Bungeni: Waziri Mpango asema Serikali imetenga bajeti 2017/18 kufufua kiwanda cha General Tyre

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,359
2,000
Serikali imetoa takwimu ikielezea hali ya ukuaji uchumi katika kipindi cha mwaka 2016.

Mpango Bajeti.png

Waziri Dk. Philip Mpango

=> Kiwango cha ukuaji uchumi 2016/2017kimeendelea kukua kwa wastani wa asilimia saba ikiwa ni pungufu kidogo ya kile kilichotarajiwa awali. Makadirio ya awali yalionyesha kuwa uchumi huo ungekua kwa wastani wa asilimia 7.2.

=> Hali ya ukuaji uchumi imeendelea kushuhudiwa katika kiwango kilekile cha awali cha asilimia saba na hii imechangiwa na mambo mengi ikiwamo baadhi ya sekta kutofanya vizuri. Sababu hizo ni pamoja na kushuka wa sekta ya kilimo iliyotarajiwa kukua kwa asilimia 2.9, lakini malengo hayo hayakufikiwa na badala yake yalikuwa kwa asilimia 2.1.

=> Sekta ya biashara ilikuwa 6.7% hali ambayo ni tofauti na makadirio yaliyowekwa awali yaliyokuwa 7.8%

=> Eneo la chakula limechangia kufikia kwa malengo ya ukuaji uchumi. Makadirio yetu yalikuwa kwamba sekta ya chakula ingekua kwa 8%, lakini bahati mbaya ilishuka na kuwa 3.7%.

=> Kuna sekta zimefanya vizuri na kusaidia uchumi wa Taifa, sekta hizo ni pamoja na habari na mawasiliano, madini na kiashirio cha kuendelea kukua kwa sekta ya viwanda.

=> Kwa mwaka 2016/2017 Serikali ilipanga kutumia Shilingi Bilioni 11,820.5 kwa ajili ya bajeti ya mandeleo. Hadi April 2017 fedha zilizokuwa zimetolewa ni Shilingi Bilioni 4516.7 sawa na Asilimia "38" ya Bajeti nzima.

2017/2018

=> Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya kufufua kiwanda cha matairi yaani General tyre.

=> Serikali inafanya utaratibu katika kuboresha maisha ya wananchi na watumishi wa umma kwa kuweka malengo na bajeti katika kutekeleza hayo.
 

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,317
2,000
Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philip Mpango amesema serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 kwaajili ya kufufua kiwanda cha matairi yaani General tyre, Dr Mpango amesema hayo leo bungeni wakati akitoa hotuba ya hali ya uchumi nchini na mpango wa maendeleo wa Taifa katika kikao cha bajeti cha bunge la 11,

Aidha Dr Mpango amesema serikali inafanya utaratibu katika kuboresha maisha ya wananchi na watumishi wa umma kwa kuweka malengo na bajeti katika kutekeleza hayo.Vilevile Dr Philip Mpango amesema serikali itashirikiana na sekta binafsi katika kupanua wigo wa ajirakwa kushirikiana na baraza la biashara la taifa yaani NBC kwa kujadiliana jinsi ya kuboresha biashara na ajira kwa wananchi
 

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,317
2,000
Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mpango amesema serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 kwaajili ya kufufua kiwanda cha matairi yaani General tyre,

Dr Mpango amesema hayo leo bungeni wakati akitoa hotuba ya kuwasilisha mpango wa maendeleo wa Taifa katika kikao cha bajeti cha bunge la 11, aidha Dr Mpango amesema serikali inafanya utaratibu katika kuboresha maisha ya wananchi na watumishi wa umma kwa kuweka malengo na bajeti katika kutekeleza hayo.
 

StingRay

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
478
1,000
Why most of our projects fail to deliver and impact our community and a country as whole because of too many cooks!!!!!
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,611
2,000
Vipi kuhusu viwanda vingine kama Machine tools, wana mpango gani navyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom