Elections 2010 Bungeni: Upinzani wapendekeza serikali 3 Tanzania

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Na Restuta James

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imependekeza kuundwa kwa serikali tatu; ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar, ili kuondoa hisia za upande mmoja wa Muungano kunyonywa pamoja na mambo yanayoonekana ni kero.

Pia imependekeza mafuta ya Zanzibar yaamuliwe na wananchi wa visiwa hivyo kwa kuwa vina rasilimali chache.

Waziri Nchi Kivuli, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Pauline Gekul, aliliambia Bunge jana kuwa kuundwa kwa serikali tatu kutaondoa kero za Muungano na kuufanya uwe endelevu kwa maslahi ya wananchi wa pande zote.

"Ni vyema serikali ikazingatia umuhimu wa kuwapo serikali tatu kwenye mchakato wa Katiba mpya…suala la mafuta liachwe mikononi mwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwa visiwa hivi vina rasilimali chache sana za kiuchumi," alisema Gekul.

Alisema ili kudumisha Muungano, serikali inapaswa kujenga utamaduni wa kuitisha mikutano maalum ya kikatiba kati ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ili wawakilishi waweze kujadili masuala yanayohusu uhusiano wao.

"Pia tunashauri kuwapo kwa kikao cha pamoja cha uongozi wa ngazi ya taifa kutoka pande zote za Muungano," alisema Gekul.

Kambi hiyo imependekeza uanzishwaji wa Mahakama ya Muungano ya Katiba itakayosuluhisha malalamiko yanayohusu Muungano.

"Masuala ya rasilimali nyingine yatajadiliwa ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na rasilimali za Tanzania na inatoa mchango wake sahihi katika uchumi wa taifa," alisema Gekul.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia walishauri serikali iwachukulie hatua watumishi wanaoonekana kuchangia kero za Muungano.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alishauri kwamba kuna haja ya wabunge kupewa semina na ili wauelewe Muungano kwa kuwa asilimia 55, ni vijana ambao hawauelewi vizuri.

Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wamekuwa wakitaka Muungano uvunjwe bila kuelewa athari au sababu za kuwepo kwake, kwa kuwa michango yao mingi imekuwa ni ya kusoma au kusikia.

Alisema inashangaza kusikia baadhi ya wabunge wakieleza kwamba Zanzibar imemezwa na serikali ya Muungano wakati ndani ya Bunge wapo wabunge wanaotoka Zanzibar kupitia Muungano.

"Wengine wanasema Zanzibar imemezwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania wakati hata mimi leo ni mbunge kutokana na Muungano huo sasa tumemezwa wapi na mimi natokea Zanzibar," alisema.

Mbunge huyo alisema Muungano una manufaa kwa Watanzania wote na kwamba, unapaswa kulindwa kwa nguvu na gharama yoyote.

Alisema wanaobeza Muungano wanamkatisha tamaa Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuhakikisha Muungano unadumu.

Mbunge wa Wete (CUF), Ali Mbarouk, alisema kuna kero ndogondogo za Muungano, ambazo zimeingizwa kwenye kamati inayozishughulikia na kuchukua mchakato mrefu bila sababu za msingi.

Alisema inashangaza kuona kero kama ya kutoza ushuru bidhaa zinazotoka upande mmoja wa Muungano kwenda upande mwingine.

Mbunge wa Meatu (Chadema), Meshack Opurukwa, alisema serikali tatu ndilo jibu pekee la kuondoa kero za Muungano zilizopo.

Alisema nia ni kuhakikisha kuwa serikali ya Muungano itakuwa na jukumu la kutatua matatizo ya serikali zote mbili.

Opurukwa alisema masuala kama kodi, umeme na rasilimali, yataweza kutatuliwa na serikali husika na iwapo kutakuwapo kero yoyote, itashughulikiwa na serikali ya Muungano.

Awali, Waziri wa wizara hiyo, Samia Hassan Suluhu, alisema serikali imekuwa ikishughulikia kero za Muungano na kwamba, jukumu hilo ni endelevu hadi zitakapokwisha
 
Nilisema jana kuwa Lissu kwa hoja yake ya hati za muungano ni kama CHADEMA wapiga hodi ya nguvu Zanzibar. Leo naweza kusema kwa kauli ya huyu msemaji wa CHADEMA (Mh. Pauline) ni kama chama hiki kimekaribiswa sebuleni huko Zanzibar na watakuta tende, chai na halua mezani huku sebule ikiwa imetanda maua ya 'kilua na jasmine'.

