Bungeni Dodoma: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai apiga marufuku Wabunge kubandika kope na kucha

Mwisho watasema ni marufuku watu kupiga jeki na kubusti maziwa halikadhalika kuvaa boksa.
Yetu macho!!
 
kukosa maono..serikalini wachache sana hutumia akili zao vizuri,wamelemaa kifikra..kwa kuwa muda mrefu wanatenda kufuata utaratibu uliowekwa..
 
Kwani hawana dressing code? wanawake ukiwaingilia kwenye huo uringo wa kujipodoa unaweza pata tabu sana. Angalau wanaume tunaweza kujizuia kupiga pamba nyepesi na kunyoa kiduku
 
Siamini ninachosoma na sidhani kama ni kweli.

Nchi masikini kama Tanzania , ndani ya Bunge mada ni kucha na Kope! Hiyo ni kazi ya Spika kweli. I mean Spika anazungumzia Kope na Kucha, sijui alianza lini kufikiri na kisha kutafuta ushauri , kufanya kautafiti n.k. Waafrika tuna matatizo makubwa.
 
Hapa ndipo wabunge wanawake walipotakiwa kuonyesha msimamo wao.

Hii kauli ya Spika ni kinyume cha haki zao. Nimebahatika kuisha kwa muda kusini mwa Africa, yaani ukilinganisha wanawake wa kusini na hawa dada zetu utaona ni jinsi gani dada zetu walivyonyuma katika kupigania haki zao. Wanawake wa Kusini wameamuka na wala wasingekubali kuvumilia huu udhalilishaji waliofanyiwa na Spika. Maana kwa kauli ya spika ina maana hao wabunge leo jioni wende saloon kuondoa kope, nyusi na kucha zao ......... kesho waonekane ni different creatures. Kama siyo kuwaabisha na kuwadhalilisha ni nini!!?

Kama leo wanakatazwa kucha na nyusi kesho watakatazwa na nywele zao pendwa za Brazil.

Naandika haya siyo kuwa nawatetea au napenda kucha na kope bandia bali nawashangaa kwa kushindwa kumchallenge spika. Wameanza huko Bungeni kesho watakuja maofisini na keshokutwa mtaani.
 
Hivi amenukuu kifungu gani cha sheria kuzuia hili?haoni kuwa bado anaendeleza utawala DUME ndani ya jamii yetu,tutaona vichekesho vingi sana awamu hii,halafu spika wangu naye anatembelea nchi zingine na kuona wenzetu wanavyojitahidi kuleta usawa wa kijinsia kwenye nchi zao sisi bado tupo kwenye ujima,lini utazuia wabunge wa kiume wasifuge ndevu zao???
 
Uhuru wa haki ya mwanamke wa kitanzania kujiamulia nini anapenda kuvaa na vipi anapenda aonekane UMEKIUKWA...Kila mwanamke anapenda kujipamba na aonekana mzuri,kuwakataza wanawake wasijipambe ni sawa na kuwakatia UHURU wao wa kujiamulia ambao ni haki yake ya kimsingi

Nyusi,kucha za kubandika,Nywele bandia ni kitu cha kawaida kwawanawake kuvitumia hata haowanawake wa nchi zilizoendelea wanatumia sana hivyo vifaa..

Spika angelipiga angelikataza wanawake wanaojichubua kuingia Bungeni,Kwani kujichubua inaleta madhara ya kiafya kwa wanawake
 
Kazi wanayo kufanya ukaguzi. Ila waweza bandika kucha na usijulikane umebandika. Ila sidhani kama ni fair
 
Huu ndio ujumbe wake huko twitter:

Mamlaka ya Spika yanapaswa kuwa na nguvu na uwezo wa kuisimamia serikali katika mambo ya msingi.Mh.Lissu hajawahi kupata hadhi ya ubunge toka aliposhambuliwa kwa risasi.Lakini leo tumeona mamlaka ya spika yakiweza kuwa imara katika vita ya kucha na kope za Wanawake Wabunge.
 
Ataacha kweli kuitwa na kuhojiwa kwenye ile kamati maarufu?

Mpaka sasa hakuna alieomba muongozo wa kiti juu ya ujumbu huu?
 
Tunaacha kujadili mambo ya kututoa kwenye umasikini tunahangaika na upumbavu wa mtu mmoja mmoja
 
Wakuu natanguliza salamu , Baada ya salamu naingia moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kitendo cha Spika wa bunge la Tanzania kuingilia masuala ya urembo wa wanawake na kuamua kupiga marufu wabunge wanawake kujiremba kwa kucha na nyusi bandia, si tu kwamba ni kuingilia uhuru wa akina mama bali ni jambo la kibabe linalorudisha nyuma maendeleo ya viwanda na wala halina tija yoyote ile kwa Taifa.

Ni wivu wa kizamani usiofahamika chanzo chake , Kuzuia matumizi ya nyusi na kucha bandia ni sawa na kuzuia biashara ya vitu hivyo iliyosambaa kila pembe ya nchi na ambayo tayari imelipiwa kodi , jambo hili likiachwa bila kujadiliwa iko siku spika atazuia mitindo ya nywele bungeni na kuamuru wabunge wote wasuke " TWENDE KILIONI au TATU KICHWA "

Wako watu waliopiga hatua za maendeleo kwa kufanya biashara hii ya kuuza kucha , kope na nywele bandia zikiwemo Rasta , Mmoja wa wafanyabiashara hii anaitwa Jokate Mwongelo ambaye juzijuzi juhudi zake hizi zimeheshimika hadi kateuliwa kuwa DC , kuzuia matumizi haya kwa wabunge ni sawa na kuipiga marufuku biashara hii jambo ambalo halina tija yoyote kwa nchi masikini kama yetu , tukiacha jambo hili bila kujadiliwa iko siku tutazuiwa kutumia lotion au perfume na kuamriwa kuogea sabuni mbuni au kodrai .

Kuna haja ya bunge kujikita kwenye kujadili mambo ya maendeleo badala ya kujadili masuala ya urembo ambayo hayatasaidia chochote kwa yeyote .

Naomba kuwasilisha .
 
Back
Top Bottom