Bungeni: Halima Mdee aambiwa anacheza 'mbwa kachoka'

Bungeni: Halima Mdee aambiwa anacheza 'mbwa kachoka'

Naomba ushauri wenu, kwa mambo kama haya tuwaombe maaskofu, wachungaji, mashehe, manabii, mitume nk waendelee kuliombea taifa au tufanyeje?? Please help me!!
 
Mbunge wa Viti Maalumu, Tawhida (CCM) anachangia sasa, anasema Halima Mdee anacheza "mbwa kachoka". Wataalamu wa lugha tusaidieni. NI mwendelezo wa matusi bungeni kutoka chama tawala.
Hebu dadavua aliongea kwenye mkutadha gani?
 
Hebu wenye ukweli wa movie hii, tupeni chanzo cha matusi haya mbungeni hasa katika wakati huu.

Kaongea hayo maneno ila ni watu wameamua tu kupotosha kwa sababu ya njaa zao tu.Anamkataza waziri asijibu hoja za wapinzani cha ajabu na yeye anaongelea hayo hayo then anaunga mkono hoja kwa asilimia 100
 
Naomba ushauri wenu, kwa mambo kama haya tuwaombe maaskofu, wachungaji, mashehe, manabii, mitume nk waendelee kuliombea taifa au tufanyeje?? Please help me!!

Hivi si kuna mtu aliwahi kumulikwa na kamera akinyunyiza unga katika vii vya wabunge! Au ndo kale kadawa kameanza kufanya kazi yaani kana-disconnect ubongo na midomo. Siwezi kuamini yanayondelea zaidi ya hako kadawa.
 
Hakika hapo hakuna spika! Angesema mpinzani angetolewa nje!
 
Siamini huyu mama ajatolewa nje!
 
Mbunge wa Viti Maalumu, Tawhida (CCM) anachangia sasa, anasema Halima Mdee anacheza "mbwa kachoka". Wataalamu wa lugha tusaidieni. NI mwendelezo wa matusi bungeni kutoka chama tawala.
Hayo maneno mh mbunge kayatamka lakini hakumlenga mh Mdee kwa vile alikuwa akiponda taarifa ya kambi ya upinzani kuhusu Muungano! Taarifa ambayo iliwasilishwa na mh Silinde. Mh Mdee aliwasilisha maoni ya mazingira. Mdee aliposimama kuomba muongozi mbunge akasikika akisema anayaondoa maneno! Tuwe makini tunapotoa taarifa jamani
 
Mbunge wa Viti Maalumu, Tawhida (CCM) anachangia sasa, anasema Halima Mdee anacheza "mbwa kachoka". Wataalamu wa lugha tusaidieni. NI mwendelezo wa matusi bungeni kutoka chama tawala.
Nimemuona akiongea...Hana lolote ni type ya mipasho.
 
Kushindwa kwa kila mbunge wa ccm ni K.O ya raundi 3,tuwasaidie wamalize 2015 watuachie nchi yetu kwa amani bila vita
 
Bora wewe stanley umeeleza kilicho jili tofauti na wengine! Hivi kuondoa maneno ni suluhu ya tatizo! Kama kejeli na matusi yapo pale pale, kuomba msamaha na kuondoa maneno kisiwe ni kichaka cha maovu kwani haya maneno ndio chanzo cha vurugu!

Kwenye hili spika anazidi kudhihirisha kuwa ni mtu asiye makini na anatekeleza ukada mule na uchama juu! Nafikiri huyu mama angetolewa nje kama spika alivyo sema three days back ingekuwa fundisho kwa wengine!

Kwa mwendo huu ni kwamba wabunge watkuwa wanatukana alaf wanasema naondoa maneno kwishaa!

Spika hatakiwi kuyumba katika misimamo yake, huyu mama ilibidi aende nje arudi kesho!

Sasa kwenye hili kwa nini wapinzani wasiseme wanaonewa?

Huu ni udhaifu mkubwa wa spika na yeye ni sehemu ya vurugu hizi.
Hayo maneno mh mbunge kayatamka lakini hakumlenga mh Mdee kwa vile alikuwa akiponda taarifa ya kambi ya upinzani kuhusu Muungano! Taarifa ambayo iliwasilishwa na mh Silinde. Mh Mdee aliwasilisha maoni ya mazingira. Mdee aliposimama kuomba muongozi mbunge akasikika akisema anayaondoa maneno! Tuwe makini tunapotoa taarifa jamani
 
Last edited by a moderator:
Nimemsikiliza yule mama mzanzibari, ameongea mipasho tuuuu na taarabu bila hata kujenga hoja,
Kilichonishangaza zaidi anamzuia waziri adijibu hoja za wapinzani, na badala yake wapinzani wakitaka majibu wamfuate yeye,
Inavyoelekea huyo mama hajui hata nafasi na wajibu wake masikini!!, yuko pale kutetea serikali na waxiri wake badala ya kuibana na kuihoji kwa manufaa ya wananchi, anajua kuwa ameingia bungeni ili kupambana na wapinzani. Pole zake!!.
Tupo pamoja mkuu.
 
Mbunge wa Viti Maalumu, Tawhida (CCM) anachangia sasa, anasema Halima Mdee anacheza "mbwa kachoka". Wataalamu wa lugha tusaidieni. NI mwendelezo wa matusi bungeni kutoka chama tawala.

Mbwa kachoka!! Ngoma ya Zanziberi hii!
 
Nauliza swli tena! Hayo maneno yalitamkwa au hayakutamkwa?

* kama haya kutamkwa nini kilitamkwa? Naomba uweke maneno yaliyo tamkwa!

*kama hakumshambulia Halima Mdee alimshambulia nani?

*je hayo maneno yana ruhusiwa bungeni?

kwa hiyo amemshambulia mdee? huna aibu? kwanza mdee alisoma tu haikuwa hoja yake binafsi au mdee hakuwa anachangia. alisoma kwa niaba ya mchungaji msigwa ambaye amepigwa ban na naibu spika. so kom hakumwaattack mdee personal bali alimwomba waziri ajibu hoja za wananchi na si majungu na malalamiko ya kambi ya upinzani
 
Last edited by a moderator:
Prince Hope nimesha wauliza wote wano sema hakutamka hayo maneno waseme maneno yaliyo tamkwa si kupinga tuu!

Naomba waseme maneno gani aliongea huyo mama kinyume na hayo?

Usitumie kigezo cha yeye kuwa verified user kumfundisha WOGA. Hilo tusi la Mbwa kachoka, limetamkwa. Unless ukute ulikuwa unasikiliza kupitia tundu tofauti na yaliopo ktk masikio ya mwanadamu.
 
Last edited by a moderator:
manyerere njaa zako zitakuuwa, hadi unashindwa kusikia anachosema mtu bungeni..ongeza sauti ya tv yako hadi mwisho pengine kelele zitakusaidia kuelewa

Nakiri Manyerere Jackton ana njaa, sio peke yake anayeongozwa na tumbo kwanza kichwa ndio kinafuata. Wapo wengi humu hata Pasco anajua. Lakini nikukumbushe kuwa kwa level ya uzoefu, ujuzi, uweledi wa mambo, hufikii hata robo ya robo ya uwezo alionao Manyerere. So uwe na adabu mdogo wangu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom