Taazia: Buriani Mwajame bint Dossa Aziz

Taazia: Buriani Mwajame bint Dossa Aziz

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,253
Reaction score
33,860
Nukuu za Simanzi na Buriani
Mohamed Said anaanza kwa kutoa taarifa ya kifo cha dada yake na kuelezea mazingira ya mazungumzo yao ya mwisho:
  • "Nimefiwa na dada yangu Mwajame Dosa Azizi Wajabe ni mkubwa kwangu mimi naikumbuka kama jana siku nilimtembelea nyumbani kwake Kigamboni ilikuwa mwaka wa 2023".
  • "Siku zote unapozungumza na watoto wa wapigania uhuru huwa mazungumzo ya simanzi na wanakueleza mengi ambayo wewe ulikuwa huyajui".
  • "Wanahistoria wamewapuzi wazee hawa kiasi kwamba hawajawapa heshima".
Siri ya Handaki la Nyerere (Ruvu)
Mwajame alimfichulia Mohamed Said siri kuhusu baba yake (Dossa Aziz) kumjengea Mwalimu Nyerere nyumba ya chini ya ardhi (handaki) kwa ajili ya usalama:
  • "Mohamed ulikuwa na shamba zuzuri sana la baba pale... kulikuwa na handaki... walijenga endapo waingereza wakati ule wa kugombea kupigana uhuru watamkamata mwalimu nyerere".
  • Dossa Aziz alimwambia Nyerere: "Kambarage... hapa endapo tutoke kitu chochote basi wewe tutakuweka hapa huku tunafanya mipango wewe ya kukutorosha nje ya nchi hii lakini hatuwezi kukubali sisi kukuona wewe wanakufanya kama walivyomfanya Kenyatta".
Nukuu Kuhusu Maasi ya Jeshi ya Mwaka 1964
Mwajame alisimulia ujasiri wa baba yake wakati wa maasi ya kijeshi ya Januari 1964:
  • Dossa Aziz alimwambia mkewe: "Namwacha mke wangu hapa nagla mimi nakwenda mjini kumtafuta Nyerere nijue yuko wapi... siwezi kukaa hapa... wakati mimi sijui ndugu yangu Kambarage hali yake ikoje".
  • Baada ya kurudi jioni akiwa amechoka, alijibu kwa ufupi kuhusu usalama wa Nyerere: "Kambarage salama... nimekuambia salama sawa".
Malalamiko ya Watoto wa Wapigania Uhuru
Mwajame alieleza masikitiko yake kuhusu namna familia za wapigania uhuru zinavyosahaulika na kudhulumiwa:
  • "Baada ya baba kufariki tumepoteza ardhi zetu nyingi sana... na cha kusikitisha ni kuwa watu wanaochukua zile ardhi ni watu ambao wako serikalini na watu ambao walikuwa wanamjua baba yetu".
  • Dada mwingine, Aisha Wahid, alinukuliwa akisema: "Mimi kwa dhati niliumia sana kuwa na magazeti ya TANU The Nationalist na Uhuru hakuna lolote lililoandika hata tazia baba yangu".


View: https://youtu.be/sPQbHkLYFYA?si=Mu-sT7R5cVQAqX6C
 
Kinyungu,
Hapakuwa na kitu kama hicho.
Mwajame ni mtoto wa Dossa Aziz.

Wakati wa kupigania uhuru alikuwa msichana mdogo akisoma Al Jamiatul Islammiya Muslim School.
Asante kwa ufafanuzi

Hiyo shule ya Al Jamiatul Islammiya Muslim School ndiyo Zanaki au?
 
Asante kwa ufafanuzi

Hiyo shule ya Al Jamiatul Islammiya Muslim School ndiyo Zanaki au?
Kinyungu,
Zanaki ilikuwa Aga Khan School.
Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika Muslim School ni shule ilijengwa 1933 na Waislamu wale waliounda African Association 1929.
 
Mambo ya familia yako hayo ndiyo unapenda kuyaanika hadharani halafu unadai ni historia iliyosahaulika.
Huihui,
Ikiwa haikufutwa ilikuwa ikijulikana yote sawa tuendelee na mengine.
 
First of all, it is important to understand that sex dolls were not created solely for sexual purposes; their functions extend far beyond that. In fact, their most significant role lies in alleviating loneliness.
 
Kinyungu,
Zanaki ilikuwa Aga Khan School.
Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika Muslim School ni shule ilijengwa 1933 na Waislamu wale waliounda African Association 1929.
Kwa sasa iko wapi hiyo shule? Au inaitwaje kwa sasa?
 
Kinyungu,
Shule Iko Mtaa wa Max Mbwana (zamani Stanley kisha Aggrey na sasa Max Mbwana) kona na Lumumba Avenue (zamani New Street).

Sasa shule inaitwa Lumumba.
Nimekupata.

Mtaa wa Aggrey nao umeshabadilishwa jina?
 
Loooh. Kwa hiyo kwa sasa Aggrey hana mtaa hapo Dar es Salaam?🥲
Kinyungu,
Dr. Kweggyr Aggrey hana Mtaa Dar es Salaam.

Lakini ni hicho kibao cha Mtaa kuonyesha jina la Max Mbwana hakijawekwa sasa miaka kama cha Mshume Kiyate ambacho nacho hakijawekwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom