Buriani AISHA MUNGU AKULAZE PEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Buriani AISHA MUNGU AKULAZE PEMA!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchaga, Nov 3, 2008.

 1. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Machozi yananitoka Aisha wakati naandika maandishi haya machache wakati ukiwa umefunikwa na udongo na mifupa yako ikiliwa na ardhi.

  Aisha uliamka asubuhi na mapema katika kambi ya wakimbizi ukitarajia kuwa siku moja utaweza tena kuishi na ndugu jamaa na marafiki na kufurahia maisha kama binadamu wengine.

  Aisha hukujua ya kuwa ulimwengu na hadaa na kuna bin adam na bin shetani ambao wote wanaishi katika ulemwengu huu ulijaa kila aina ya ufisadi, chuki na matatizo yasiyo na mwisho....aisha moyo wangu unaniudunda na mapigo ya moyo ni kama vile yanataka kusimama ninavyo wafikiria wale wanaume 1000 waliokuja kushuhudia kifo chako kama vile wanaangalia mpira kombe la dunia...Aisha nakulilia kwa sababau sikupata fursa ya kuwa katika uwanja kwani na mimi ningepigwa risasi kama yule kijana aliyepigwa risasi akitaka kuoka maisha yako.

  Aisha umenishangaza kwani wakati unapigwa mawe ulikuwa unatabasamu na kumwomba Alah akupumzishe na mateso ya dunia hiii....Aisha ni kwanini lakini wamekuua eti kisa umeshtaki umebakwa? Ndani ya nchi yako ni wanawake wangapi waliobakwa na ambao hawatasema kwa kuhofia lile truck lilobeba mawe na wanaume 1000 kuja kushuhuduia jinsi unavyokufa kwa mateso na fedheha....hiii ni aibu na unyama wa kutisha sana.

  Aisha siku ya kwanza ulivyobakwa.....siwezi kuvumila machozi yananitoka na kushusha pumzi kwa jazba na hasira. Aisha siku ya kwanza ulivyobakwa ulikwisha kufa ila MUNGU alitaka uwe shujaa kwa wengine na ulete mabadiliko katika jamii. Wewe ni shujaaa na utabaki kuwa hivyo kwani ni Mungu pekee mweye mamlaka ya kuchuka uhai wako na wala sio bin adam.

  Aisha wakakupiga mawe na kuwatuma manesi wakuangalie kama umekwisha kata roho..eti umekwisha kata roho wanaijua? aisha ulifumba macho kwa huzini na wala hukujutia kitendo chako cha kusema umebakwa kwani ulijua wazi yatakayokukuta lakini ulitaka kuleta mabadiliko na dunia isikie na wamesikia...Aisha hupoulipo fahamu ya kuwa yupo Mchaga anayekupenda tena sana na nitaendelea kukupenda daima nitakulilia na wala hazina yangu ya machozi kamwe haitakauka...

  Aisha sina la zaidi lakuongeza lakini napenda kukuambia roho yako na ujasiri wako utandelea kuishi kwani wameua mwili lakini hawajaua kauli na tendo lako la kishujaa. Aisha uliishi katika kipindi kigumu kwa miaka 13, eti wanasema ulikuwa na miaka zaidi ya hiyo...walitaka tu kuhalalisha kifo chako...natambua ya kuwa kwa mateso makali uliyoishi chini ya jua ulistahili kuonekana una umri zaidi ya huo.

  Aisha wapo wengi waliokupenda kuliko waliokuchukia kwani wakati unapeigwa mawe wapo waliojitokeza kutaka kukuoka hawa ndi bin adam lakini walizidiwa na bin shetani na hivyo ndoto yako yakutaka kuleta mabadiliko ikatimia...

  Mikono na vidole vyangu vinatetemeka kw hasira na chuki kali dhidi ya hawa waliokupiga mawe, natamani ningepata na mimi fursa ya kuwa na wewe pamoja nikakukumbatia na kukutia moyo wakati wote tukipigwa mawe.

  RIP.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sahih Bukhari V9 B89 #79 :

  I asked the Prophet, "O Allah's Apostle! Should the women be asked for their consent to their marriage?" He said, "Yes." I said, "A virgin, if asked, feels shy and keeps quiet." He said, "Her silence means her consent."
   
 3. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Baada ya wanaume wenye nguvu wapatao 50 kukabidhiwa mawe toka kwenye roli wamempiga yule mtoto hadi akawa nusu mfu.
  Manesi wakaambiwa wathibitishe kama kafa ama la.
  Manesi wakasema bado hajafa, wakafukuwa tena lile shimo na kuendelea kumpiga mawe hadi binti ukakata pumzi.
  Zilaaniwe aya za namna hii.
  Tanzania hatutaki OIC kuingia kwetu. Wanaotaka waende ilikotoka.
   
 4. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni sheria za kikatili kwa kweli! MUNGU ATUEPUSHE NA HAYA
   
 5. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2008
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  This is a very moving Factual piece....It moved me almost to tears. Truly what happened to Aisha was Very Cruel. Tanzania doesn't need this. Therefore....NO O.I.C.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hakuna binadamu mwenye akili timamu anaweza ua mtu kwa mawe... Lazima hao wa psychosis ya namna fulani, hata kama wangekua wasafi na si wazinzi!!!

  Sina cha kusema kuhusu oic kwa sababu sijui nani alienda kufukua maiti iliyokwishazikwa zamani, btw hivi ni kwanini hawa akina membe walileta huu mjadala uliokwisha? Damu ya wakristu itakayomwagika na iwe mikononi mwao na vizazi vyao
   
Loading...