Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,777
Leo nimeona "live" katika bunge wakati wa majumuisho ya bajeti ya Wizara ya fedha, kuna mbunge (sikumbuki jina) alisimama kumtetea mtu wa jimboni kwake kuwa alidhulumiwa wakati wa "uhujumu uchumi" na amekuwa anahangaishwa kulipwa madai yake na mwisho akaambiwa amechelewa. Mbunge huyo alisema kama kuchelewa alikuwa hajachelewa kwani anadai siku zote na ushahidi upo. Ndipo aliposimama Naibu Waziri wa Fedha na kumtaka huyo mbunge kuwa awasilishe madai yake yote kwake na karatasi zake zote na anaahidi kushughulikia hilo na kuhakikisha haki inapatikana kwani ni kweli wengi walidhulumiwa wakati wa (operesheni) ya Uhujumu Uchumi.

Ikumbukwe kuwa hii operesheni ilifanyika wakati marehemu Nyerere akiwa Rais na marehemu Sokoine akiwa Waziri Mkuu.

Huyo mbunge alisema kuwa wapo pia waliolipwa kwa kuonekana kweli walidhulumiwa.

Sasa nnajiuliza, na tusichangie hili kwa jazba, Ikiwa serikali inakiri tena bungeni, watu walidhulumiwa, jee ni hatua gani wale waliodhulumiwa wazee ambao wameshakufa ili kudai haki zao, si kurudishiwa tu mali zao na hukumu ipi "posthumous" inayoweza kutolewa kwa waliodhulumu?

Tukumbuke watu walidhulumiwa si katika uhujumu uchumi tu, kama Serikali ilivyokiri leo bungeni bali pia kuna watu waliodhulumiwa wakati wa Azimio la Arusha. Nao wakati wa Mwinyi waliambiwa wakadai lakini kwa kuwa haikutangazwa sana wengine walipoenda wakaambiwa wamechelewa, hivi haki ya mtu kweli ina kuchelewa katika kuidai?

Kwanza nnaisifu sana Serikali ya awamu hii kwa kukiri hilo bungeni "live" kuwa kweli kuna dhuluma ilitendeka. Kwa hakika Serikali kukiri hilo kosa ni ujasiri mkubwa sana na ni njia nzuri sana ya wananchi waliodhulumiwa kuweza kurudisha imani kwa Serikali yao na sasa wapokelewe na kurudishiwa mali zao na kusiwe na hili suala la kuchelewa.

Naipongeza Serikali kwa hilo, na lisiishie hapo watutangazie tuanzie wapi? Kwani nnaamini si wengi waliosikia hilo bungeni kwani si wengi wanaotazama bunge.

Nawaomba na waandishi wa habari walitangaze hili, kwani ni jambo la kheri kubwa sana, hakuna dua inayopokelewa haraka kama ya mwenye kudhulumiwa, pengine haya majanga yote yanayotupata Tanzania ni kwa hizo dhuluma zilizofanywa na viongozi wetu huko nyuma, ni wakati muafaka Serikali kukiri hilo na kuanza kufanya toba na kurudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Hansard zitakuwa zipo kwa wanaotaka kuelewa zaidi.

Ahsante Serikali kwa kuliweka wazi hilo.
 
DHULUMA ZINGINE PIA ZIFIDIWE, DHULUMA ILIYOTENDEKA ZANZIBAR mwaka 1995 na mwaka 2000 Nazo ziangaliwe Upya zisiwe tu za kuhujumu Uchumi. Hata Kuhujumu Haki ya Mpiga Kura wa zanzibar lazima ifidiwe.

Hilo nalo neno, tunataka nchi isiyodhulumu raia wake, na ikiwa leo wamekiri hili nililoandika nadhani na hayo uyaletayo ukiyawakilisha kwa mbunge wako kwa ushahidi kama alivyofanya huyo aliyetetewa na mbunge wake leo bungeni utakuwa umefanya la maana sana katika kupigania haki.
 
Nimeisoma Vizuri sana

Naona umeielewa mada na wala si mimi "na Nyerere", mimi nimewasilisha tu hapa na kukumbushia kwa waliokuwa hawapo kuwa huo wakati wa "Uhujumu Uchumi" ulioongelewa bungeni ulikuwa ni wakati wa uongozi upi.
 
Naona umeielewa mada na wala si mimi "na Nyerere", mimi nimewasilisha tu hapa na kukumbushia kwa waliokuwa hawapo kuwa huo wakati wa "Uhujumu Uchumi" ulioongelewa bungeni ulikuwa ni wakati wa uongozi upi.

Tuko pamoja kabisaaa mkuu!!
 
Mambo kama haya mimi huwa sipo!

Mimi nimelisikia hilo bungeni na nnahisi kukiri hilo kwa Serikali na kuwa tayari imewalipa wengine waliodhulumiwa na bado kuwa na nia kuendelea kuwasikiliza na kuwalipa wengine wenye madai kama hayo ni jambo la maana sana kwa upande wa Serikali.

Inabidi tuwape pongezi.
 
