Bungeni: Wabunge wapinga kanuni mpya za 'kuwaziba midomo'

Wayyi

Member
May 26, 2012
14
0
Mchakato wa marekebisho ya kanuni za Bunge umeibua mjadala mkali baina ya wabunge, huku wengi wao wakieleza kuwa hatua hiyo ina lengo la kulifanya Bunge kukosa meno ya kuisimamia Serikali.

Miongoni mwa mambo yaliyozua mvutano katika kikao cha awali cha wabunge wote ni suala la muda wa wabunge kuchangia bungeni na jinsi wanavyotakiwa kupangwa kulingana na idadi yao kwa kila chama.

Bunge linakusudia kuwasilisha azimio la kutaka kubadili kanuni ambazo zilitarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika jana bungeni, lakini kutokana na baadhi ya mapendekezo kupingwa, hatua hiyo iliahirishwa hadi leo.

Mabadiliko hayo ni muhimu kabla ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuwasilishwa leo, kwani baadhi yake yanalenga kuwezesha mfumo mpya wa Bunge wa kuanza na Bajeti za wizara na baadaye kumalizia na Bajeti Kuu ya Serikali.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika juzi jioni na kuendelea jana, wabunge karibu wote walipinga pendekezo la kamati ya kanuni la kutaka kupunguza muda wa mbunge kuchangia mjadala kutoka dakika 15 zinazotajwa kwenye kanuni ya sasa Kifungu cha 62 (1) hadi dakika 10.

Suala jingine ambalo limeingizwa kwenye kanuni na ambalo limekuwa linapendekezwa na wabunge wa CCM la kutaka wabunge wapate nafasi za kuzungumza kulingana na idadi yao katika kila chama.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kikao hicho kimesema endapo suala hilo litapitishwa, kulingana na mgawanyo wa wabunge kivyama, itabidi wazungumze wabunge wa CCM zaidi ya 10 ndipo apate nafasi mmoja kutoka kambi ya upinzani.

Pia wabunge katika kanuni mpya, wakati wa kujadili bajeti hawataruhusiwa kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa suala hilo ambalo lilizua mvutano kutokana na kuungwa mkono na wabunge wa CCM, huku likipingwa na wabunge wa upinzani, linaelekea kupitishwa kutokana na wingi wa wabunge wa chama tawala.

Kutokana na mjadala huo, ilibidi mambo mengine yarejeshwe kwenye kamati ya kanuni ili kufanyiwa marekebisho kutokana na ushauri wa wabunge.

Masuala mengine ni katika majukumu ya kamati za Bunge ambayo yakipitishwa kamati hizo hazitaweza kufuatilia sera ya ubinafsishaji wala kufanyia tathmini mashirika ya umma kwa kuwa vifungu vilivyokuwa vinaruhusu hali hiyo kwenye nyongeza ya nane, kifungu cha 13 havikuingizwa katika mapendekezo mapya.

"Kwa jumla kanuni hizi mpya zinapendekeza kamati za Bunge zisiwe zinatoa maagizo, bali zitoe ushauri na hii ni sawa na kuling'oa meno Bunge," kilisema chanzo kingine.

SOURCE: MWANANCHI JUMATANO APRIL 10, 2013
 
watakaa kama kamati ya wabunge wa chama cha mapinduzi chini ya uwenyekiti wa mtoto wa mkulima -- ngoma itanyenyuka tu, hiyo ndiyo huwa dawa yake.
 
Unaweza kuona udhalimu Mkubwa uliyopo ndani ya Serikali hii ya CCM,. inashangaza kuwa na wabunge wasioona haya kuunga mkono udhalimu huu ati kwasababu tu wanatoka chama tawala., hii inaudhi, lakini zaidi sana inaondoa uvumilivu wa watu kwa serikali hii.,

Inatuonyesha nia hasa ya watu hawa, niku "tawala" na si kuongoza., nikunufaika, nasi kuwajibika!
lakini laiti wangejua, sifa kubwa ya watawala hua ni anguko!,

Na lakwao haliko mbali sana, linakuja.
tutaendelea kuwapigia kelele., hatutachoka nasiku ikifika tutawawajibisha.
 
Dawa yake ni siku moja kumpandia huyu mama Makinda na kumtandika makofi. Amekuwa naibu wa Sitta, alishindwa kujifyunza uendeshaji wa bunge--sasa yeye kutafuta njia ya kubana upinzani tu...Anyway, anafanya kazi aliyotumwa na mafisadi.
 
Kha kumbe Bunge limejaa majambazi yasiyowakilisha wapiga kura! hata mmoja. Kwamba hata Mibunge ya CCMajambazi hayana hoja basi yaongee tu utumbo ili kumaliza muda tunaolipia kodi zetu. Lakini hata wanaCCM waelewe tu Ukandamizaji wa hali ya juu unapofikia UPEO sasa kila mmoja ajiandae na ANGUKO!
 
Mapendekezo yote kama yatapita nayaona ni hatari ka ustawi wa bunge lenyewe na wabunge wenyewe hasa wa uoinzani ambao ni wazi watakuwa wamekandamizwa sana.
 
Mimi sioni hata haja ya wabunge wa upinzani kuwepo bungeni kwani Bunge la huyu mama ni kama Kikao cha chama kujadili sera za chama ilimradi tu linaitwa bunge. Bunge gani linashindwa kutekeleza wajibu wake kwa wananchi. Watoto wanafail, kila kitu kinapanda maisha magumu rushwa inaongezeka eti kuna bunge. Huyu mama kafanya bunge kuwa taasisi ya chama ndani ya serikali kiasi kwamba bunge linashindwa kusimamia misingi yake kazi imekuwa ni kubadili kanuni tu kila kukicha ili mradi tu wengine wasiongee. Halina maana ya kuitwa Bunge
 
Alafu uatsikia....sisiemu imetutoa mbali....kuipenda sisiem ni lazima uwe na matatizo ya akili
 
Mchakato wa marekebisho ya kanuni za Bunge umeibua mjadala mkali baina ya wabunge, huku wengi wao wakieleza kuwa hatua hiyo ina lengo la kulifanya Bunge kukosa meno ya kuisimamia Serikali.

Miongoni mwa mambo yaliyozua mvutano katika kikao cha awali cha wabunge wote ni suala la muda wa wabunge kuchangia bungeni na jinsi wanavyotakiwa kupangwa kulingana na idadi yao kwa kila chama.

Bunge linakusudia kuwasilisha azimio la kutaka kubadili kanuni ambazo zilitarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika jana bungeni, lakini kutokana na baadhi ya mapendekezo kupingwa, hatua hiyo iliahirishwa hadi leo.

Mabadiliko hayo ni muhimu kabla ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuwasilishwa leo, kwani baadhi yake yanalenga kuwezesha mfumo mpya wa Bunge wa kuanza na Bajeti za wizara na baadaye kumalizia na Bajeti Kuu ya Serikali.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika juzi jioni na kuendelea jana, wabunge karibu wote walipinga pendekezo la kamati ya kanuni la kutaka kupunguza muda wa mbunge kuchangia mjadala kutoka dakika 15 zinazotajwa kwenye kanuni ya sasa Kifungu cha 62 (1) hadi dakika 10.

Suala jingine ambalo limeingizwa kwenye kanuni na ambalo limekuwa linapendekezwa na wabunge wa CCM la kutaka wabunge wapate nafasi za kuzungumza kulingana na idadi yao katika kila chama.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kikao hicho kimesema endapo suala hilo litapitishwa, kulingana na mgawanyo wa wabunge kivyama, itabidi wazungumze wabunge wa CCM zaidi ya 10 ndipo apate nafasi mmoja kutoka kambi ya upinzani.

Pia wabunge katika kanuni mpya, wakati wa kujadili bajeti hawataruhusiwa kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa suala hilo ambalo lilizua mvutano kutokana na kuungwa mkono na wabunge wa CCM, huku likipingwa na wabunge wa upinzani, linaelekea kupitishwa kutokana na wingi wa wabunge wa chama tawala.

Kutokana na mjadala huo, ilibidi mambo mengine yarejeshwe kwenye kamati ya kanuni ili kufanyiwa marekebisho kutokana na ushauri wa wabunge.

Masuala mengine ni katika majukumu ya kamati za Bunge ambayo yakipitishwa kamati hizo hazitaweza kufuatilia sera ya ubinafsishaji wala kufanyia tathmini mashirika ya umma kwa kuwa vifungu vilivyokuwa vinaruhusu hali hiyo kwenye nyongeza ya nane, kifungu cha 13 havikuingizwa katika mapendekezo mapya.

“Kwa jumla kanuni hizi mpya zinapendekeza kamati za Bunge zisiwe zinatoa maagizo, bali zitoe ushauri na hii ni sawa na kuling’oa meno Bunge,” kilisema chanzo kingine.

SOURCE: MWANANCHI JUMATANO APRIL 10, 2013

C:C- ZeMarcopolo
majebere
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kuona udhalimu Mkubwa uliyopo ndani ya Serikali hii ya CCM,. inashangaza kuwa na wabunge wasioona haya kuunga mkono udhalimu huu ati kwasababu tu wanatoka chama tawala., hii inaudhi, lakini zaidi sana inaondoa uvumilivu wa watu kwa serikali hii.,

Inatuonyesha nia hasa ya watu hawa, niku "tawala" na si kuongoza., nikunufaika, nasi kuwajibika!
lakini laiti wangejua, sifa kubwa ya watawala hua ni anguko!,

Na lakwao haliko mbali sana, linakuja.
tutaendelea kuwapigia kelele., hatutachoka nasiku ikifika tutawawajibisha.

Uhai wa nyavu ni matundu uhai wa ccm ni pamoja na udhalim hakuna jipya ccm zaidi ya kuzidi kuumbuka
 
Back
Top Bottom