Bungeni kumewaka moto-mgomo wa madaktari

Bi kiroboto kama hataki mwongozo aseme tu hakuna mwongozo. Analalamika nini? Eti hakuna cha kumwongoza mtu hapa wala taarifa. Huyu mama vipi? Naona kaja kala pilipili anasura ya ukali hasa.
 
Mh! zambi Anaomba muongozo wa spika juu ya mgomo wa madaktari bingwa na kumtaka spika aruhusu mjadala wa dharura. Anatoa hoja na kutaka wabunge wengine wamuunge mkono. Wanainuka baadhi yao. Mara spika anawaamuru wakae chini na kusema kwa ukali kua hawezi kuruhusu mjadala kwa kua kamati iliyoundwa bado iko kazini. Anainuka mbuge mwingine kuomba muongozo na anajibiwa kua hakuna mwongozo. Mwingine anainuka na kutaka kutoa taarifa. Na yeye anaambiwa kwa ukali kua hakuna cha taarifa. Spika anasema tunaendelea na ratiba! Duu leo bibi kachachamaa!
 
Jamani kwanini Bunge lisimame wakati kamati yake ya huduma za jamii inalishughulikia suala hilo? Kwanini wabunge wasiwe na subra kusubiri majibu ya kamati?

Labda tujiulize wanataka kujadili nini kuhusu kadhia hiyo? au wanataka wavute muda na kuongeza posho.

Tafadhali wa Tz mnatakiwa kujua muda ni mali sana.

Nawapa pole wale wanaoshabikia issue hii ya mgomo.
 
Kwake yeye huyu Spika suala la watu kukosa huduma ya afya sio la msingi. Unafika mahali unashindwa kuelewa kama kweli huyu ni binadamu wa kawaida au la? Inatia kinyaa!!!

Tiba
 
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda anaendelea kuliendesha bunge kwa udikteta wa hali ya juu!.

Mfano ni leo Mbunge Zambi kaomba muongozo wa spika kuhusu jambo la dharura la mgomo wa madaktari bingwa!.
Hoja hiyo ikaungwa mkono na wabunge kadhaa lakini spika Makinda sio tuu akaizima, bali pia akagoma kupokea hoja yoyote wala taarifa yoyote!.

Hivi ni kweli kwa mujibu wa kanuni, spika ana uwezo wa kuzuia mbunge asitoe muongozo ? au zinamtaka spika kwanza asikilize huo muongozo au taarifa ndipo atoe uamuzi?!.

Udikteta kama huu unavumilika vipi huko bungeni huku jumba hilo limesheheni wanasheria mahiri lukuki?!.

Wanamwachiaje spika kuliendesha bunge kwa kadri anavyojisikia, wakati bunge linaendeshwa kwa kanuni na sio feelings na imotions?!.

Pasco.
 
viongozi wenu wauwaji wakubwa....na wanapenda kubebana sana..huyu makinda ni wa kufukuzia mbali....pinda nae anataa kuondoka haraka....
 
Wabunge wametaka kujadili kuhusu mgomo wa Madaktari, Spika almanusura aongee kikwao kwa Hasira zilivyomganda.
Hakuna mwongozo wala nini, Bunge lichape kazi,
Speaker Oyeeee,

Kama nimekuudhi, Leave me alone
sasa umeferahi nini? ngoja uvunjike mfupa tuone nan i atakutibu. kumbuka Mungu ndie anapanga hakuna anayeomba kuumwa
 
Makinda hataki mwongozo wala taharifa

Nashangaa wabunge wengi walisimama kuunga mkono hoja, yeye akawakalisha, akatema pumba ...wengine wakagumia mwongozo na taarifa...yeye kakaza kasema ashaamua hamna mwongozo na bunge liendelee kama kawaida
 
hili swala la mgomo sii zuri lakini inaonekana viongozi wa nchi yenu hawana moyo wa dhali kumaliza tatizo hili.......waondoeni madarakani haraka
 
jamani hivi hili litakwepwa mpaka lini? japo nimeona spika ametoa hoja yenye mashiko kidogo kuwa wabunge wasubiri kamati itakuja na nini kutoka kwa madaktari. maana wana kikao leo. japo kwa mtazamo wangu kama serikali haitaki kutoa kauli rasmi basi bunge lijadili na kutoa msimamo, maana kauli ya wabunge ndio ya watanzania
 
Hata kama anajiona kuwa yeye si wa daraja la kutibiwa katika hospitali zetu hapa TZ, Je hana ndugu wanaomhusu ambao wanatibiwa hapa TZ?
 
Tafadhari naomba mtujuze kinachoendelea......

Kuna Mbunge amesimama na kunukuu vifungu na pia taarifa ya habari na mazungumzo yake na wafanyakazi Wa Muhimbili kuwa madaktari bingwa wamegoma na wagonjwa wakitolewa wodini. Amelitaka bunge kuahirisha shughuli zote za Leo na kujadili Hali tete ya afya za watanzania. Wabunge wote walisimama kuunga mkono, Mh spika a.k. a Bi Kiroboto akawaamuru waliosimama, kaa chini! Ikasikika
Sauti kuomba mwongozo akakataa, nyingine ikisema taarifa, akakataa na kumuita Ngeleja aanze kutoa hoja ya gas issue huku wabunge wakitoka nje mmoja baada ya mwingine
 
amekataa kumpa nafasi Mnyika kuomba mwongozo na kutoa taarifa.
Sura imemshuka huyu bibi utadhan kamwagiwa tindikali

Kukataa madai ya mwongozo ama taarifa sio kuvunja kanuni? Tumngoje Tundu Lissu lazima ataliibua tena. Bi Kiroboto amevunja kanuni za bunge.
 
Nashangaa wabunge wengi walisimama kuunga mkono hoja, yeye akawakalisha, akatema pumba ...wengine wakagumia mwongozo na taarifa...yeye kakaza kasema ashaamua hamna mwongozo na bunge liendelee kama kawaida


huo ndo ujinga mkubwa.......huyo mama hastahili kuwa hapo.........
 
Back
Top Bottom