Mimi nimelisikia hilo bungeni na nnahisi kukiri hilo kwa Serikali na kuwa tayari imewalipa wengine waliodhulumiwa na bado kuwa na nia kuendelea kuwasikiliza na kuwalipa wengine wenye madai kama hayo ni jambo la maana sana kwa upande wa Serikali.

Inabidi tuwape pongezi.
Sheria ya Economic sabotage na Organized crimes ilirekebishwa na A. H. Mwinyi 1989.
Sina uhakika, ila if not found guilty mali iliyotaifishwa itarudishwa kwa mwenyewe.

IGP ataandika notice, na baada ya muda Fulani usipojitokeza itakuwa kama ume-abscond. Time frame sijui ila inaweza ikawa kama ya mirathi (90days?).

Kuhusu azimio la Arusha, wachache walipata nyumba zao, nakumbuka kina Bibi Titi wakatukimbia kabisa uswahilini, alikuwa anajua sana kutengeneza togwa na bwimbwi.
 
Sheria ya Economic sabotage na Organized crimes ilirekebishwa na A. H. Mwinyi 1989.
Sina uhakika, ila if not found guilty mali iliyotaifishwa itarudishwa kwa mwenyewe.

IGP ataandika notice, na baada ya muda Fulani usipojitokeza itakuwa kama ume-abscond. Time frame sijui ila inaweza ikawa kama ya mirathi (90days?).

Kuhusu azimio la Arusha, wachache walipata nyumba zao, nakumbuka kina Bibi Titi wakatukimbia kabisa uswahilini, alikuwa anajua sana kutengeneza togwa na bwimbwi.

Leo waziri kasema zipelekwe karatasi za huyo aliyetetewa na mbunge na pia kama kuna wengine waende.

Ni jambo jema hilo.

90 Days ni kidogo sana, wengine wamekufa waliobaki ni warithi, nope, ni ndogo sana. Na kama ni hivyo usemavyo ni sawa (ingawa hauna uhakika) basi iondolewe hiyo sheria ya 90 days, wengine hawakuwepo nchini na wana haki zao.
 
Jee, UKAWA ikitokea bahati mbaya mkachukuwa nchi mtaendeleza hili la kurudishia watu mali zao walizodhulumiwa?
 
FaizaFoxy

Samahani jamani,huko mirembe mmewahesabu vizuri wapo wote?isijekuwa kuna mmoja kachoropoka yuko huku anapiga bla bla,wanafiki utawajua tu.leo hii miaka kadhaa ndo wanajifanya kukiri bungeni,ili waonekane wema kwa watu.mbona hawakiri epa,escro,meremeta,kagoda etc?kwanini wasikiri kuwa wizi wao umesababisha watanzania wanaishi kwa tabu?
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy

a classic case of selective outrage. dhuluma kila kukicha watu wanapigwa risasi(death penalty)wakiandamana kwa kosa ambalo kama wangekamatwa fine yake shs.15,000 under section iv of civil case on public disobedience.
 
Last edited by a moderator:
Dhulumma za Escrow, EPA, Kagoda and the likes ambazo zipo dhahiri na tumedhulumiwa watanzania wote sijui zitalipwa lini?
Ndiyo maana hawataachia nchi kirahisi maana malipo yake wanayajua. Ndiyo hizo hela wanatukania watu mitaani na kujibu ovyo.
 
a classic case of selective outrage. dhuluma kila kukicha watu wanapigwa risasi(death penalty)wakiandamana kwa kosa ambalo kama wangekamatwa fine yake shs.15,000 under section iv of civil case on public disobedience.

Why selective?

Huyo mbunge alikuwa anamtetea mtu bungeni alidhulumiwa wakati huo. Na waziri kakiri kweli dhuluma ilifanyika, sasa nini usichokielewa hapo hata utake kubadilisha mada?

Inauma?
 
Kwa sababu Nyerere alishakufa, mimi nashauri adhabu wapewe watoto zake, Hao Akina Makongoro si wapo badala ya kuwa rais apewe adhabu kwa niaba ya baba yake.

Nafikiri faiza utakuwa umefurahi.

Mtu alishakufa hawezi kubadilisha chochote wala kujibu chochote.
Huyu mwenzenu anayeshindwa kudhibiti ufisadi Hana tatizo kwa sababu ni ndugu Katika Imani.
 
Kuna unalolitaka bibiye si hili la dhulma.....

Jee, hauoni kuwa Serikali imefanya la maana sana kukiri waziwazi kuwa wako kweli waliodhulumiwa wakati wa uhujumu uchumi na huyo Mzee Rage ni mmoja wapo. allitwajwa kwa jina. Alidhulimiwa million 85 za wakati huo, za leo ngapi?

Tunamsifu sana Waziri kukiri hilo na kusema atalishugulikia na kama kuna wengine wana madai wakamuone.

Tunashangazwa sana habari muhimu kama hiyo, ambayo ilikuwa inatakiwa vyombo vya habari viipe kipaumbele, lakini cha ajabu, sijaona hata chombo kimoja cha habari kikirudia hayo, si magazeti, si kwenye TV wala redio ili kuwe na chance kubwa zaidi ya waliodhulumiwa wasikie na wakadai fidia zao. Kulikoni?
 
Back
Top Bottom