Bungeni Dodoma: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai apiga marufuku Wabunge kubandika kope na kucha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amepiga marufuku wabunge kuingia bungeni wakiwa na kucha za kubandika na kope za kubandika. Spika Ndugai amesema, ataendelea kupokea maoni kuhusu suala la wabunge kuchibua.

====

BUNGENI, DODOMA: WABUNGE WALIOBANDIKA KUCHA NA KOPE MARUFUKU KUINGIA BUNGENI


Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai, amepiga marufuku wabunge wanawake wenye kucha na kope za kubandika wasiingie bungeni.

"Kwa mamlaka niliyopewa, napiga marufuku wabunge waliobandika kucha za bandia na kope za bandia kwamba ni marufuku na hilo la kujipodoa bado najadiliana na wataalam wangu," amesema Spika.

Spika Ndugai alitoa kauli hiyo leo bungeni muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa afya, Dk Faustin Ndugulile kutoa majibu ya madhara makubwa wanayopata wanawake wanaotumia kucha na kope za bandia.

Naibu Waziri alisema takribani wagonjwa 700 hupokelewa kwa mwaka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kumeza vidonge vinavyobadili sura pamoja na vipodozi vyenye kemikali na kuwa watu hao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani na ya ngozi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatuma Toufiq alihoji ni wanawake wangapi wameathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia.
Naibu Waziri alisema kucha na kope za kubandika si vipodozi kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219 inayosimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

"Kwa mujibu wa sheria hiyo, kipodozi ni kitu chochote kinachotumika kwenye mwili au sehemu ya mwili," alisema Dk Ndugulile.
 
Hizo kucha bandia na kote.. zina uhusiano gani na wao kuongia bungeni na kuketi tu?..duh

Pia kama amepata malalamiko.. ni juu ya nini haswa na kivipi zinasumbua wengind au yeye?
Mkiambiwa huu ni utawala wa kidkteta ambao utawala wa sheria unakuwa matamko ya mtu mnakuwa hamkubali, lakini kwa namna hawa viongozi wa awamu hii wanavyoenenda hakuna mtu hatofikiwa, wote hata nyie vichwa maji mtaelewa tu kile watu wenye akili timamu wanakipigie kelele
 
Hizo kucha bandia na kote.. zina uhusiano gani na wao kuongia bungeni na kuketi tu?..duh

Pia kama amepata malalamiko.. ni juu ya nini haswa na kivipi zinasumbua wengind au yeye?
Ikitokea vurumay, hizo kucha zinaweza kutumika kama majambia kuuwa wengine . Nawaza tu .
 
Natamani panga hilo liwahusu hata MaDC.....Mh Kidoti sijui angeficha wapi sura yake 😂😂😂😂😂
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amepiga marufuku wabunge kuingia bungeni wakiwa na kucha za kubandika na kope za kubandika. Spika Ndugai amesema, ataendelea kupokea maoni kuhusu suala la wabunge kuchibua.

====

BUNGENI, DODOMA: WABUNGE WALIOBANDIKA KUCHA NA KOPE MARUFUKU KUINGIA BUNGENI

Spika Job Ndugai amepiga marufuku Wabunge wenye kucha na kope za kubandika kuingia Bungeni huku akiendelea kuchukua maoni ya nini kifanyike kwa Waliojichubua

Ameyasema hayo leo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Faustine Ndugulile kujibu maswali ya nyongeza ya Mbunge Fatma Theofiki aliyeuliza iwapo Serikali inaona umuhimu wa kutoa elimu juu ya kujichubua

Waziri Ndugulile amesema kwa mwaka takribani wagonjwa 700 hupokelewa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kijichubua

Aidha, amesema kuwa watafanya uchunguzi na kuanza kutunza takwimu mbalimbali zitokanazo na kubandika kucha, kope na kujichubua ili wazifanyie kazi

Ameongeza, kwa sasa Wizara kupitia TFDA haina utaratibu wa kuzuia kucha wala kope za kubandika kwa sababu hakuna sheria inayotoa mamlaka hayo
Hadi Kairuki naye amekatazwa?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom