Buriani: Watanzania Wengi Hawakumjua Rais Mkapa. Nami Nishuhudie

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,529
41,046
Mwaka 2002, nilikuwa jijini Santiago kikazi. Nilijumuika na watu wengi toka pande mbalimbali za Dunia. Mmoja wa niliyejumuika naye alikuwa ni ofisa mmoja wa kutoka Indonesia. Wakati huo Indonesia ilikuwa haijapita muda mrefu tangu wamchague Waziri Mkuu.

Wakati huo, kwenye hoteli ile kulikuwa na King Hassan wa Jordan, na George Bush aliondoka siku mimi nilipoingia. Ni hoteli ambayo wakubwa wa Dunia walipenda kufikia, na gharama yake haikuwa haba.

Wakati fulani wa maongezi, nikiwa nimesimama na yule ofisa wa Indonesia, afisa wa juu wa Serikali ya Canada, akamwambia yule afisa wa kutoka Indonesia, 'this time you have a got a very good Prime Minister', yule Muindonesia akasema, 'you are right'. Kisha yule afisa wa juu wa Canada, akasema, 'but I assure you, he is not as good as this genteman's President, President Benjamin William Mkapa.

Last week Benjamin Mkapa was in Toronto, he addresed like the President of Africa. He spoke on behalf of Africa. We were expecting such a speech from Thabo Mbeki, but it was Benjamin Mkapa who made it. He is an exceptional leader. He has made what even the First World Presidents cannot. Can you imagine, lowering inflation from 30% down to 4%, that had never happened anywhere but Benjamin has done it. Unfortunately, I do not think the Africans understand the greatness of Benjamin. Had it been in any American or European countries - he would be in success records'.

Nilimjua Mkapa kwa mbali sana. Niliijua kazi aliyoifanya Mkapa, hasa kwenye uchumi wa nchi yetu lakini sikufikiria kuwa alichokifanya kilikuwa ni cha pekee sana Duniani.

Ni Mkapa ndiye aliyesimamia sera ya uwekezaji. Kuna watu wajati wa uhai wake wamekuwa kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya madini, na kuashiria kuwa aliuza rasilimali za Taifa kwa mabeberu. Lakini kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, na kwa kumheshimu Mungu aliyeniumba, nina hakika Rais Mkapa alikuwa mzalendo wa kweli wa nchi yetu. Uwekezaji kwenye sekta ya madini, haukuwa na rushwa yoyote wala dhamira yoyote ya kuangamiza Taifa.

Naikumbuka hotuba aliyoitoa Mkapa pale Bulyanhulu, mbele ya Watanzania na Balozi wa Kudumu wa Marekani, Andrewa Young, 'to make an investor come to Tanzania, not to South America, Asia or even Kenya, where there is electricty, good roads, assured communication facilities, instead come to Tanzania where all the necessary enabling infrastructure is missing, there is a price to pay, and my government has accepted it".

Mkapa wakati huo alikuwa akigangaika kupata hrla ya kuendeshea Serikali. Wakati Mkapa anaingia madarakani, hata mishahara ya wafanyakazi wa umma ilikuwa inakosekana. Mwezi wa 7, mfanyakazi analipwa mshahara wa mwezi wa 5 au 6. Mkapa aliondoka madarakani wafanyakazi wote wa umma wakilipwa kwa wakati.

Ukitaka kumjua kiongozi mzuri, uone atafanya nini wakati nchi ikiwa katika matatizo. Mkapa aliweza kuonesha uwezo wake wa kuitoa nchi kwenye dimbwi la dhiki kubwa. Mkapa hakuwahi kuhangaikia sifa bali alihangaikia mafanikio ya nchi.

Ni bahati mbaya sana watanzania huwa tunavutika na kushawishika kwa vitu vidogo vidogo, huku makubwa tukiyapa umuhimu mdogo.

Sina nia ya kumlaumu mtu lakini kama kuna kitu ambacho mpaka leo huwa najiuliza, sipati jibu, ni mtazamo wa Serikali ya awamu ya 5 kuamini kuwa hakuna makubwa yaliyowahi kufanyika awamu zilizopita. Wanataka kuwaaminisha watu kuwa mambo makubwa, mazuri na ya ajabu yamefanyika awamu hii. Lakini kwa hakika misingi muhimu ya uchumi wa kisasa kwa Tanzania, iliwekwa na Mkapa.

Mkapa aliuchukua uongozi wa nchi, hazina ikiwa ina zero balance. Akaondoka akiwa ameacha $5 billion. Ni Mkapa ndiye aliyejenga taasisi imara za utawala, uongozi na za kusimamia uchumi. Ni Mkapa ndiye aliyeifanya sekta binafsi kuwa mhimili wa uchumi. Ni Mkapa aliyeingia madarakani $1 = TZS 800; akaishusha mpaka $1 = 500. Mwinyi aliipandisha $1 = TZS 5 mpaka $1=TZS 800.

Hakuna mtawala mwingine yeyote aliyeweza kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine kubwa za Dunia kama alivyofanya Mkapa.

Niliwahi kukutana na kiongozi mmoja aliyehudumu kipindi cha Mkapa, Kikwete na Magufuli - alisema, 'katika awamu zote, ni kipindi cha Makapa pekee, ukitaka kufanya maamuzi unaangalia sheria, kanuni na miongozo. Huna haja ya kumwuliza mkubwa wako. Leo ukijifanya kuangalia sherua na kanuni bila kujitahidi mkubwa anataka nini, umeebda na maji".

Yale maelezo ya Mkanada na huyu afisa kiongozi wa Serikali, yanadhihirisha kuwa Mkapa alikuwa Kiongozi. Kiongozi hutengeneza mifumo. Mifumo huwatengeneza viongozi wengi na kuwapa moyo wa kujiamini katika kutenda kazi zao.

Watawala badala ya kujenga mifumo, huyajenga majina yao. Hawapendi kujenga mifumo kwa sababu mifumo hutoa nafasi ya watu wengine kuonesha umahiri wao. Watawala hupenda wasifiwe wao tu. Hawataki kujenga mifumo ambayo huwajenga watu wengi, na kuyainua majina yao.

Mpendwa ndugu yetu Rais Mstaafu Mkapa, umeimaliza safari yako. Umeziacha nyayo zako Duniani. Wapo watakaopenda kuzifuta lakini hawataweza kwa sababu nyayo zako zimechapwa kwenye miamba kwa kutumia wino usiofutika.

Mazuri ya Mkapa, ni zawadi ya Mungu kwetu tunaoebdelea kuishi.

Kwa watawala waliopo sasa na wajao, wasiyanene mazuri ya Mkapa kama hadithi bali waweke dhamira ya kuyaiga na kuyaishi. Watakapoyaishi watakuwa wanamuenzi Mungu ambaye hugawa karama fulani kwa kila mwanadamu ili zikijumuika pamoja zimtunze, zimjenge na zimlinde mwanadamu.
 
Unaweza weka summary ya hiki ulichokiandika mkuu, ndefu sana aisee
 
Mkuu, nimekuelewa vyema!! Ingawa ndani ya Andiko lako kuna upenyo wa maswali ama la, niamue kuwadharau waliowahi kumpondea Mzee Mkapa

Kuna ka kikundi kazi Yao ni kuwatafutia watu ubaya ili wawe wabaya machoni pa wengi, hii ndiyo dhambi mbaya kabisa, na kakikundi hako kapo Hadi Leo na hata sasa kangali kakifanya kazi hiyo ya Kishetani na wakishirikiana vema na Lusifa

Kwa bandiko hili kama ni kuomba Moto ushuke juu ya shetwani basi ni pamoja na maagenti hao,

RIP Mzee Mkapa, hakika umefanya mengi Kwa Taifa letu
 
Mwaka 2002, nilikuwa jijini Santiago kikazi. Nilijumuika na watu wengi toka pande mbalimbali za Dunia. Mmoja wa niliyejumuika naye alikuwa ni ofisa mmoja wa kutoka Indonesia. Wakati huo Indonesia ilikuwa haijapita muda mrefu tangu wamchague Waziri Mkuu.

Wakati huo, kwenye hoteli ile kulikuwa na King Hassan wa Jordan, na George Bush aliondoka siku mimi nilipoingia. Ni hoteli ambayo wakubwa wa Dunia walipenda kufikia, na gharama yake haikuwa haba.

Wakati fulani wa maongezi, nikiwa nimesimama na yule ofisa wa Indonesia, afisa wa juu wa Serikali ya Canada, akamwambia yule afisa wa kutoka Indonesia, 'this time you have a got a very good Prime Minister', yule Muindonesia akasema, 'you are right'. Kisha yule afisa wa juu wa Canada, akasema, 'but I assure you, he is not as good as this genteman's President, President Benjamin William Mkapa. Last week Benjamin Mkapa was in Toronto, he addresed like the President of Africa. He spoke on behalf of Africa. We were expecting such a speech from Thabo Mbeki, but it was Benjamin Mkapa who made it. He is an exceptional leader. He has made what even the First World Presidents cannot. Can you imagine, lowering inflation from 30% down to 4%, that had never happened anywhere but Benjamin has done it. Unfortunately, I do not think the Africans understand the greatness of Benjamin. Had it been in any American or European countries - he would be in success records'.

Nilimjua Mkapa kwa mbali sana. Niliijua kazi aliyoifanya Mkapa, hasa kwenye uchumi wa nchi yetu lakini sikufikiria kuwa alichokifanya kilikuwa ni cha pekee sana Duniani.

Ni Mkapa ndiye aliyesimamia sera ya uwekezaji. Kuna watu wajati wa uhai wake wamekuwa kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya madini, na kuashiria kuwa aliuza rasilimali za Taifa kwa mabeberu. Lakini kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, na kwa kumheshimu Mungu aliyeniumba, nina hakika Rais Mkapa alikuwa mzalendo wa kweli wa nchi yetu. Uwekezaji kwenye sekta ya madini, haukuwa na rushwa yoyote wala dhamira yoyote ya kuangamiza Taifa.

Naikumbuka hotuba aliyoitoa Mkapa pale Bulyanhulu, mbele ya Watanzania na Balozi wa Kudumu wa Marekani, Andrewa Young, 'to make an investor come to Tanzania, not to South America, Asia or even Kenya, where there is electricty, good roads, assured communication facilities, instead come to Tanzania where all the necessary enabling infrastructure is missing, there is a price to pay, and my government has accepted it".

Mkapa wakati huo alikuwa akigangaika kupata hrla ya kuendeshea Serikali. Wakati Mkapa anaingia madarakani, hata mishahara ya wafanyakazi wa umma ilikuwa inakosekana. Mwezi wa 7, mfanyakazi analipwa mshahara wa mwezi wa 5 au 6. Mkapa aliondoka madarakani wafanyakazi wote wa umma wakilipwa kwa wakati.

Ukitaka kumjua kiongozi mzuri, uone atafanya nini wakati nchi ikiwa katika matatizo. Mkapa aliweza kuonesha uwezo wake wa kuitoa nchi kwenye dimbwi la dhiki kubwa. Mkapa hakuwahi kuhangaikia sifa bali alihangaikia mafanikio ya nchi.

Ni bahati mbaya sana watanzania huwa tunavutika na kushawishika kwa vitu vidogo vidogo, huku makubwa tukiyapa umuhimu mdogo.

Sina nia ya kumlaumu mtu lakini kama kuna kitu ambacho mpaka leo huwa najiuliza, sipati jibu, ni mtazamo wa Serikali ya awamu ya 5 kuamini kuwa hakuna makubwa yaliyowahi kufanyika awamu zilizopita. Wanataka kuwaaminisha watu kuwa mambo makubwa, mazuri na ya ajabu yamefanyika awamu hii. Lakini kwa hakika misingi muhimu ya uchumi wa kisasa kwa Tanzania, iliwekwa na Mkapa.

Mkapa aliuchukua uongozi wa nchi, hazina ikiwa ina zero balance. Akaondoka akiwa ameacha $5 billion. Ni Mkapa ndiye aliyejenga taasisi imara za utawala, uongozi na za kusimamia uchumi. Ni Mkapa ndiye aliyeifanya sekta binafsi kuwa mhimili wa uchumi. Ni Mkapa aliyeingia madarakani $1 = TZS 800; akaishusha mpaka $1 = 500. Mwinyi aliipandisha $1 = TZS 5 mpaka $1=TZS 800.

Hakuna mtawala mwingine yeyote aliyeweza kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine kubwa za Dunia kama alivyofanya Mkapa.

Niliwahi kukutana na kiongozi mmoja aliyehudumu kipindi cha Mkapa, Kikwete na Magufuli - alisema, 'katika awamu zote, ni kipindi cha Makapa pekee, ukitaka kufanya maamuzi unaangalia sheria, kanuni na miongozo. Huna haja ya kumwuliza mkubwa wako. Leo ukijifanya kuangalia sherua na kanuni bila kujitahidi mkubwa anataka nini, umeebda na maji".

Yale maelezo ya Mkanada na huyu afisa kiongozi wa Serikali, yanadhihirisha kuwa Mkapa alikuwa Kiongozi. Kiongozi hutengeneza mifumo. Mifumo huwatengeneza viongozi wengi na kuwapa moyo wa kujiamini katika kutenda kazi zao.

Watawala badala ya kujenga mifumo, huyajenga majina yao. Hawapendi kujenga mifumo kwa sababu mifumo hutoa nafasi ya watu wengine kuonesha umahiri wao. Watawala hupenda wasifiwe wao tu. Hawataki kujenga mifumo ambayo huwajenga watu wengi, na kuyainua majina yao.

Mpendwa ndugu yetu Rais Mstaafu Mkapa, umeimaliza safari yako. Umeziacha nyayo zako Duniani. Wapo watakaopenda kuzifuta lakini hawataweza kwa sababu nyayo zako zimechapwa kwenye miamba kwa kutumia wino usiofutika.

Mazuri ya Mkapa, ni zawadi ya Mungu kwetu tunaoebdelea kuishi.

Kwa watawala waliopo sasa na wajao, wasiyanene mazuri ya Mkapa kama hadithi bali waweke dhamira ya kuyaiga na kuyaishi. Watakapoyaishi watakuwa wanamuenzi Mungu ambaye hugawa karama fulani kwa kila mwanadamu ili zikijumuika pamoja zimtunze, zimjenge na zimlinde mwanadamu.
Mtaongea sana yaani mwaka huu

Alipokua mzima mlifunga madomo yenu,sasa hivi funueni sana!
 
Hivi unajua kuwa hakuna wa kwanza kama hakuna wa mwisho? Tunasema Mkapa alivutia sana uwekezaji mkubwa kwa sababu waliofuatia wote, hakuna aliyefikia kiwango chake. Tunasema Mkapa alikuwa ni kiongozi kwa sababu alipenda nchi iongozwe kwa kufuata sheria na katiba, tofauti na sasa ambapo nchi inaongozwa zaidi kwa matamko ya watawala. Kama kila awamu ingeongoza kwa kufuata sheria na katiba, upekee wa Mkapa usingeonekana.

Hakuna mwanademokrasia kama hakuna dikteta wa kumlinganisha naye, labda uwe na absolute indicators.

Mazuri yake yote yanasemwa sasa kwa sababu amefunga kitabu chake. Hii ni tafakari ya maisha yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipokua hai hukuleta makala hapa kuyasema yote haya....

Swali,kwanini unafiki wote huu ?
 
Bams,

..wasaidizi wa Mkapa ktk kufufua na kuusuka upya uchumi wa Tz ni kama Prof.Simon Mbilinyi, Daniel Yona, Basil Pesambili Mramba, na Dr.Abdalah Omari Kigoda[r.i.p]. Unadhani mchango upo uwezekano wa mchango wao kutatambuliwa? Kwasababu Mkapa alikuwa Raisi, lakini hao ndio walikuwa mawaziri wa fedha, uchumi, au mipango.
 