CCM - you've been cornered on this one. Na huyo mbunge wa viti maalum (ccm) anayesema wabunge wengi ni vijana, hawajui muungano hivyo wafanyiwe semina, inabidi atambue kuwa zaidi ya 60% ya watanzania wote wana umri chini ya 30! Na Zanzibar ambako muungano ni shubiri kwa sasa takribani 80% ya wakazi wake wana umri chini ya miaka 40! Huu wimbo wa kuwa muungano una faida, ulindwe kwa nguvu zote umekuwa unaimbwa kwa miaka yote lakini sasa watanzania wamekuwa wanataka kuwa na muungano 'shirikishi'.

Hakuna semina, warsha au kikao cha aina yoyote kwa wabunge kinaweza kubadilisha mawazo, mtazamo na madai ya wananchi (Tz Bara & Zanzibar), na CHADEMA, again, wanaonekana kulitambua hili ndio maana wanafanya 'people's politics- bungeni'. CCM have only one option - Zanzibar, to comply with CHADEMA's views or die. In otherwords, CCM hawana option.
 
Unajua CCM walipoizima hoja hii kinguvu mwaka 1993 walidhani Watanzania wataendelea kuwa walivyo miaka yote. Sasa kikombe walichokikwepa kipindi kile leo wanacho tena.
 
........ Na huyo mbunge wa viti maalum (ccm) anayesema wabunge wengi ni vijana, hawajui muungano hivyo wafanyiwe semina, inabidi atambue kuwa zaidi ya 60% ya watanzania wote wana umri chini ya 30! Na Zanzibar ambako muungano ni shubiri kwa sasa takribani 80% ya wakazi wake wana umri chini ya miaka 40! Huu wimbo wa kuwa muungano una faida, ulindwe kwa nguvu zote umekuwa unaimbwa kwa miaka yote lakini sasa watanzania wamekuwa wanataka kuwa na muungano 'shirikishi'.

Mkuu unajua uitakakujua watu wenye mawazo mgando ndio hao hao watupeleke mbele. Hawajui hii karne ya sayansi na Teknolojia.

Kuna video conferencing, teleconfeerencing, Social Media, etc

So
  • Semina sio lazima watu waende Ngurdoto au Golden tulip kama alivyo kalili yeye. Jamiiforum ni ngurdoto( electonically).
  • twitter , facebook ndio Idara ya habari Maelezo ya kizazi cha sasa. Nimeshanga kuna mbunge anatuhumiwa kukwapua taulo hotelini lakini hajatoa statement. Labda anasubiri Idara ya habari maelezo ya mwaka 1970.
Sasa viongozi kama hao ndio tunatagemea wawe na mawazo ya kulipeleka taifa letu mbele ????!!!!!!!!

Angejua vijana anaosema wako more informed kuliko yeye.
 
..sidhani kama wamewasikiliza wa-ZNZ kwa umakini.

..wa-ZNZ wanataka kujiongoza wenyewe kama Kenya,Rwanda,Burundi, etc etc.

..serikali 3 hazitakidhi matakwa ya wa-ZNZ kuendesha mambo yao vile wanavyotaka.
 
Na Restuta James
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imependekeza kuundwa kwa serikali tatu; ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar, ili kuondoa hisia za upande mmoja wa Muungano kunyonywa pamoja na mambo yanayoonekana ni kero.

Pia imependekeza mafuta ya Zanzibar yaamuliwe na wananchi wa visiwa hivyo kwa kuwa vina rasilimali chache.
Waziri Nchi Kivuli, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Pauline Gekul, aliliambia Bunge jana kuwa kuundwa kwa serikali tatu kutaondoa kero za Muungano na kuufanya uwe endelevu kwa maslahi ya wananchi wa pande zote.

"Ni vyema serikali ikazingatia umuhimu wa kuwapo serikali tatu kwenye mchakato wa Katiba mpya…suala la mafuta liachwe mikononi mwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwa visiwa hivi vina rasilimali chache sana za kiuchumi," alisema Gekul.
Alisema ili kudumisha Muungano, serikali inapaswa kujenga utamaduni wa kuitisha mikutano maalum ya kikatiba kati ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ili wawakilishi waweze kujadili masuala yanayohusu uhusiano wao.

"Pia tunashauri kuwapo kwa kikao cha pamoja cha uongozi wa ngazi ya taifa kutoka pande zote za Muungano," alisema Gekul.
Kambi hiyo imependekeza uanzishwaji wa Mahakama ya Muungano ya Katiba itakayosuluhisha malalamiko yanayohusu Muungano.
"Masuala ya rasilimali nyingine yatajadiliwa ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na rasilimali za Tanzania na inatoa mchango wake sahihi katika uchumi wa taifa," alisema Gekul.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia walishauri serikali iwachukulie hatua watumishi wanaoonekana kuchangia kero za Muungano.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alishauri kwamba kuna haja ya wabunge kupewa semina na ili wauelewe Muungano kwa kuwa asilimia 55, ni vijana ambao hawauelewi vizuri.
Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wamekuwa wakitaka Muungano uvunjwe bila kuelewa athari au sababu za kuwepo kwake, kwa kuwa michango yao mingi imekuwa ni ya kusoma au kusikia.

Alisema inashangaza kusikia baadhi ya wabunge wakieleza kwamba Zanzibar imemezwa na serikali ya Muungano wakati ndani ya Bunge wapo wabunge wanaotoka Zanzibar kupitia Muungano.
"Wengine wanasema Zanzibar imemezwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania wakati hata mimi leo ni mbunge kutokana na Muungano huo sasa tumemezwa wapi na mimi natokea Zanzibar," alisema.

Mbunge huyo alisema Muungano una manufaa kwa Watanzania wote na kwamba, unapaswa kulindwa kwa nguvu na gharama yoyote.
Alisema wanaobeza Muungano wanamkatisha tamaa Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuhakikisha Muungano unadumu.
Mbunge wa Wete (CUF), Ali Mbarouk, alisema kuna kero ndogondogo za Muungano, ambazo zimeingizwa kwenye kamati inayozishughulikia na kuchukua mchakato mrefu bila sababu za msingi.

Alisema inashangaza kuona kero kama ya kutoza ushuru bidhaa zinazotoka upande mmoja wa Muungano kwenda upande mwingine.

Mbunge wa Meatu (Chadema), Meshack Opurukwa, alisema serikali tatu ndilo jibu pekee la kuondoa kero za Muungano zilizopo.
Alisema nia ni kuhakikisha kuwa serikali ya Muungano itakuwa na jukumu la kutatua matatizo ya serikali zote mbili.
Opurukwa alisema masuala kama kodi, umeme na rasilimali, yataweza kutatuliwa na serikali husika na iwapo kutakuwapo kero yoyote, itashughulikiwa na serikali ya Muungano.
Awali, Waziri wa wizara hiyo, Samia Hassan Suluhu, alisema serikali imekuwa ikishughulikia kero za Muungano na kwamba, jukumu hilo ni endelevu hadi zitakapokwisha

Hivi baadhi ya Wabunge hawauelewi Muungano, mnafanya nini humo. Mnafikiri semina ya wiki moja au mwezi itawafanya muelewe Muungano.Naanza kuamini kumbe baadhi ya Wabunge ni wavivu kujisomea. Laiti mngekuwa mnasoma historia ya Tanzania, msingetaka Semina. Au ni janja mnataka kuongeza wigo wa mapato (Sitting allowance)
 
Serikali moja ndo inafaa na ndo ilikuwa iwe hivyo, ingawa kuna hotuba ya Mzee Karume akifananisha muungano na koti na ukiona linakubana unalitupilia mbali. Tulicho nacho sasa ni Serikali tatu ila sisi hatujui tu au tunachagua kuto kujua, mfano haingii akilini kuwa na wabunge utitili kutoka Zanzbar ndani ya bunge la muungano wakati hata siku moja sijasikia rais wa muungano anaalikwa kwenye vikao vya Baraza la wawakilishi!
 
Bado mtoto wewe,rudi shule usome.
 
Nilisema jana kuwa Lissu kwa hoja yake ya hati za muungano ni kama CHADEMA wapiga hodi ya nguvu Zanzibar. Leo naweza kusema kwa kauli ya huyu msemaji wa CHADEMA (Mh. Pauline) ni kama chama hiki kimekaribiswa sebuleni huko Zanzibar na watakuta tende, chai na halua mezani huku sebule ikiwa imetanda maua ya 'kilua na jasmine'.

CCM - you've been cornered on this one. Na huyo mbunge wa viti maalum (ccm) anayesema wabunge wengi ni vijana, hawajui muungano hivyo wafanyiwe semina, inabidi atambue kuwa zaidi ya 60% ya watanzania wote wana umri chini ya 30! Na Zanzibar ambako muungano ni shubiri kwa sasa takribani 80% ya wakazi wake wana umri chini ya miaka 40! Huu wimbo wa kuwa muungano una faida, ulindwe kwa nguvu zote umekuwa unaimbwa kwa miaka yote lakini sasa watanzania wamekuwa wanataka kuwa na muungano 'shirikishi'.

