Bungeni Leo: Juni 29, 2012

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
12,013
10,169
Ndugu Lukuvi anawasilisha hoja ya serikali kufanya mazungumzo na NSSF ili wajenge ofisi ya kila mbunge jimboni na ameinda zaidi kwa kusema mbunge ni taasisi hivyo kuna haja ya kila mbunge awe na wasaidizi wake wanne ambapo serikali inategemea kuajiri mwaka huu wa fedha kilichonishangaza pale aliposema wataajiriwa kwa matakwa ya mbunge.

Hoja yangu wabunge wenyewe hawapo ktk majimbo yao pia kama suala ni la ofisi si apewe nafasi katika halmashauri husika ili awe karibu na halmashauri ya wilaya kwa kuhoji utendaji wa serikali ya mitaa.

Kuhusu kuajiri wafanyakazi wanne wa mbunge, kila kata ina diwani ambae ni mwakilishi wa wananchi katika kata husika hivyo kwanini kusiwe na utaratibu wa kuangalia shida hizi za wananchi kama team kuanzia kwa madiwani pia mbunge akipata nafasi anakwenda kusikiliza wananchi, naomba kuwakilisha ndugu wana JF.
 
Tuna wabunge kama sikosei ni 357 kama kila mbunge atakuwa na wasaidizi 4, basi 357 x 4= 1,428. Hii ndiyo idadi watu watakoingia kwenye payroll ya serikali. Jumlisha sasa na gharama za office kwa kila mbunge. Then turudi kwenye hali halisi:

1. Nchi ambayo wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda kimoja na wengine chini, wasaidizi 4 kwa mbunge watasaidia nini?

2. Serikali ina uwezo wa kuwapa chochote (hongo?) wabunge lakini likifika swala la kulipa watu wanaokoa maisha ya raia inasema haina fedha!

3. Watoto wanakalia mawe, ndoo, vitabu hakuna, vyumba vya madarasa havitoshi serikali inaona kipaumbele ni office za wabunge?

4. Kuna shule zingine zina mwalim mmoja tu - wabunge ndio priority?

Hivi vipaumbele vya serikali ya CCM ni vipi? Nchi yoyote isiyowekeza kwa watu wake (rasilimali watu) inajitakia balaa. Nchi jirani zinakazana kuwekeza kwa watoto na umma kwa jumla, elimu bora, huduma nzuri za afya, hapa serikali ya CCM inaona ingelee kuwafurahisha wabunge ili waendelee kupiga makofi na kupitisha bajeti za kipuuzi zinazoishia kwenye mifuko ya wachache.

Kama kweli serikali itaanza kujenga office za bunge kabla ya kumaliza kadhia ya nyumba za walimu nchi nzima, basi walimu wanayo haki ya kuandamana. Huu ni upuuzi.
 
Wasaidizi wenyewe ni hawa:

  1. Dereva
  2. Mpiga chapa
  3. Karani
  4. Mhudumu wa ofisi
 
This is Hilarious

tangu 1961 mpaka sasa tumekuwa na wabunge
wabunge wametekeleza majukumu yao
51 years later ndio tunaleta wasaidizi?
who initiated this?

NI UKWELI?????
 
Mpiga chapa na karani? Kati ya dawa za kuokoa maisha au madawati na mpiga chapa kipi muhimu?

Kwenye sekta binafsi mhudumu wa ofisi huwa anafanya kazi zote hizi za mpiga chapa na karani pamoja na ya uhudumu na hakuna workload yoyote pia na mbunge awe wa kisasa angalau na laptop ya kufanya kazi zake sio utamaduni waliozoea wa kuandika kwa mkono alafu unampa mpiga chapa kisha una-print karatasi kwa ajili ya editing (hapa unapoteza muda na karatasi wakati nguvu iliyotumika kuandika kwa mkono ni kubwa kuliko kama kazi zingine wangekuwa wanachapa wenyewe kwenye laptop), dereva tena wakati kila baada ya uchaguzi mbunge anapewa gari lake dereva wa nini tena wakati gari alilopewa mbunge ni moja na amekopeshwa, hapo ina maana kutakuwa na gari lingine.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mbunge Wa vitimaalum mkoa Wa katavi Anna merystela Malac amemlipua pinda baada ya kuona amejisahaujimboni kwake,Mwenyewe ajitetea bungeni
 
hili jambo serikali ifikilie mara 2 miaka yote hiyo hakunaga hizo mambo ndio ije kuwa leo
 
Naona viti vingi vipo wazi...inaniuma sana kutowaona tulikowatuma...!afadhari angekua mmoja..ila duh mpaka haibu..bora tulivunje tu bunge lenyewe..tunawapa bure tu kodi zetu...!
Namuona Mh Pinda...sioni kama anatoa majibu...!
"Vox populi,Vox dei"
 
Ni kweli kabisa.

Hivi ni wapi kunaweza kupatikana idadi ya wabunge wanaohudhuria kikaoa ikawekwa wazi magazetini walau tukaanzia hapo. Ikiwa hivyo watashtuka na kuikwepa hii absence kwa execuuse mbalimbali.
 
Kwa nini tusiitafutie MUWEKEZAJI awekeze hapo?Labda atatusaidia hata kufikiri kwa manufaa kuliko walioko kwa sasa!:A S cry:
 
Mbunge Wa vitimaalum mkoa Wa katavi Anna merystela Malac amemlipua pinda baada ya kuona amejisahaujimboni kwake,Mwenyewe ajitetea bungeni
Hii mada ungeweka kwenye status yako ya Facebook ili kutupunguzia gharama ya intaneti(MB) kusoma hii kitu.
 
jamani nitakwenda kwa kagame anikodishe zile silaha smg tuwape machinga tuanze kuchapana pale mjengoni dodoma hawa washenzi hawasikii dawa ni hii tu
 
Mhe Lukuvi na Serikali yako mmechumsha katika hili, Watumishi wote hao wa nini, Mbunge pekee yake anatosha ,
Hayo ni Matumizi mabaya ya fedha za Wananchi
 
Tuna wabunge kama sikosei ni 357 kama kila mbunge atakuwa na wasaidizi 4, basi 357 x 4= 1,428. Hii ndiyo idadi watu watakoingia kwenye payroll ya serikali. Jumlisha sasa na gharama za office kwa kila mbunge. Then turudi kwenye hali halisi:

1. Nchi ambayo wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda kimoja na wengine chini, wasaidizi 4 kwa mbunge watasaidia nini?

2. Serikali ina uwezo wa kuwapa chochote (hongo?) wabunge lakini likifika swala la kulipa watu wanaokoa maisha ya raia inasema haina fedha!

3. Watoto wanakalia mawe, ndoo, vitabu hakuna, vyumba vya madarasa havitoshi serikali inaona kipaumbele ni office za wabunge?

4. Kuna shule zingine zina mwalim mmoja tu - wabunge ndio priority?

Hivi vipaumbele vya serikali ya CCM ni vipi? Nchi yoyote isiyowekeza kwa watu wake (rasilimali watu) inajitakia balaa. Nchi jirani zinakazana kuwekeza kwa watoto na umma kwa jumla, elimu bora, huduma nzuri za afya, hapa serikali ya CCM inaona ingelee kuwafurahisha wabunge ili waendelee kupiga makofi na kupitisha bajeti za kipuuzi zinazoishia kwenye mifuko ya wachache.

Kama kweli serikali itaanza kujenga office za bunge kabla ya kumaliza kadhia ya nyumba za walimu nchi nzima, basi walimu wanayo haki ya kuandamana. Huu ni upuuzi.

Halafu kwenye mambo ya anasa za wabunge huwa hakuna upinzani bungeni,wote wanakuwa chama kimoja.Kwaweli nguvu ya hoja ya ziada inahitajika kunishawishi nirudishe imani na Siasa uchwara ya bongo.

SWALI:Samahani mkuu,hao wabunge 357 nadhani 102 ni viti maalum ambao hawana majimbo so sidhani kama hao wafanyakazi wa4 wanawahusu wao lakini bahati mbaya sikusikiliza bunge leo wamesema hadi viti maalumu(a.k.a wapiga vigeregere) wanapewa wasaidizi wa4?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kuna uhuni unaendelea bungeni. Spika, kwa ubunifu wa hali ya juu ameondoa kipengele kinachoruhusu mbunge kuuliza mara mbili wakati wa kupitisha vifungu vya bajeti. Kwa maana hiyo kama mbunge alikuwa na kero, serikali ikatoa maelezo lakini hayakutosha au sio sahihi basi hapewi nafasi ya kuuliza tena tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Nimesema huu ni ubunifu wa spika maana kwa sasa yule mama anafanya udikteta wa hali ya juu.
 
This is Hilarious

tangu 1961 mpaka sasa tumekuwa na wabunge
wabunge wametekeleza majukumu yao
51 years later ndio tunaleta wasaidizi?
who initiated this?

NI UKWELI?????

Muulize lukuvi akwambie vipaumbele vya serikali yake ni nini??

Leo Hospitali ya Bombo wamemwambia mgonjwa aliyesagwa miguu na Semi trailer aende hospital ya private akapige XRay kwasababu ya pale hospital imeharibika!!

CCM ni wapuuzi wakubwa!!
 
Back
Top Bottom