Bungeni: Kigwangalla amfundisha Mbowe hekima

Bungeni: Kigwangalla amfundisha Mbowe hekima

Mhe Kigwangala ambae ni mbunge wa jimbo la Nzega amemtaka Mbowe kuacha kuongea kauli tata kwani yeye ni kiongozi na maneno ya viongozi ni yenye kuaminiwa na watu.

Kwa mantiki hiyo, amemtaka Mbowe kuwa makini sana
Na yeye aache kuandika barua tata, na awe makini vilevile mtu mzima kushindwa hata kuandika barua, hizo Masters zake ni nini kama hazimsaidii hata kuandika barua

nawawasiwasi kama wewe uko vizuri upstairs. Subirini muda mwafaka video atakapowekwa hapa mmtatafutana wewe na wenzio.

Mkuu video tayari imeshawekwa mitandaoni,wameaachwa uchi mchana kweupe!ila hiyo video inasikitisha,inatia simanzi,inatia hasira kubwa na chuki dhidi ya watawala wetu!sidhani kama tutafika salama!wanadai bomu limetoka china na ni jipya,hivi baada ya Lwakatare kukamatwa na polisi na kuwekwa mahabusu kwa ushaidi wa youtube,mnakumbuka kua Mwigulu Nchemba(LAMECK) alikwenda China kusoma week moja?ni course gani ya week moja aliyokwenda kuisoma?je sio yeye aliyerudi na bomu ilo!siku zao zinakaribia,Mwl Nyerere aliwahi sema "itafika wakati watu watachagua kifo kuliko fedhea,na ole wao watakaosababisha siku hiyo ifike" naona sasa wanataka kulazimisha siku hiyo ifike!

Ni nani aliyemwambia Kigwangwala kwamba Mhe.Mbowe alikuwa jukwaani bomu lilipokuwa linarushwa? Na wewe mleta mada umeajiriwa kushinda JF, umepata taarifa ya nani kwamba Mhe.Mbowe alikuwa jukwaani? Acheni kukurupuka kama kuku aliyekatwa kichwa!

Vp kauli ya Nape kaichambua vp?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

By HAMY-D

Akiwa ana changia, Mhe Kigwangala ambae ni mbunge wa jimbo la Nzega amemtaka Mbowe kuacha kuongea kauli tata kwani yeye ni kiongozi na maneno ya viongozi ni yenye kuaminiwa na watu.

Kwa mantiki hiyo, amemtaka Mbowe kuwa makini sana na kauli zake, hasa kwenye sakata la mlipuko wa bomu Arusha.

Akiwa ana changia pia akusita ku-challenge kauli ya Mbowe, kwa kusema yafuatayo "Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"

We na huyo vitumbua ni mapimbi, nani alisema bomu lilirushwa nyuma ya jukwaa? ninani alisema mda huo mbowe alikuwa bado jukwaani? Mbowe alikuwa ameshuka kukusanya sadaka....Kwani Nepi Nnauye sio kiongozi? inamana kauli aliyoitoa nepi ni ya ukweli, yeye Nepi hapaswi kuwa makini na kauli zake??? subirini video ije.....
Huyu Kigwangala yuko kama kapigwa ngwala, kama hajui kilichotokea aachane na Mbowe,
Aendelee kuchangia budget, aachane na mambo ya Arusha

Kwake Nzega wazungu wa resolute wamemshinda anadandia gari la A towm nani kamuomba

Akiwa ana changia, Mhe Kigwangala ambae ni mbunge wa jimbo la Nzega amemtaka Mbowe kuacha kuongea kauli tata kwani yeye ni kiongozi na maneno ya viongozi ni yenye kuaminiwa na watu.

Kwa mantiki hiyo, amemtaka Mbowe kuwa makini sana na kauli zake, hasa kwenye sakata la mlipuko wa bomu Arusha.

Akiwa ana changia pia akusita ku-challenge kauli ya Mbowe, kwa kusema yafuatayo "Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"

Mbowe aliposema alierusha bomu tunamjua hakukosea.Hivi kwa akili yako huwezi kufikiri kuwa eneo la mkutano watu walikuwa wakiendeleakurekodi video?Au na wewe akili zako ni sawa na za huyo Kigwangala?.Msitulazimishe wananchi tuishi mtakavyo ninyi watawala.

"Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"
Kigwangala ona hii red, ulijuaje kama bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa???? Mtego unaomtegea Mh. Mbowe umekunasa kabla haujamnasa Mbowe!!!!!!

Akiwa ana changia, Mhe Kigwangala ambae ni mbunge wa jimbo la Nzega amemtaka Mbowe kuacha kuongea kauli tata kwani yeye ni kiongozi na maneno ya viongozi ni yenye kuaminiwa na watu.

Kwa mantiki hiyo, amemtaka Mbowe kuwa makini sana na kauli zake, hasa kwenye sakata la mlipuko wa bomu Arusha.

Akiwa ana changia pia akusita ku-challenge kauli ya Mbowe, kwa kusema yafuatayo "Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"

ukweli siku zote unauuma!! So nategemea kauli kama hizo nyingi tu kutoka kwa wahusika..ikiwezekana nunueni na vipind vya matangazo myaseme hayo..but indeed wanaoumia ni binadamu wenzenu na ipo siku kila mmoja atapokea kadri ya matendo na maneno yake!!

Hii nayo kali Kigwa kapata wapi busara mpaka awe mshauri wa Mbowe.H.kigwa aliye mshauri mwenyekiti wake amuondoe mkuu wa mkoa wa mtwara kwa kuwa ni mkatoliki leo amegeuka kuwa mshauri wa Mbowe.

Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Hamisi bhana ! Haya tumekusikia , Tutamshauri Mh .Rais akuachie tena kiti cha Meza kuu kwenye ziara ya Obama .

Kila dakika, pasco wa Lumumba unamuwaza Mbowe na CHADEMA, naona upo kwenye special payroll ya buku saba mia. Tano eh!

Kigwangala ndo nani tena huyu?AU Ndio yule aliyeiba jina la mtu ili asome?Kihiyo atawezaje kumshauri mtu mwenye hadhi ya Mbowe?Aende ITV wakampatie ile habari walioitoa katika taarifa yao ya habari ya Jumapili saa mbili usiku ili ajue alichozungumza Mbowe na sio kubwatabwata hovyo.

Kingwangwala hana hekima za kumpatia Mbowe, kimsingi anatafuta airtime tu kupitia ishu hii. Wameona bajesti imedoda wanadakia Arusha chezea chadema full coverage Arusha.

Akiwa ana changia, Mhe Kigwangala ambae ni mbunge wa jimbo la Nzega amemtaka Mbowe kuacha kuongea kauli tata kwani yeye ni kiongozi na maneno ya viongozi ni yenye kuaminiwa na watu.

Kwa mantiki hiyo, amemtaka Mbowe kuwa makini sana na kauli zake, hasa kwenye sakata la mlipuko wa bomu Arusha.

Akiwa ana changia pia akusita ku-challenge kauli ya Mbowe, kwa kusema yafuatayo "Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"

Mkuu saa nyingine unakurupuka sana ku post kama Kigwangala anavyobwabwaja. Wewe unashinda humu na unajua kabisa alichosema Mbowe kuwa video walizonazo zinaonyesha kabisa mhusika ni nani. Hili suala la kusema yeye alionaje kama alikuwa jukwaa kuu ni upuuzi.

Suala la kuwa yeye ni kiongozi wa juu hakutakiwa kuongea vile hilo mimi nalikubali pia.

Tuwe objective na balanced tunapotoa mada si ushabiki tu.

Akiwa (Kigwangala) anachangia pia akusita ku-challenge kauli ya Mbowe, kwa kusema yafuatayo "Mbowe amewezaje kumuona mrusha bomu wakati Mbowe alikuwa jukwaa kuu na bomu limerushwa kwa nyuma ya jukwaa?"

Hahaha...mkuu kama huyo jamaa aliyasema hayo basi nina mashaka na uwezo wake wa kuchambua kauli...

Nahudhunika sana herufi nyingi za jina langu kufanana na lake,huyu ni msomi ambae hakupata bahati ya kuelimika pamoja na Nchemba,hawa wana sifa zinazofanana,wote ni wezi wa majina ya watu,Tafadhali Said Bagaile,rudia kutumia jina lako la awali,mbona mwenzako Lameck Madelu ameshaanza mchakato huo kwa kuongeza Lameck kwenye CV yake?

naona wabunge wa ccm bila kuwataja wabunmge wa cdm wanaona hawajachangia kabisa, watu wameachwa peke yao ila bado wanawataja cdm, wamemisi changamoto zao nini? kingwangala simamia kwenye hoja iliyo bungeni, ya arusha waache walioko arusha.

Wewe ulitaka Mbowe akae kimya wakati tunajua kuwa mnatumia propaganda zenu chafu kupandikiza makosa na kukijengea chuki CDM mbele ya jamii. Kwanini asingeanza kuwashauri Kina NAPE, MWIGULU, LUKUVI, PINDA, CHAGINJA na wengine wengi. Wewe subiri muda muafaka utajua huyo mliemtuma akavuruge amani ameshajulikana na kumbukumbu za kutekeleza uhalifu huo zipo. This time tunataka swala hili lisishughulikiwe kienyeji kama lile la marehemu Daudi Mwangosi.

Nahudhunika sana herufi nyingi za jina langu kufanana na lake,huyu ni msomi ambae hakupata bahati ya kuelimika pamoja na Nchemba,hawa wana sifa zinazofanana,wote ni wezi wa majina ya watu,Tafadhali Said Bagaile,rudia kutumia jina lako la awali,mbona mwenzako Lameck Madelu ameshaanza mchakato huo kwa kuongeza Lameck kwenye CV yake?

Hehehe Hawa jamaa inachekesha kuna mwingine ni naibu waziri ametajwa kwenye baed pionners ya fb kuwa anatumia jina si lake kwa kugushi vyeti na sijasikia akikanusha. Hatari kwelikweli.

Back
Top Bottom