Kama kuna Raisi bora kuwahi kutokea Afrika, Ben ni kinara!
Alikuwa na madini ya maana kichwani, kiongozi wa kipekee sana!
Bado naukumbuka mdahalo wa wagombea uraisi mwaka 1995, mdahalo ule ulitufanya tumjue Mkapa, aliwa outshine wagombea wenzake hadi ambao ni Maprofesa
 
Bams,

..wasaidizi wa Mkapa ktk kufufua na kuusuka upya uchumi wa Tz ni kama Prof.Simon Mbilinyi, Daniel Yona, Basil Pesambili Mramba, na Dr.Abdalah Omari Kigoda[r.i.p]. Unadhani mchango upo uwezekano wa mchango wao kutatambuliwa? Kwasababu Mkapa alikuwa Raisi, lakini hao ndio walikuwa mawaziri wa fedha, uchumi, au mipango.

Kama umemuelewa mtoa mada vizuri amesema wazi alijenga mifumo imara iliyowapa fursa wenye uwezo kuonyesha uwezo wao! Watendaji waliweza kutekeleza wajib wao kwa kuangalia sheria inasema nini badala ya boss kasema nini!
Sio kwamba Mchango wa hao uliowataja umepuuzwa lakini anasifiwa aliyewawezesha hao ndugu kuutoa Mchango wao kwa uhuru na weledi
 
Kuwaridhisha binadamu ni kazi kubwa na ngumu sana.
Wenye kumbukumbu bado hatujasahau kauli kama "Ukapa", "Mmakonde huyu kabania fedha" na baadhi ya hao watu leo wamegeuka wanamsifia jamaa alikuwa kiongozi bora.

Nilichojifunza kila kiongozi ana mambo yake mazuri sana na mabaya pia, tusiaminishwe ubaya au uzuri tu wa kiongozi yeyote.
Kitu kingine nimejifunza walalamikaji au wasifiaji wa kiongozi flani ni watu waliokosa fursa au waliopata fursa kupitia kiongozi husika.
Yaani wakosoaji wameachwa nje ya meza ya kulia keki ya taifa, na wasifiaji ni wale walioshiriki meza ya ulaji wa keki ya taifa kipindi cha huyo kiongozi.

Hawa wachache ambao kati yao ni wanasiasa au/na wafanyabiashara ndiyo wanaojaribu kushawishi umati mkubwa wa wananchi kwamba kiongozi husika ni mbaya au mzuri. Wanalazimisha wote tuafikiane na hisia zao.
 
Kama umemuelewa mtoa mada vizuri amesema wazi alijenga mifumo imara iliyowapa fursa wenye uwezo kuonyesha uwezo wao! Watendaji waliweza kutekeleza wajib wao kwa kuangalia sheria inasema nini badala ya boss kasema nini!
Sio kwamba Mchango wa hao uliowataja umepuuzwa lakini anasifiwa aliyewawezesha hao ndugu kuutoa Mchango wao kwa uhuru na weledi

..kama ni hivyo hata Mkapa hastahili kutajwa, wanaotakiwa kutajwa ni Watanzania ambao walimchagua, walimuwezesha, na kumpa fursa Mkapa.

..hoja yangu ni kwamba tujenge utamaduni wa kutambua michango ya Watanzania wengi zaidi na siyo kuelekeza sifa zooote kwa Wakuu wa Nchi.
 
Bams,

..wasaidizi wa Mkapa ktk kufufua na kuusuka upya uchumi wa Tz ni kama Prof.Simon Mbilinyi, Daniel Yona, Basil Pesambili Mramba, na Dr.Abdalah Omari Kigoda[r.i.p]. Unadhani mchango upo uwezekano wa mchango wao kutatambuliwa? Kwasababu Mkapa alikuwa Raisi, lakini hao ndio walikuwa mawaziri wa fedha, uchumi, au mipango.
Umemsahau Dr Balali
 
Back
Top Bottom