Bungeni Dodoma: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai apiga marufuku Wabunge kubandika kope na kucha

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,271
2,000
Kwa haya yanayoendelea hapa bongo,napata picha kamili ya hari ilivyokuwa kipindi cha Adolf Hitler kule ujerumani,au kipindi cha Idi Amin pale UG,
 

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,748
2,000
Hoja ya Kucha na kupe imekaa vizuri sana ni Kwaajili ya Afya zao ni swala mtambuka kwa Maana ya Vifaa Vinavyo tumika na Wahudumu wenyewe Afya zao zikoje Jiulize kazi za kucha zako na kope ni zipi? Mungu alituumba Jinsi tulivyo wewe unafanya ''Modifications'' kwenye Mwili wako''
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,460
2,000
Kama hamkubaliani naye katengueni ama peleka kesi kwa malkia wenu marekani
 

Sandinistas

JF-Expert Member
Jul 5, 2013
2,336
2,000
Kama yule Mbunge wa Zimbabwe, (Fumai?) aliyewatuhumu wanawake kusababisha kuenea kwa UKIMWI kwa kupendeza na kunukia vizuri! Jana hii habari ilikuwa headline kwenye bbc focus on Africa!
 

rubaman

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
4,965
2,000
Haya yote YATAPITA. Nakumbuka walipigaga marufuku wanawake kuvaa Suruali na vikuku. Kuna issues muhimu za kujadili na kubadilishwa Tanzania. Hatusikii huyu mtu akipiga marufuku uvunjwaji wa katiba by viongozi wa CCM, Policcm na wapambe kama yule Mkurya sitaki kumpa time anayejitokeza ktk press kuongea upuuzi wake from time to time. Bunge lijadili mambo muhimu ya kuendeleza nchi sio upuuzi huu.
 

Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,489
2,000
Hizo kucha bandia na kote.. zina uhusiano gani na wao kuingia bungeni na kuketi tu?..duh

Pia kama amepata malalamiko.. ni juu ya nini haswa na kivipi zinasumbua wengine au yeye?
Ni dhahiri pasi na shaka kwamba tumeshapoteza muelekeo kama taifa, wenzetu walioendele siku nyingi wanaweza kutushangaa sana wakisikia Bunge letu linajadili nonsense issues kama hizi, nina wasiwasi Spika atakuwa amewalenga wabunge fulani wa upinzani hapo, tumekalia mambo ya hovyo hovyo tu, Je swala hilo linaweza kuleta mkate mezani ?, Je mbunge akiwa na kope bandia haweza kutoa hoja ya tanzania ya viwanda ?.
 

monongo

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
388
225
Hata Mimi nakubaliana na Job Ndugai maana hawa mama zetu wana matatizo makubwa dhidi ya miili yao na urembo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom