Busara itumike kuiepusha CCM na ukanda uchaguzi 2017

Chama Cha Mapinduzi kimejijenga na kuwa muumini wa umoja na kuepuka kujipambanua kuwa chama cha ukanda, udini na ukabila.

Mara zote imekuwa si desturi ya chama hiki kujadili upatikanaji wa viongozi kwa misingi ya ukanda, ukabila na udini. Lakini tangu kuanzishwa kwake uongozi wake umekuwa wenye sura ya kitaifa zaidi.

Katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kumekuwa na malalamiko mengi kutoka upinzani na wananchi wa kanda ya kaskazini kuwa teuzi nyingi zimekuwa zikiwabeba watu wa kanda ya ziwa zaidi hali ambayo ni hatari kwa umoja wetu kama taifa.

Katika uchaguzi mkuu huu wa mwaka 2017 ndani ya CCM hususani katika jumuiya ya UWT na UVCCM wagombea walio wengi wanatoka kanda ya ziwa mfano nafasi za uenyekiti.

Kwa mfano katika nafasi ya uenyekiti wa UWT karibu wagombea wote wanatoka kanda ya ziwa. UVCCM pia wagombea wanne wanatoka kanda ya ziwa kati ya 7.

Hatari iliyopo ni kupata mwenyekiti wa UWT na UVCCM Taifa kutoka kanda ya ziwa huku mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wa JMT naye anatoka kanda ya ziwa ambao wote kwa pamoja ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM.

Hili likitokea kisiasa si zuri. CCM itatajwa kuwa na siasa za ukanda huku serikali nayo ikituhumiwa kufanya teuzi zake kwa kuipendelea kanda ya ziwa.

Hili likitokea ni hatari sana kwa kanda ya kaskazini, nyanda za juu kusini na Dar es salaam kisiasa. Ni vyema wajumbe wa vikao au mikutano ya uchaguzi kuona umuhimu wa kuchagua viongozi katika jumuiya kwa namna ambayo uwakilishi wenye sura ya kitaifa unapatikana. Narudia tena haitaipa taswira nzuri CCM pale mwenyekiti wa UWT, UVCCM na CCM Taifa watatoka kanda moja.

Tafakari.

KADA08
Fikra Huru.
Unashindwa kuzungumzia chama chenye ukabila na ukanda unazungumzia CCM? Kweli? Hivi mwenyekiti mpya wa BAVICHA ni nani kweli? Sikuweza kufuatilia naombeni mnijuze jamani.
 
Back
Top Bottom