Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu

Sheikh Mohammed said,..
Naomba nkushaur mwalim wangu..
Umefka wakat Utuandikie kitabu cha Maisha yako na Picha zoote za Kihistoria zako utuwekee Lkn Utupe uhusiano na wote waloipgania Nchi yetu..
Hyo ni Kumbu Kumbu Nzur kwetu..
Ahsante
Always...
Unajua watu wengi sana wananiambia niandike kitabu maisha yangu.

Bahati mbaya mie siami hata kidogo kama ninalo la maana la kusema kuhusu mimi.

Ukiwa umenisoma hapa au kwenye blog yangu bila shaka utakuta kwa namna moja au nyingine nimewaeleza baadhi ya wapigania uhuru ambao nilipata kuwajua kwa mbali na wale niliokutananao uso kwa uso.

Wengine hawakuwa wapigania uhuru lakini ni watu muhimu katika historia ya Tanganyika na Tanzania.

Naingia Maktaba kupekura picha za hawa watu mashuhuri mnaotaka sana kuwajua kutoka kwangu.

1625309653101.png

Dome Okochi Budohi na Mohamed Said, Ruiru Nairobi 1972.

Dome Budohi alikuja Tanganyika kutafuta maisha na aliingia katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953 pamoja na Julius Nyerere katika uchaguzi wa rais ambao Nyerere aligombea nafasi ya urais dhidi ya Abdul Sykes.

Historia ya Dome Budohi nimeiandika katika kitabu cha Abdul Sykes kwa kirefu.
Mwaka wa 1954 ilipokuja kuundwa TANU Dome Budohi kadi yake ya TANU ikawa No.6.

1625310165739.png

Ally Sykes na Mwandishi, Muthaiga Club Nairobi 1989.

Amuhitaji maelezo hapa.
Huyu mtu maarufu.

Yeye na kaka yake wamempokea Nyerere 1952.
Kadi yake ya TANU No. 2.

Hii Muthaiga Club ni club ya millionaires ukimuona Mwafrika ndani yake basi ni mtumishi.
Ally Sykes alikuwa mwanachama toka mwaka wa 1967.

Baada ya Vita Vya Pili kumalizika Ally Sykes akiwa ndani ya meli akitokea Kalieni, Bombay (Mumbai) India pamoja na kaka yake na askari wengine yeye alitoroka Mombasa akaenda Nairobi kwa Peter Colmore kutafuta kazi.

Ally Sykes alikuwa na miaka 19.

Mimi na Ally Sykes pamoja tumeandika kitabu cha maisha yake, ''Under The Shadow of British Colonialism in Tanganyika.''

Hakijachapwa.

1625311996891.png


Peter Colmore na Mwandishi nyumbani kwa Peter Colmore Muthaiga, Nairobi wakati natafiti kitabu cha Ally Sykes 1995.

Huyu mtu ana historia nzuri sana.

Mimi nimemjua Peter Colmore toka 1964 alikuwa na ofisi yake Dar es Salaam Mtaa wa Lindi karibu na Mtaa wa Nkrumah jirani na nyumba tuiyokuwa tukiishi.

Alipofariki nilimwandikia taazia ambayo ilichapwa na The East African.Kenya
Mhariri alishangazwa vipi nimemjua Peter Colmore kwa kiasi kile kwani taazia ziizoandikwa na waandishi wengine wa Kenya zilikuwa nyepesi.

Ana mengi katika historia ya Tanganyika.
Itakuwa ndefu sana na tuiishie hapa.
 
Sheikh Mohammed said,..
Naomba nkushaur mwalim wangu..
Umefka wakat Utuandikie kitabu cha Maisha yako na Picha zoote za Kihistoria zako utuwekee Lkn Utupe uhusiano na wote waloipgania Nchi yetu..
Hyo ni Kumbu Kumbu Nzur kwetu..
Ahsante
Uchuro kujiandikia kitabu,akiandika tu bye bye.
 
Kede...
Nifafanulie sijaweza kuelewa.
Hamza Mwapachu baba yao ni Mdigo wa Tanga.

Mbona umetaja Kenya?
Au kuna mahali mimi sijaeleweka?

