Sikutaka kujadili maada hii,lakini kwa uzito wa swali inanilazimu na mimi niwe sehemu ya mjadala huu.Kikatiba kuna mbunge mama LOLENSIA BUKWIMBA(CCM),alimshinda Ndg.FINIAS MAGESSA (CHADEMA)kwnye chaguzi mbili mfululizo.
Mama huyu hana sifa ya kuwa mwanasiasa hajui kujenga hoja wala kutetea maslahi ya wananchi wake. bahati nzui nimehudhuria mkutano wake na nilicho ambulia ni kuona vikundi vya ngoma. Mama huyu kwenye uchaguzi uliopita aliahidi mambo mengi sana ikiwemo kero sugu ya umeme.
Na ni kweli nguzo za umeme zililetwa na akina ngereja pale katoro(makao makuu ya jimbo-ngome ya chadema) ili kuawapumbaza wananchi,bahati mbaya wananchi bado wanaamini kupewa umeme ni msaada na siyo jukumu la serikali hivyo baada ya uchaguzi CCM ilishinda na huyu mama mkazi wa MIKOCHENI akatangazwa mshindi.
zaidi ya miaka miwili aliyo shika madaraka hakuna hata kimoja anachoweza kujivumia. Mimi ni mmoja wa wakosoaji wake wakuu na siku zote nimekuwa na sisitiza kuwa huyu mama hawezi kuongoza jimbo hili siyo kwasababu ni mwanamke bali hana uweza wa kupambana na changamoto zinazowakabili wanabusanda ambao wengi ni masikini lakini wakiwa wanazungukwa na madini kila upande.
Mama huyu badala ya kufuata ule usemi usemao "IF U CAN'T BEAT THEM,JON THEM, yeye ameamua kujenga fitina na watu wa katoro ambapo ni ngome imara ya CDM ambapo kwenye uchaguzi mkuu uliopita Rais,mbunge na diwani wa CCM hawakushinda hata kituo kimoja( hapa daima CCM imekuwa chama cha upinzani).
Kazi yake imekuwa kukaa MIKOCHENI na akiamua kuja huku jimboni anaenda vijijini ambapo akigwa vijisenti kidogo tu basi,lakini anogopa kwenda katoro kwa watu wenye uelewa mkubwa kwa hofu ya kuulizwa maswali mepesi asiyo weza kuyajibu.
Kudhihirisha udhaifu alionao,hadi mda huu ninapoandika mbunge hana ofisi,jaribu kufikiria ni kwajinsi gani ataweza kuwatumikia wananchi wake kwa ufasaha bila kuwa na ofisi? ni ajabu sana tena..! kingine cha ajabu ni yeye kuona jimbo zima la BUSANDA hakuna mtu wa kumuajiri kuwa katibu wake,yeye akaamua kwenda kwa Diwani wa kata ya kaseme(CCM) mh.masoud kwa katibu wake,hapa napo kuna maswali ya kujiuliza;
kwanza Masoud ni diwani hivyo anahitaji mda wa kuwatumiakia wananchi wake,pia Masoud anakaa kata ya mbali sana kutoka yalipo makao makuu ya Jimbo(Katoro) kwa hoja hizi dhaifu unaona ni kwajinsi gani mbunge huyu asivyo makini na hata mapungu yake yanakosa wakuyaziba.
Maana wabunge wengi wanakaa mijini lakini wanakuwa na makatibu ambao wapo active hata pengo la mbunge halionekani,ukienda ofisini unamkuta katibu unaeleza shida yako, mbunge anapigiwa simu(ndiyo mtindo wa sasa kuongoza jimbo kwa simu---refer J.Makamba) tatizo linatatuliwa siku zinasonga,lakini kwa busanda nikama jimbo lipo wazi:
Nimeamua kusema haya kwa ufupi kwasababu ni mdau mkuwa wa jimbo hili, na siyo kwa sababu nategemea kuomba ridhaa ya kuliongoza jimbo hili hapo 2015 kupitia CDM(Mungu akipenda)
KWA VYOVYOTE ITAKAVYO KUWA 2015 BUKWIMBA ATEGEMEE KUNI-FACE