Hakuna semina, warsha au kikao cha aina yoyote kwa wabunge kinaweza kubadilisha mawazo, mtazamo na madai ya wananchi (Tz Bara & Zanzibar), na CHADEMA, again, wanaonekana kulitambua hili ndio maana wanafanya 'people's politics- bungeni'. CCM have only one option - Zanzibar, to comply with CHADEMA's views or die. In otherwords, CCM hawana option.
Ni kweli mkuu naona hii kama gia ya Chadema kuingilia zanzibar maana CDM walikuwa hawana kipya cha kuwaambia wazanzibari sasa wamepata kitu cha kuwaambia kuwa tutawapa serikali yenu kitu ambacho wazanzibari wengi wanakihitaji na CCM haina ubavu wa kusema hivyo.
 
Sioni faida ya Muungano zaidi ya ukurusedi. Jee huu muungano una faida gani kwa nchi? Mimi naona kwa kubaki na Muungano linalofaidika ni kanisa tu.
 
Sioni faida ya Muungano zaidi ukurusedi. Jee huu muungano una faida gani kwa nchi? Mimi naona kwa kubaki na Muungano linalofaidika ni kanisa tu.

If that is the case, kwa nini viongozi wa juu serikalini ambao ni Waislamu hawapigii kelele muungano uvunjwe? Just curious...
 
Sioni mantiki ya serikali tatu. Ofisi ya rais wa serikali ya muungano itakuwa bara au visiwani? Na huyo rais wa serikali ya muungano mbali na masuala ya usalama (wakati jeshi kubwa liko chini ya rais wa serikali ya Tanganyika) na mahusiano na nchi za kigeni, atakuwa anafanya kazi gani? Kama hatuwezi kuwa na serikali moja na kama kuna kasoro na utaratibu huu wa serikali mbili basi kila mtu aende zake. Sisi wabara itatupunguzia gharama zisizo na tija.
 
ni nini kinachokataliwa, muungano, kama unavunjwa uvunjwe tu, hii ya serikali tatu ni bado still muungano, na hiwe zanzibar kivyake na bara kivyake.wabunge wanaotoka zenji ni lazima watetee muungano, chenji wanayovuta ni kubwa, sifikirii kama wanaweza kupata ata nusu ya hiyo chenji kama muungano hautakuwepo.
 
Serikali moja ndo inafaa na ndo ilikuwa iwe hivyo, ingawa kuna hotuba ya Mzee Karume akifananisha muungano na koti na ukiona linakubana unalitupilia mbali. Tulicho nacho sasa ni Serikali tatu ila sisi hatujui tu au tunachagua kuto kujua, mfano haingii akilini kuwa na wabunge utitili kutoka Zanzbar ndani ya bunge la muungano wakati hata siku moja sijasikia rais wa muungano anaalikwa kwenye vikao vya Baraza la wawakilishi!
United state na ukubwa wake wakitaka umoja wa mataifa ina kiti kimoja tu ,hujui hilo ? Comoros na udogo wake kile kisiwa kina kiti kimoja tu katika umoja wa mataifa.

Hapa tulitakuwa katika bunge la muungano kuwe na wakilishi wachache tu,sio hao 300 na 60 kutoka zanzibar,ilikuwa tanganyika iwepo ili mujadili mambo yenu,na katiba bunge la muungano muteuwe aidha mawaziri wenu ndio washiriki katika bunge la muungano na sisi kutoa mawaziri wetu kuingia katika bunge hilo ingelikuwa ni mfumo mzuri sana na tungewiana kwa number.
 
Sioni mantiki ya serikali tatu. Ofisi ya rais wa serikali ya muungano itakuwa bara au visiwani? Na huyo rais wa serikali ya muungano mbali na masuala ya usalama (wakati jeshi kubwa liko chini ya rais wa serikali ya Tanganyika) na mahusiano na nchi za kigeni, atakuwa anafanya kazi gani? Kama hatuwezi kuwa na serikali moja na kama kuna kasoro na utaratibu huu wa serikali mbili basi kila mtu aende zake. Sisi wabara itatupunguzia gharama zisizo na tija.
Wataka bunge tujenge chumbe ?
 
ni nini kinachokataliwa, muungano, kama unavunjwa uvunjwe tu, hii ya serikali tatu ni bado still muungano, na hiwe zanzibar kivyake na bara kivyake.wabunge wanaotoka zenji ni lazima watetee muungano, chenji wanayovuta ni kubwa, sifikirii kama wanaweza kupata ata nusu ya hiyo chenji kama muungano hautakuwepo.
Selikari tatu ya nini na ninyi Chadema.jengeni tabia ya kuuliza wanachama wenu wanataka nini.Serikali ya tatu ni kero tupu. Acha Zanzibar waende zao, tuache debate za muungano tujenge Tanganyika yetu na Zanzibar wajenge nchi yao tuonyeshane heshima kwenye ushindani
 
[h=1][/h]Written by ukreina // 07/07/2011 // Habari // 13 Comments

Na Restuta James
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imependekeza kuundwa kwa serikali tatu; ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar, ili kuondoa hisia za upande mmoja wa Muungano kunyonywa pamoja na mambo yanayoonekana ni kero.
Pia imependekeza mafuta ya Zanzibar yaamuliwe na wananchi wa visiwa hivyo kwa kuwa vina rasilimali chache.
Waziri Nchi Kivuli, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Pauline Gekul, aliliambia Bunge jana kuwa kuundwa kwa serikali tatu kutaondoa kero za Muungano na kuufanya uwe endelevu kwa maslahi ya wananchi wa pande zote.
“Ni vyema serikali ikazingatia umuhimu wa kuwapo serikali tatu kwenye mchakato wa Katiba mpya…suala la mafuta liachwe mikononi mwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwa visiwa hivi vina rasilimali chache sana za kiuchumi,” alisema Gekul.
Alisema ili kudumisha Muungano, serikali inapaswa kujenga utamaduni wa kuitisha mikutano maalum ya kikatiba kati ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ili wawakilishi waweze kujadili masuala yanayohusu uhusiano wao.
“Pia tunashauri kuwapo kwa kikao cha pamoja cha uongozi wa ngazi ya taifa kutoka pande zote za Muungano,” alisema Gekul.
Kambi hiyo imependekeza uanzishwaji wa Mahakama ya Muungano ya Katiba itakayosuluhisha malalamiko yanayohusu Muungano.
“Masuala ya rasilimali nyingine yatajadiliwa ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na rasilimali za Tanzania na inatoa mchango wake sahihi katika uchumi wa taifa,” alisema Gekul.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia walishauri serikali iwachukulie hatua watumishi wanaoonekana kuchangia kero za Muungano.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alishauri kwamba kuna haja ya wabunge kupewa semina na ili wauelewe Muungano kwa kuwa asilimia 55, ni vijana ambao hawauelewi vizuri.
Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wamekuwa wakitaka Muungano uvunjwe bila kuelewa athari au sababu za kuwepo kwake, kwa kuwa michango yao mingi imekuwa ni ya kusoma au kusikia.
Alisema inashangaza kusikia baadhi ya wabunge wakieleza kwamba Zanzibar imemezwa na serikali ya Muungano wakati ndani ya Bunge wapo wabunge wanaotoka Zanzibar kupitia Muungano.
“Wengine wanasema Zanzibar imemezwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania wakati hata mimi leo ni mbunge kutokana na Muungano huo sasa tumemezwa wapi na mimi natokea Zanzibar,” alisema.
Mbunge huyo alisema Muungano una manufaa kwa Watanzania wote na kwamba, unapaswa kulindwa kwa nguvu na gharama yoyote.
Alisema wanaobeza Muungano wanamkatisha tamaa Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuhakikisha Muungano unadumu.
Mbunge wa Wete (CUF), Ali Mbarouk, alisema kuna kero ndogondogo za Muungano, ambazo zimeingizwa kwenye kamati inayozishughulikia na kuchukua mchakato mrefu bila sababu za msingi.
Alisema inashangaza kuona kero kama ya kutoza ushuru bidhaa zinazotoka upande mmoja wa Muungano kwenda upande mwingine.
Mbunge wa Meatu (Chadema), Meshack Opurukwa, alisema serikali tatu ndilo jibu pekee la kuondoa kero za Muungano zilizopo.
Alisema nia ni kuhakikisha kuwa serikali ya Muungano itakuwa na jukumu la kutatua matatizo ya serikali zote mbili.
Opurukwa alisema masuala kama kodi, umeme na rasilimali, yataweza kutatuliwa na serikali husika na iwapo kutakuwapo kero yoyote, itashughulikiwa na serikali ya Muungano.
Awali, Waziri wa wizara hiyo, Samia Hassan Suluhu, alisema serikali imekuwa ikishughulikia kero za Muungano na kwamba, jukumu hilo ni endelevu hadi zitakapokwisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom