BURIANI Mhariri Willy Edward tutakukumbuka kwa hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BURIANI Mhariri Willy Edward tutakukumbuka kwa hili!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mongoiwe, Jun 17, 2012.

 1. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Siyo vyema kumsema marehemu, hivyo name sikusudii kumsema bali kueleza nitakachomkumbuka nacho. Lakini kwa desturi ya makabila ya Wajita, Wakerewe na kabila la Wajaruo ambalo ninaamini marehemu kama mtani wangu, lilikuwa kabila lake (Kama nitakosea kabira nisamehewe), msibani hulia wakati wa maombolezo kwa kueleza mambo ambayo marehemu alifanya wakati wa uhai wake.

  Kwa kuwa ni mtani wangu, ninachoeleza ni hiki ambacho kitanifanya kumkumbuka sana marehemu Willy Edward Ogunde.

  Ni kile ulichoakiandika kwa jina lako kwenye Gazeti lako la JAMBO LEO (Aprili 16, 2012) Ukurasa wa kwanza Maneno yakiwa na kichwa cha Habari kisemacho "Chadema Inahusishwa na mashetani, kwamba ‘Dk. Slaa ana jini lake linalomsaidia katika mambo yake ya kisiasa', na ukaongeza kwamba katika dini hiyo (Freemason) ‘Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa naye yumo".

  Ulikwenda zaidi ya hapo na hata kuwagusa Marehemu Kanumba na dini hiyo ya mashetani ambaye sasa nina hakika mkikutana huko mtaulizana vyema na kisha utuletee majibu ya uhakika.

  Katika kujenga hoja amewaonyesha viongozi mbalimbali wa Dunia kuwa ni waumini wa dini hyo ya kishetani..

  Ki ukweli andiko lako hili lilishambuliwa na kuitwa upotoshaji mkubwa, uzushi, uzandiki na uongo kwa umma. Nakumbuka hata mmoja alijaribu kukueleza ukweli huu, nanukuu hapa[FONT=&amp]:
  [/FONT]

  Hata mashabiki wa mpira hutmia, wachezaji na hata makocha wao (japo wengine hufikili kuwa wanamanisha watashnda goli mbili) siyo Chadema peke yao!"

  Hii ilianzia hapa jamiiforumu: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/251267-upotoshaji-huu-wa-gazeti-la-jambo-leo-ni-mpaka-lini.html

  Ninayakumbuka haya Mhariri, lakini ninakumbuka ulivyokoa busara hata ukamshambulia mwandishi mwenzako Frederick Katulanda pale alipoiweka habari hiyo katika Jukwaa la Mabadiliko, (sijui mliishia wapi ila nikusihii kumsamehe maana katika majadiliano yenu alisema kukusamehe).

  Ulichomjibu Katulanda kilikuwa hiki; nakukumbusha maana najua unaweza kuwa umeondoka bila ya kumbukumbu, kwani ninaamini wanaofariki hawabebi vitu kwenda navyo huko mbinguni ama ahera, soma majibu yako haya:


  Nikusihi basi huko uliko kuchunguza kwa makini jambo hili na kasha tutumie majibu yake, natambua mawasiliani ni shida baina ya huko na hapa duniani, lakini jaribu hata kutushushia kwa ndoto ili tujue ukweli maana kwa jinsi ulivyokufa Ghafla na hali ya mambo ilivyo sasa hapa Tanzania huku na wewe sasa utaanza kutajwa kuwa Ulikuwa Freemason.

  Ni hayo tu ambayo niliyawaza haraka baada ya kupata aarifa za msiba wako. Buriani mimi nitakumbuka kwa hayo!
   

  Attached Files:

  • WE.jpg
   WE.jpg
   File size:
   29.7 KB
   Views:
   24
 2. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Aisee..
   
 3. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,291
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  sadly, but dah si na la kusema, huyo ni matani wako mnajuana...
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Mmmh,
  kweli kumbe naye kaondoka tena, lol.
  Yake mbele yetu nyuma
   
 5. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali inapostahili.
   
Loading...