Tafadhali nifahamishe.
Pole mzee,nasikia mzee wao na akina mwapachu wakati anafariki watoto wake including wendo walikuwa wadogo sana hivyo wakalelewa na mwalimu nyerere sijui ikulu sijui msasani sijui
 
Baba yao akiitwa hamza mwapachu alikuwa naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani .alifariki 1962,akiwa na miaka 49,Tanga ni kwao kwa asili tu ila hao mjini kitambo

Hamza si alisoma n Nyerere Makerere?
Duh alikufa mapema sana kumbe
 
Mzee kumbe ulisoma St. Joseph's Convent!
Watu wengi wa zamani wamepita hapo, marehemu babangu mmojawapo
 
Mwapachu kafariki 1962
Sheikh Amri Abeid mwaka 1963..
Fundikira alishafukuzwa cabinet mwaka huo ..
Prominent Muslims were becoming even more fewer in the government..
The Boss,
Mwaka wa 1963 ulikuwa mwaka wa matukio makubwa kwa Waislam wa Tanganyika.

Ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU Julius Nyerere alipambana kwa maneno makali na Titi Mohamed ugomvi ukiwa Aga Khan na East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Ugomvi huu hakuweza kumalizika kwani wote wawili walikuwa na mfundo ndani ya nafsi zao.
Shariff Hussein Badawy na mdogo wake Mwinyibaba wakafukuzwa nchini warudi kwao Kenya.

Shariff Hussein alikuwa na madrasa kubwa Msikiti wa Badawy (sasa Rawdha).

Mwaka huo wa 1963 Bilal Rehani Waikela akakabiliana na Nyerere katika risala aliyosoma mbele yake katika ufungaji wa Muslim Congress iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Aga Khan ya Wasichana.

Mwaka huo Baraza la Wazee wa TANU chini ya uenyekiti wa Mzee Iddi Tulio likavunjwa kwa madai kuwa baraza lilikuwa linachanganya dini na siasa.

Wajumbe wote wa baraza hili walikuwa Waislam na lilitoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hiyo hapo juu nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Hapo chini ni picha ya Baraza la Wazee wa TANU:

1625423602593.png


1625423499981.png
 
Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu!

Leo jioni katika makaburi ya Kisutu tumemzika Wendo Mwapachu.

Nimemjua Wendo kwa kujulishwa kwake na Ted kama tulivyozoea kumwita.

Ted sasa hivi Chief Edward Makwai wa Siha ndiye aliyenijulisha kwake.

Wao ni ndugu wa damu na ni siku hiyo hiyo nilimjua kaka yake Juma Mwapachu na mdogo wao wa mwisho Jabe.

Siku hiyo nilikwenda kuhudhuria birthday party ya Ted rafiki na classmate form 1 D St. Joseph's Convent School.

Ilikuwa mwaka wa 1967.

Wendo akawa rafiki yangu hadi leo tunamtia kaburini.

Kuna picha mbili za kwanza za tukio moja nimeweka hapo chini, hii picha ina umri wa nusu karne.

Katika picha hiyo waliokaa kulia ni Wendo, Esther Mzena, Stella Emmanuel aliyesimama ni Kamili Mussa kulia waliosimama ni Haitham Rashid na mimi mwandishi na nyuma yangu ni Philip sikumbuki jina lake la pili ila namkumbuka alikuwa mtoto wa mmoja wa wapigania uhuru wa Afrika Kusini akisoma Shule ya Wakimbizi Kurasini sasa (Centre for Foreign Relations).

Tulikwenda picnic Kigamboni kwenye nyumba ambayo wakati wa ukoloni magavana ndipo walipokuwa wakienda kupumzika.

Baada ya uhuru nyumba hii ikawa mahali alipotakiwa apumzike rais wa Tanganyika Julius Nyerere na familia yake.

Taarifa ni kuwa Mwalimu hakuwa mtu wa kupenda kupumzika pwani mchangani hivyo nyumba hiyo sisi tukawa na fursa ya kuitumia kila tulipotaka kwani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi State House walikuwa vijana wenzetu.

Picnic hii ilikuwa mwaka wa 1968.

Leo naiangalia picha hii machozi yanataka kunitoka.

Hakika tumetoka mbali.
Namtazama Wendo na sura yake jamil.

Naona ni kama jana.

Picha nyingine kundi zima ''The Scorpions,'' lime ''pose.''

Kulia waliosimama Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bokhari, Abdallah Tambaza.

Waliochutama kulia: Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais.

Hii ilikuwa party ya kumuaga Liliane Abbas Sykes anakwenda shule Ufaransa mwaka wa 1968.

Lily kama tulivyopenda kumwita tulikuwa tukisoma pamoja hapo St. Joseph's Convent.

Hakika ni nusu karne lakini kila nikiipeleka akili yangu nyuma naona kama jana.

Namkumbuka Wendo kama alivyokuwa tukiwa watoto wadogo na jinsi alivyokuwa ukubwani.

Wendo alikuwa mtu wa kupendeka.

Nimeweka picha nyingine Wendo akiwa na Chief Edward Makwaia na Jenerali Ulimwengu ambae leo nyumbani kwa marehemu alimzungumza Wendo na akaeleza ule moyo wake wa huruma aliokuwanao na mkono mwepesi wa kuwasaidia wahitaji.

Picha hii nilimpiga kwenye msiba wa Kleist.
Namkumbuka Wendo Mtega Mwapachu.

Wendo alikuwa mtu mwema karim hujapata kuona.

Wendo hakuwa mzungumzaji alikuwa mtu mkimya.

Mara moja moja miaka ya nyuma mimi na yeye na jamaa tukiwa pamoja Wendo kwa kutambua mapenzi yangu kwa Prof. Ali Mazrui atanieleza jinsi alivyokuwa anaburudika na "lectures," za Mazrui wakati akisoma Makerere katika miaka ya mwanzoni 1970s.

Miaka hiyo Mazrui alikuwa akifundisha chuoni hapo.

Hapo chini ni moja kati ya kumbukumbu inayoishi moyoni kwangu ambayo Wendo ameniachia.

Mwaka wa 1991 nilikuwa naondoka Dar es Salaam kwa kipindi kirefu kidogo na safari siku ya pili.

Siku hiyo kabla ya safari wakaja vijana nyumbani kwangu wanatafuta msaada wa kujenga madrasa ya kisasa ya chekechea na kuendelea Mwananyamala A wawafundishe watoto kusoma, kuandika, hesabu na Qur' an.

Hii madrasa ilikuwa imeanzishwa na Bi. Fatuma na akisomesha mwenyewe kisha wanafunzi wake wakaichukua wakimsaidia kusomesha.

Hawa vijana ndiyo wakaja na fikra mpya ya kuiboresha madrasa yao iende na nyakati.

Hawa vijana wakaamua kuja kwangu niwatafutie mfadhili.

Mimi nikawachukua hadi kwa Wendo ofisini kwake Business Centre International (BCI).

Wendo akaniambia mimi nindelee na safari yangu na wale vijana nimwachie yeye.

Kama nilivyosema kuwa Wendo hakuwa mtu wa maneno mengi.

Tukaagana.

1992 niliporudi wale vijana wakanichukua hadi Mwananyamala A kunionyesha aliyofanya Wendo.

Nimeingizwa kwenye darasa safi la kisasa lina madawati mazuri wanasoma watoto wadogo.

Wale ndugu zangu wakaniambia kuwa fedha walizopewa na Wendo wao hawakutegemea zitakuwa nyingi kiasi kile alichowapa.

Siwezi kusema mengi kwani chuo hicho kimesomesha watoto wengi Qur'an na kinaendelea kusomesha hadi leo.

Allah mfanyie wepesi mja wako huyu, msamehe dhambi zake na mtie peponi.

Amin.





Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu
"Nimemjua Wendo kwa kujulishwa kwake na Ted kama tulivyozoea kumwita.
Ted sasa hivi Chief Edward Makwai wa Siha ndiye aliyenijulisha kwake.
Wao ni ndugu wa damu na ni siku hiyo hiyo nilimjua kaka yake Juma Mwapachu na mdogo wao wa mwisho Jabe".

Pumziko La Amani apate Bw Wendo.

Ufafanuzi kidogo hapo, Wendo na Ted au Chief Edward Makwai wa Siha ni ndugu wa damu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom