Buriani: Watanzania Wengi Hawakumjua Rais Mkapa. Nami Nishuhudie

Mwaka 2002, nilikuwa jijini Santiago kikazi. Nilijumuika na watu wengi toka pande mbalimbali za Dunia. Mmoja wa niliyejumuika naye alikuwa ni ofisa mmoja wa kutoka Indonesia. Wakati huo Indonesia ilikuwa haijapita muda mrefu tangu wamchague Waziri Mkuu.

Wakati huo, kwenye hoteli ile kulikuwa na King Hassan wa Jordan, na George Bush aliondoka siku mimi nilipoingia. Ni hoteli ambayo wakubwa wa Dunia walipenda kufikia, na gharama yake haikuwa haba.

Wakati fulani wa maongezi, nikiwa nimesimama na yule ofisa wa Indonesia, afisa wa juu wa Serikali ya Canada, akamwambia yule afisa wa kutoka Indonesia, 'this time you have a got a very good Prime Minister', yule Muindonesia akasema, 'you are right'. Kisha yule afisa wa juu wa Canada, akasema, 'but I assure you, he is not as good as this genteman's President, President Benjamin William Mkapa.

Last week Benjamin Mkapa was in Toronto, he addresed like the President of Africa. He spoke on behalf of Africa. We were expecting such a speech from Thabo Mbeki, but it was Benjamin Mkapa who made it. He is an exceptional leader. He has made what even the First World Presidents cannot. Can you imagine, lowering inflation from 30% down to 4%, that had never happened anywhere but Benjamin has done it. Unfortunately, I do not think the Africans understand the greatness of Benjamin. Had it been in any American or European countries - he would be in success records'.

Nilimjua Mkapa kwa mbali sana. Niliijua kazi aliyoifanya Mkapa, hasa kwenye uchumi wa nchi yetu lakini sikufikiria kuwa alichokifanya kilikuwa ni cha pekee sana Duniani.

Ni Mkapa ndiye aliyesimamia sera ya uwekezaji. Kuna watu wajati wa uhai wake wamekuwa kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya madini, na kuashiria kuwa aliuza rasilimali za Taifa kwa mabeberu. Lakini kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, na kwa kumheshimu Mungu aliyeniumba, nina hakika Rais Mkapa alikuwa mzalendo wa kweli wa nchi yetu. Uwekezaji kwenye sekta ya madini, haukuwa na rushwa yoyote wala dhamira yoyote ya kuangamiza Taifa.

Naikumbuka hotuba aliyoitoa Mkapa pale Bulyanhulu, mbele ya Watanzania na Balozi wa Kudumu wa Marekani, Andrewa Young, 'to make an investor come to Tanzania, not to South America, Asia or even Kenya, where there is electricty, good roads, assured communication facilities, instead come to Tanzania where all the necessary enabling infrastructure is missing, there is a price to pay, and my government has accepted it".

Mkapa wakati huo alikuwa akigangaika kupata hrla ya kuendeshea Serikali. Wakati Mkapa anaingia madarakani, hata mishahara ya wafanyakazi wa umma ilikuwa inakosekana. Mwezi wa 7, mfanyakazi analipwa mshahara wa mwezi wa 5 au 6. Mkapa aliondoka madarakani wafanyakazi wote wa umma wakilipwa kwa wakati.

Ukitaka kumjua kiongozi mzuri, uone atafanya nini wakati nchi ikiwa katika matatizo. Mkapa aliweza kuonesha uwezo wake wa kuitoa nchi kwenye dimbwi la dhiki kubwa. Mkapa hakuwahi kuhangaikia sifa bali alihangaikia mafanikio ya nchi.

Ni bahati mbaya sana watanzania huwa tunavutika na kushawishika kwa vitu vidogo vidogo, huku makubwa tukiyapa umuhimu mdogo.

Sina nia ya kumlaumu mtu lakini kama kuna kitu ambacho mpaka leo huwa najiuliza, sipati jibu, ni mtazamo wa Serikali ya awamu ya 5 kuamini kuwa hakuna makubwa yaliyowahi kufanyika awamu zilizopita. Wanataka kuwaaminisha watu kuwa mambo makubwa, mazuri na ya ajabu yamefanyika awamu hii. Lakini kwa hakika misingi muhimu ya uchumi wa kisasa kwa Tanzania, iliwekwa na Mkapa.

Mkapa aliuchukua uongozi wa nchi, hazina ikiwa ina zero balance. Akaondoka akiwa ameacha $5 billion. Ni Mkapa ndiye aliyejenga taasisi imara za utawala, uongozi na za kusimamia uchumi. Ni Mkapa ndiye aliyeifanya sekta binafsi kuwa mhimili wa uchumi. Ni Mkapa aliyeingia madarakani $1 = TZS 800; akaishusha mpaka $1 = 500. Mwinyi aliipandisha $1 = TZS 5 mpaka $1=TZS 800.

Hakuna mtawala mwingine yeyote aliyeweza kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine kubwa za Dunia kama alivyofanya Mkapa.

Niliwahi kukutana na kiongozi mmoja aliyehudumu kipindi cha Mkapa, Kikwete na Magufuli - alisema, 'katika awamu zote, ni kipindi cha Makapa pekee, ukitaka kufanya maamuzi unaangalia sheria, kanuni na miongozo. Huna haja ya kumwuliza mkubwa wako. Leo ukijifanya kuangalia sherua na kanuni bila kujitahidi mkubwa anataka nini, umeebda na maji".

Yale maelezo ya Mkanada na huyu afisa kiongozi wa Serikali, yanadhihirisha kuwa Mkapa alikuwa Kiongozi. Kiongozi hutengeneza mifumo. Mifumo huwatengeneza viongozi wengi na kuwapa moyo wa kujiamini katika kutenda kazi zao.

Watawala badala ya kujenga mifumo, huyajenga majina yao. Hawapendi kujenga mifumo kwa sababu mifumo hutoa nafasi ya watu wengine kuonesha umahiri wao. Watawala hupenda wasifiwe wao tu. Hawataki kujenga mifumo ambayo huwajenga watu wengi, na kuyainua majina yao.

Mpendwa ndugu yetu Rais Mstaafu Mkapa, umeimaliza safari yako. Umeziacha nyayo zako Duniani. Wapo watakaopenda kuzifuta lakini hawataweza kwa sababu nyayo zako zimechapwa kwenye miamba kwa kutumia wino usiofutika.

Mazuri ya Mkapa, ni zawadi ya Mungu kwetu tunaoebdelea kuishi.

Kwa watawala waliopo sasa na wajao, wasiyanene mazuri ya Mkapa kama hadithi bali waweke dhamira ya kuyaiga na kuyaishi. Watakapoyaishi watakuwa wanamuenzi Mungu ambaye hugawa karama fulani kwa kila mwanadamu ili zikijumuika pamoja zimtunze, zimjenge na zimlinde mwanadamu.
Salute sanaaa Mkuu..
Makala nzuri sana.
 
Kuwaridhisha binadamu ni kazi kubwa na ngumu sana.
Wenye kumbukumbu bado hatujasahau kauli kama "Ukapa", "Mmakonde huyu kabania fedha" na baadhi ya hao watu leo wamegeuka wanamsifia jamaa alikuwa kiongozi bora.

Nilichojifunza kila kiongozi ana mambo yake mazuri sana na mabaya pia, tusiaminishwe ubaya au uzuri tu wa kiongozi yeyote.
Kitu kingine nimejifunza walalamikaji au wasifiaji wa kiongozi flani ni watu waliokosa fursa au waliopata fursa kupitia kiongozi husika.
Yaani wakosoaji wameachwa nje ya meza ya kulia keki ya taifa, na wasifiaji ni wale walioshiriki meza ya ulaji wa keki ya taifa kipindi cha huyo kiongozi.

Hawa wachache ambao kati yao ni wanasiasa au/na wafanyabiashara ndiyo wanaojaribu kushawishi umati mkubwa wa wananchi kwamba kiongozi husika ni mbaya au mzuri. Wanalazimisha wote tuafikiane na hisia zao.

Hadi mdahalo ambao alishindwa vibaya leo inasemekana eti alishinda..

Achilia mbali kashfa zote za sumaye hadi kuitwa zero ..Rais akiwa Mkapa..
 
Ila ingekuwa udaku Wa akina Wema ungeusoma wote.. Hiki kizazi hovyo sana, kama unaona ugumu kusoma hii page, Utakuwa na moyo Wa kusoma vitabu mbalimbali vikuongee maarifa?
Humu jamvini kuna matakataka mengi sana mkuu
 
Msiba wa Mkapa umeonyesha ni kwa kiasi gani Serikali ya awamu ya 5 hata ikiendelea kuwepo madarakani kwa miaka 20 haitofikia hata Robo ya mafanikio ya awamu ya 3
Ngumu kumesa hii ndg yangu watakuja wanachana wa praise and worship watakuponda
 
You have spoken....
alafu Mkapa tulimchukulia poa sana mapaka amefariki ndio tumeona umahiri wake....
nilifanya makosa sana kutokwenda kumsalimia wakati wa uhai wake na kumpongeza....
nitajitahidi nisirudie makosa nikamsalimie mzee Mwinyi na Jakaya......
Mungu akinijaalia.
 
Mkuu usitie chumvi nyingi unaposema Mwinyi alikuta $=sh 5 za Tanzania your report is null and void.
Nazungumza kitu ambacho nina uhakika nacho kwa 100%. Huenda ulikuwa mdogo. Wakati ule dola 1 ilikuwa sh 5. Kwa hiyo ukipanda basi la mzunguko mjini Dar unalipa sh 5. Yale basi ya Ikarusi ya kutoka Romania. Waswahili hiyo sh 5 waliita dala. Ndiyo chanzo cha kuyaita mabasi ya mzunguko mjini daladala (yaani doladola) kwa sababu kila mahali ulilipa sh 5, sawa na dollar 1.

Na noti ya sh 20 iliitwa paundi kwa sababu paundi 1 ilikuwa sawa na sh 20. Wakati ule viwango vya ubadilishaji fedha vilikuwa vinapangwa na Serikali.

Mwinyi aliporidhia masharti ya IMF ya kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania, dola 1 kwanza ilikuwa sh 20, kisha ikaruka ikawa sawa na sh 60, halafu ilienda mpaka sh 90, kisha sh 190, ikapaa mpaka dollar 1 ikawa sawa na sh 390. Baada ya hapo iliendelea kushuka mpaka kufikia dola 1 sawa na sh 800. Wakati huo inflation ilikuwa imefikia 30%.

Sina sababu ya kuweka chumvi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachukia sana maandiko kama haya, angeliona hili bandiko akiwa hai angejisikiaje? Au mnahisi huko aendako kuna jamii forum?!
 
Mkuu acha kujifanya matanga, kuomba summary ni kosa? Au una maana gani? Wengine ni executives so usomaji wetu ni tofauti na wako. Pathetic
Soma habari uliyowekewa wewe wacha uvivu, summary upewe Kuna mtu unamlipa? No wonder watz wengi maskini uvivu tu hata kwa vitu vidogo. Yaani utafikiri upo biiize kumbe uvivu tu kupenda kutafuniwa. Eti executive, shwain
 
Mkuu mimi nasoma vitabu vingi sana, pia naweza soma makala ndefu pia, lakini uhandishi lazima uanze kwa kunivutia, lakini kama ndiyo kama huu lazima nipate uvivu kwani napoteza interest from the beginning.
Mkuu, huyu bwana kaandika vizuri sana. Kitu kimoja tu alichokosea ni kwenye exchange rate aliyoikuta Mkapa na aliyoikuta Mwinyi.
 
Nisahihi alijitahidi Kuwa kiongozi bora... lkn pia elezea pande zote, Eleza kuhusu meremeta, kagoda, epa, ununuzi wa rada na ndege ya rais etc. nivizuri watu wakajua na mapungufu ili wajifunze.
 
Mkuu mimi nasoma vitabu vingi sana, pia naweza soma makala ndefu pia, lakini uhandishi lazima uanze kwa kunivutia, lakini kama ndiyo kama huu lazima nipate uvivu kwani napoteza interest from the beginning.
Acha kujitetea, anayependa kusoma atasoma chochote ata kama ni kipande cha gazeti kwa ajili ya kuchambia.. atalisoma kwanza kisha alitumie
 
Soma habari uliyowekewa wewe wacha uvivu, summary upewe Kuna mtu unamlipa? No wonder watz wengi maskini uvivu tu hata kwa vitu vidogo. Yaani utafikiri upo biiize kumbe uvivu tu kupenda kutafuniwa. Eti executive, shwain
Sawa mkuu, naheshimu maoni yako, lakini habari ndefu isiyovutia mimi always ntaomba summary kama ipo.
 
Back
Top Bottom