Burnaboy ni 'lidudu' fulani likubwa

Burnaboy ni 'lidudu' fulani likubwa

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
Kwanza tujue miongoni mwa tuzo kubwa duniani kwenye muziki basi jua BET ipo ndani ya nafasi tatu bora, yaap! Ipo, kwa hiyo ukiona umechaguliwa kushindania kwenye hizo tuzo, ni heshima, haijalishi umeshindwa ama kushinda.

Kwenye masuala ya tuzo, kila mtu anapenda kuwa nominated, huwa ni ndoto ya kila mmoja. Kuna waigizaji wengi wanakwambia kuchaguliwa tu kushindania tuzo za Oscar huwa ni historia kwao, sio kuchukua, kuchaguliwa kuwania tu.

Diamond amepiga hatua kubwa mno kwenye muziki wake, kuwania tuzo hii ni moja ya jambo kubwa sana kwenye muziki wake, ni kitu ambacho atakwenda kukiandika kwenye kidaftari chake cha rekodi na kuwaonyesha wajukuu kwamba alikwishawahi kuwa nominated huko.

Kuchaguliwa kwa Diamond kulileta vita mitandaoni, maneno ya huku na kule, wengine walisema atolewe kwa kuwa tu alikuwa akiunga mkono juhudi na wengine walisema habakishwe kwani muziki na siasa kwao vilikuwa vitu tofauti.

Sizungimzii sana huko ila ninachotaka kusema ni kuwakumbusha hili jambo kubwa alilopiga mwana, ameshindwa, sawa, na pia tukumbuke hii tuzo imekwenda kwa mtu sahihi, ndiyo! Mtu sahihi.

Hakuna mwanamuziki kwa sasa duniani anayependa kukutana na Burnaboy kwenye kipengele chochote cha kuwania tuzo na huyu jamaa, ni hatari mno, kushindana na Diamond, Wizkid na wengine, ilionyesha kabisa jamaa anakwenda kuchukua tuzo hiyo.

Burnaboy ni sawa na lidudu fulani hivi likubwa, mpaka kulipiga na kuliagusha, nawe unatakiwa utoke damu kwanza, si kirahisi kabisa.

Nakumbuka kuna kipindi Diamond alikuwa levo ya juu kabisa, miaka michache tu iliyopita tulikuwa tunamuweka Wizkid, Davido na chini tunamuweka Diamond, alikuwa wa moto sana, bahati mbaya akapotea kimataifa.

Kilichomwangusha, hakuwa akitoa hit za Afrika tena, akawa anatoa hit za Tanzania. Akatoa ngoma nyingi mfululizo za kumfanya awe juu Tanzania lakini akasahau Afrika na huko duniani mpaka baadaye alipoamua kurudi na Jeje.

Nina uhakika 100% kwamba endapo Diamond angebaki kulekule alipokuwa kipindi kile, angekuwa bize na ngoma za kimataifa, leo Mond angeonekana mtu mwingine kabisa.

Kipindi kile mpaka Wanigeria walianza kumuogopa, wakajua sasa kuna mtu kutoka Tanzania ni hatari sana, hakamatiki, badala ya kuendelea kukaza, akalegeza kamba, anakuja kushukia, Wizkid, Davido wapo mbali kabisa, mile hata elfu moja kutoka alipo.

Ushauri wangu Mond arudi kufanya kazi za kimataifa, asifanye hizi za Kitanzania, sisi kama Watanzania tushamkubali, anajua, ni hatari, mwamba, hana mpinzani, sasa anatakiwa kugeukia huko kimataifa, na si kufanya kolabo na wasanii wachanga Nigeria kisa tu ni Mnigeria, wengine apotezee tu.

Achukue mfano hata wa Burnaboy, si mtu wa kolabo na ma-underground wa Nigeria, anapiga kolabo kubwa na za kimataifa. Hapa simaanishi asipige kolabo na wasanii wa Tanzania, nope! Namaanisha akienda kufanya kazi kimataifa, aangalie na wasanii wa kufanya nao kolabo, wengine amewazidi mbali sana, hanufaiki na kolabo hizo hata kidogo.

Kabla ya kumcheka Diamond, hebu tujiulize, mbali na yeye, je, tuna msanii mwingine ambaye ataweza kutufikisha huko? Kama hayupo, je, kuna dalili za msanii mwingine kutufikisha huko ndani ya miaka kumi?

Kwa upande wangu, jamaa amepambana sana, anachotakiwa kwa sasa ni kutafuta connection kubwa zaidi za nje kama wenzake, afanye kazi mbalimbali na magiant wa muziki duniani atangazike vizuri, sio achagulie kwenye tuzo fulani halafu atokee Mmarekani fulani aulize Who is Diamond? Yaani tunataka kila mtu amjue kwa kuwa alimuona kwenye ngoma kadhaa na Drake, Jay Z, Beyonce, Breezy na wengine.

Jicho lake pana kwa sasa aliweke kimataifa, hapa Tanzania kushamtosha, asipakomalie sana, ningependa kumuona akiwa nominated kwenye tuzo kubwa duniani ya muziki ya Grammy. Uwezo anao, na ninadhani nia anayo, basi afuate haya machache niliyoshauri.

Halafu hivi Rayvanny alichukuaje tuzo ya BET? Inafikirisha kishenzi!
20210628_112203.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Dimond kuwa nominated tu pia ni sehemu ya ushindi,hulka ya Mondi sio ya kukata tamaa najua ipo siku.
Hongera ziende kwake Burna boy,Dimond na washiriki wengine.
 
Rayvanny alichukua BET Viewers choice award.

Tuzo ya watoto ambayo mara nyingi wanaangalia kura zinazotokana na hashtags za social networks.
 
Diamond sasa arudi Tz kuja kuwaomba radhi watanzania kwa jinsi alivyowagawa kisiasa. Siasa ndio kitanzi cha kumnyongea Diamond. Bahati mbaya, kitanzi hicho amekitengeneza yeye mwenyewe Diamond.
 
Back
Top Bottom