sana kilichokuwa nayo kama chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Viongozi wa CUF na wanachama wao daima walionekana watu wenye shari kwenye mikusanyiko, mikutano, na maandamano yao mbalimbali na ile slogan yao ya NGANGARI ndio kabisa ilichafua image ya CUF kwa wananchi wapenda amani. Wananchi wanahitaji amani na sio shari.

Kama alivyosema Mh. Mbowe daima amani itawale, wanachama na wapenzi wa CDM wapende amani - KAMA NI VURUGU WAANZISHE 'WAO' BALI WANANCHI WAWE TAYARI KWA HILO - what a wonderful thinking!

Chadema na vyama vingine makini havihitaji kuwa na kauli za kutishatisha wananchi kama ngangari, ngunguri, au matawi yenye majina ya kishenzi kama Chechnya, Tora Bora, Hamas, Ukanda wa Gaza, ... kama ilivyokuwa kwa wengine ambao leo hii wamebaki historia. Wakithubutu kufanya hivyo watatoweka kama giza mbele ya nuru.

Viva Mbowe, viva CHADEMA.
 
Of course, Mh. Mbowe ana-busara sana, kama asingekuwepo Daktari Slaa angekuwa ametupeleka kwenye matatizo.... Mbowe Mungu yuko nawe ingawa wewe sio padri au askofu.
 
Kadri miaka inavyokwenda Mh.Mbowe anabadilika sana...anazidi kukua kisiasa...kwa sasa hata bungeni akiongea ni kama yeye ndo waziri mkuu pale bungeni.....hata mjadala wa katiba alihitimisha yeye bungeni....big up kwa kuwafundisha vijana siasa sio vurugu....politics is the war without blood shed.
 
Back
Top Bottom