Bus la 'Princess Muro' lapinduka na kuua usiku huu

HAPO ajali inanukia AU mimi ndio sielewi????
36609_318962354839682_100001777603669_774249_310210015_n.jpg
 
Eee Mungu tunaomba utunusuru! Kama kuna usafiri mbadala, hakuna haja ya kupanda haya magari. Huwa yanakimbia mwendo wa ajabu na wafanyakazi wa hayo magari bangi tupu!. Wakishapata abiria wanajiona ni miungu. Majibu ya ovyo kwa abiria hata wakiwaambia utadhani wanauwezo juu ya roho za watu. Ni shiada tupu.! Wajeuri na wamejaa matusi! Matokeo yake ni kama hivi tunavyoona. Inasikitisha sana.
 
basi hili nimepanda sana inatakiwa upumbav huu uchukuliwe hatua kwani kuna watanzania kadhaa wanacheza kamali kuonyesha basi gn litafika kwanza kati ya basi la muro happy nation na abood na kamali hii ipo sana terminal za makambako,mbeya mjin na tunduma na madereva wanalipwa kutokana na kukimbiza na kuwah kufika na wacheza kamali hao hali mbayaaaaaaaaaaaaaaa
 
Biashara inapotawaliwa na nguvu za giza haya ndo matokeo yake. Mkwema ilikuwa hivi hivi ikamaliza watu na kufunga kazi kwa kuigonga Costa iliyoua watu 25 Arusha miaka ya 2008 na ikawa ndo mwisho wake. Huyu ustaadhi Muro amehama kanda ya kaskazini baada ya nguvu zake za kichawi kuzidiwa nguvu na waombaji akaamua kuhamia kusini. Why Muro everytime; jibu ni kwamba anaoperate katika nguvu zinazomtaka kutoa kafara kulipa fadhila ya mali waliyompa. Subirini ajali nyingine la sivyo yasusieni haya mabasi mtaisha!!!
 
suala la mwendo linahusika sana maanake kama hapo lilipopiga mzinga pan flat 1 nzuri so inawezekana dereva alifungua turbo hadi mwisho and maybe ilitokea tyre burst ndo ikawa end of the story.
anyway hawa jamaa hata mwendo wamebarikiwa,bado Happy nation ya Mbeya maana mwando wake wanajua wenyewe ila siwaombei lakini kama hawatajirekebisha yetu masikio.
 
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa wahanga wote wa ajali hiyo.

Mimi nimekua nasafiri kwa mabasi tofauti tofauti kwenda sehem mbalimbali hapa nchini na wakati mwingine huwa natumia usafiri binafsi pia.

Hali iliyoko humo barabarani kwa kweli ni tofauti sana na jinsi ambavyo inaelezewa katika jamii, kwa kiasi kikubwa cha ajali hizi ni uzembe na hatuna mfumo mzuri wa kiutendaji sahihi ambao unaweza kutupa uthibiti wa vituko vya humo barabarani.

Jeshi la Polisi kwa kweli inabidi tulisaidie kuthibiti hii hali na si kama linavyojisifia kuthibiti na kuwa na mikakati mbalimbali ya kuthibiti. Mfano kwa barabara ya Dar-Mbeya, kumekua na taarifa za kulipongeza jeshi hilo kwa mkoa wa Iringa kwamba wako makini, lakini tunaosafiri hali si kama inavyoelezewa.

Madereva wamekua wakipashana habari na wanafaham maeneo ambayo trafic wanakaa kuangalia mwendo hivyo basi utakuta wakikaribia maeneo hayo wanapashana habari na kupunguza mwendo tena wakati mwingine huwa nashangaa basi linakurupuka dar spidi, mnafika sehem za chakula wanasema dkk 10, alafu mnatoka tena mbio, wakigundua wako mbele ya muda wa ratiba wanaweza simama porini na kuwaambia mkajisaidie au kwa walio wajanja wanasingizia kurekebisha gari kumbe wanapoteza muda. Sielewi kwanini wasitumie muda mwingi kukaa pale hotelini ili watu wapate huduma vizuri na kufurahia safari badala ya kwenda kuwaweka porini??

Kwa kifupi naweza sema uwepo wa kiwango kidogo cha elimu kwa wamiliki na watendaji wa hayo mabasi ianachangia sana na pia suara la ''huduma nzuri kwa wateja'' halipo kabisa hivyo busara ya kutafakari hayo haipo kabisa. Wao kumuhudumia mteja vizuri ni Msaada na sio Haki ya mteja.
Pia ni wazi na ukweli kwamba madereva wengi hapa kwetu hawathamini watumiaji wengine wa barabara, wao sheria ni kwaajili ya kuwaridhisha polisi na sio kuwasaidia wao kuepuka ajari. Tena katika hili utakuta hasa madereva wa magari ya serikari ndio wanaongoza kwa rafu humo barabarani hadi unajiuliza hivyo vyeti vya VETA vimewasaidia nini? Tena wakati mwingine unakuta na Waziri yumo humo ndani. (binafsi nimeshuhudia gari ya Mkulo na yeye akiwemo ndani likini overtake sehem mbaya wakitokea moro kwenda dar, juzi nimekuta gari ya jeshi landrover, imepark kwy kona mbaya kati ya Iringa na Mikumi, isitoshe siku hiyohiyo gari la Jaji lilituovertake sehem mbaya na yeye akiwemo)

Mie ningependekeza yafuatayo kama kweli jeshi la polisi linataka ushirikiano toka kwa abiria kupunguza hizi ajari;
1. Kuwepo na namba za simu za kutoa taarifa kwa Polisi ambazo abiria wanaweza kupiga au kutuma ujumbe mfupi endapo wataona jambo la hatari katika safari ikiwemo magari mabovu, yaliyopark vibaya, mwendo kasi, au tukio lolote baya.
2. Kuwe na database ya kupokea ujumbe huo au simu na kuzisambaza kwa polisi wote walioko katika check points nchini na vituo vyote vya polisi.
3. Wananchi wote turuhusiwe kuona taarifa hizo zinazotumwa ili kuweka uwazi na kufuatilia kwa watendaji ili kuzuia rushwa kwa wahusika wasifunike kombe.
4. Namba za kutuma ujumbe zigawiwe kwa wananchi walioko safarini kupitia check points na kwenye mabasi na daladala ziandikwe kwenye tiketi. Ikiwezekana kuwepo hata na bango njiani yanayoenyosha hizo namba barabarani kama yalivyo mabango ya kuonyesha Majina ya eneo au speed inayotakiwa kutumika ktk eneo fulani.

Naamini kwa mfumo huu tunaweza kupata taarifa mbalimba katika matukio yanayoweza kusababisha ajari, kwani ajari kama za Meli ya Bukoba na huko Zanzibar wananchi wangeweza kutuma ujumbe kabla ya maafa kutokea na hata kwa madereva wanao wadanganya trafiki wanaweza kuumbuliwa na abiria

Nawakilisha, changanya na ya kwako!
 
serikali ingefanya la maana kuyafungia haya mabus,maana kila siku hayaishi kuua,naona mmiliki anabadilisha majina anayaita luck star now,kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom