Binti Msichana
Senior Member
- Oct 9, 2016
- 109
- 247
Bila ya Busara ya Rais wetu na Bunge kutunga sheria ya bodi ya mikopo kwa makato ya 15% kutoka kwa wanufaika wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu bodi hii ingeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wapya kwani ingefilisika kabisa.
Mkae mkijua ili nchi yeyote iendelee lazima suala la elimu lipewe kipaumbele.
Sheria hii iliyoanza kufanya kazi mwezi wa pili 2017 ina umuhimu mkubwa kwa kuiwezesha Bodi ya Mkopo ya Elimu ya Juu ikusanye marejesho yake kwa wingi.Hali hii itawezesha Bodi hii iwe na pesa za kutosha hivyo kuwa na uwezo mkubwa kukopesha wanafunzi wengine.
Najua wafanyakazi wengi sheria hii ya makato ya asilimia 15 ya mkopo kutoka katika mishahara yao inawaumiza sana, kwani baadhi yao hushindwa kumudu majukumu yao ya kifamilia na pengine baadhi yao kuona kazi chungu kwa makato haya makali , wakati mwingine mfanyakazi kukosa hata nauli ya kwenda kazini au hata akienda kazini hupiga miyao ya njaa kwa kukosa pesa ya chakula.
Lakini ebu kuweni na uzalendo wa nchi yenu, mnataka Bodi ya mikopo ishindwe kujiendesha ? Hamuoni madhara ya wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo ni makubwa kuliko ya mfanyakazi kukuta sh.90000 kwenye akaunti yake baada ya makato ya 15% ? Hivi Taifa litapata wapi wataalamu mbalimbali ?
Unalalamika kwa kukatwa 15% kwa nini usitafute vyanzo vingine vya mapato kama mshahara unauona mdogo ? Kwani maisha yako hayaendi mpaka utegemee mshahara ?
Nakupongeza rais John Pombe Magufuli kwa kusaini sheria hii ya Bodi ya mikopo ya makato ya 15% ya mishahara ya wanufaika wa mikopo, ila umeniudhi kitu kimoja, ungeshinikiza makato walau yawe 30% ya mishahara ya wafanyakazi.Hii ingejenga uwezo zaidi kwa bodi.
Hongera JPM , Hongera Bunge kwa kwa upatikanaji wa sheria hii.