Bunge: Zitto kulipwa mafao yake yote

Bunge: Zitto kulipwa mafao yake yote

najiuliza uhusiano huu mkubwa kati ya CCM na Zitto ulijengeka lini maana mkuu hakuna mtu ambaye ametokea kupata favour kama anayoipata huyu jamaa kutoka kwa uongozi wa CCM
 
Last edited by a moderator:
Aliyekuwa mbunge wa Igunga bwana Rostam Azizi. SASA ni dhahiri kwamba, uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga upo mbioni kufanyika baada ya ofisi ya Spika wa Bunge kupokea rasmi barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz (CCM).

Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake mjini hapa kwamba barua hiyo ya Rostam iliyoandikwa Julai 15 mwaka huu, iliifikia ofisi hiyo Jumanne wiki hii.

Kulingana na Katiba inavyoelekeza kwamba Mbunge atahesabika kuwa si Mbunge tena siku barua ilipopokewa, tangu tarehe Rostam alipotangaza kujiuzulu, alikuwa akihesabiwa kuwa na wadhifa huo kwa maana hata maslahi yake ya ubunge, atalipwa hadi Jumapili wiki iliyopita kabla ya barua kupokewa kesho yake.

Mtendaji huyo wa Bunge alisema taratibu za Mbunge kujiuzulu zinafafanuliwa na Katiba Ibara ya 149 na Sheria ya Uchaguzi, kifungu cha 61(3).

Akizungumzia ibara hiyo ya katiba, alisema mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi hususan uwaziri, unaibu waziri na ubunge, anaweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa yenye saini yake na ataiwasilisha kwa Spika.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 149(2) atahesabiwa tangu siku barua ilipopokewa. Kwa mujibu wa barua yake, aliiandika Julai 15 na sisi tukaipokea Julai 19," alisema kaimu huyo wa katibu wa Bunge.

Joel alisema, baada ya kuipitia barua na kubaini kwamba vifungu vyote vya uamuzi wa kujiuzulu vinajitosheleza, wakamshauri Spika akakubali na wameiandikia rasmi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwamba jimbo la Igunga lipo wazi.

Akijibu maswali ya waandishi waliotaka kufahamu suala zima la mafao, Joel alisema atahesabiwa mafao yake ya miezi saba.

Katika hatua nyingine, gari inayopaswa kutumiwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe imeegeshwa karakana huku ofisi ya Bunge ikiwa haina taarifa yoyote ya kukikabidhi rasmi chombo hicho.

"Sisi tulimkabidhi kwa mujibu wa masharti, lakini yeye hajawahi kuandika barua kuwa sharti fulani lina matatizo.

Gari halitumiki, hajalikabidhi, lipo kwenye karakana. Gari linatunzwa na Serikali. Akisema analihitaji, sisi tutampa," alisema Joel.
 
Nikikumbuka jinsi Zitto alivyojolitoa mhanga kumfanyia Kampeni Wenje kule Mwanza, Nikikumbuka Jinsi alivyopiga kambi Tegeta kumsaidia kampeni Halima Mdee, Jinsi alivyotia nguvu kumsaidia kampeni Mnyika hapo Ubungo, Nikikumbuka jinsi alivyozunguuka na Dr Slaa takriban nchi nzima, halafu leo hii Hawa Chadema wamesahau hili, nashindwa kuwaelewa hawa watu ni watu wa namna gani. Lakini Tatizo ni Tundu Lissu, huyu alikuwa akimuona Zitto kama kikwazo kwake Nyota yake kung'aa ndani na nje ya chama. Sasa tumuone kama ataweza kuvivaa viatu vya ZZK
Wote wachumia matumbo tuu kila mmoja anadhani atarithi uenyekiti chadema wamejaa wanafiki .inauma sana wasivyoshukuru hata kidogo zitto amekijenga sana chadema wamemuondoa kama Hana thamani lakini historia itawahukumu
 
Dhambi ya udini na ukanda itawatafuna daima
Mungu hamtupi mja wake, Zitto tupo nawe bega kwa bega.

umeongea ukweli Gamba, hawa CDM siwaelewi kabisa huyu jamaa hakupaswa kufukuzwa ama hakika kina Mbowe watajutia kumfukuza chamani huyu jamaa.
 
nimeshangaa huyo mkuu wa shuguli za bunge john joel hata kama ajapewa barua ameenda chama kingine tayari sasa bunge linamtambua zitto kupitia chama kipi?
 
Wote wachumia matumbo tuu kila mmoja anadhani atarithi uenyekiti chadema wamejaa wanafiki .inauma sana wasivyoshukuru hata kidogo zitto amekijenga sana chadema wamemuondoa kama Hana thamani lakini historia itawahukumu

Unavyoandika ni dhahiri wewe si mwanachadema. Sasa inakuwaje wale ambao si wanachadema mnasikitishwa na Zitto kuondolewa chadema? WanaCCM na wana ACT nilitarajia sasa mfurahie ujio wake, au kuna zaidi ya tunayoyaona?
 
Ishu ni kuwa wakimpa yote CHADEMA wana haki ya kulalamika?

Sio chadema tu ndio wenye haki ya kulalamika hata wewe na mimi tunayo haki ya kulalamika kama mafao yameenda kinyume na utaratibu.
 
Hakika anastahili kulipwa tena na bonusi apewe. Kwenye hilo bunge la 9 na 10 hivi nani aliyepiga kazi kumzidi Zito?
 
najiuliza uhusiano huu mkubwa kati ya CCM na Zitto ulijengeka lini maana mkuu hakuna mtu ambaye ametokea kupata favour kama anayoipata huyu jamaa kutoka kwa uongozi wa CCM

Ndio ujue umahiri wa kiongozi huyu,hakika Zitto ni tunu kwa taifa hili.
 
Last edited by a moderator:
Unavyoandika ni dhahiri wewe si mwanachadema. Sasa inakuwaje wale ambao si wanachadema mnasikitishwa na Zitto kuondolewa chadema? WanaCCM na wana ACT nilitarajia sasa mfurahie ujio wake, au kuna zaidi ya tunayoyaona?

Hatusikitiki kwa kufukuzwa kwake Chadema,tunasikitishwa na zengwe aliloundiwa.
 
Back
Top Bottom