Dodoma: Mussa Assad(CAG), ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, ripoti kukabidhiwa kwa Spika..

Dah..
Naona jamaa katumia hekima sana kwenda.

Cha ajabu eti taarifa zinasema sio Spika aliyemuita, ila ni kamati ya maadili iliyomuagiza Spika amuite kuhojiwa.
Kinachofuata hapo jamaa ni kuibuka mshindi tu, halafu soon Jiwe anaitisha shughuli ya kitaifa anamualika Assad na kumsifia mambo yanakwisha.

Ndugai ajiangalie sana.
Jiwe si mwanasiasa.
Atamharibia sana political carrier yake, na baadaye Ndugai ataonekana kama Spika aliyevurunda Tanzania.
we,siasa za,nchii hii bado hazijakukaa vizuri kichwan
 
DODOMA: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, amesema kamati yake imemaliza kumhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad.
bunge.jpg


Akizungumza na wanahabari baada ya mahojiano ya Kamati hiyo, Mwakasaka amesema; “CAG Prof. Assad amefika leo mbele ya kamati baada ya wito aliopewa na Spika na tumemhoji. Sisi kwa kanuni zetu hapa tunamwita mtuhumiwa, tukishakamilisha hili suala tunalipeleka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai,” amesema Mwakasaka.

Aidha, Mwakasaka amesema Prof. Assad ameonyesha ushirikiano mkubwa kwa maswali aliyoulizwa kamati hiyo.
assad-1024x576.jpg


Januari 7, 2019 Spika Job Ndugai alimtaka CAG kufika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli yake ya aliyoisema akiwa nje ya nchi kwa kusema kuwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhaifu.

-GlobalP
 
hii kamati imejaa wenye leaving cert.tu akitoa neno la kitaaluma wanatafutana

wapige picha na kula chakula cha mchana mambo yaishe

sahihi mkuu, tena inaongozwa na mwenyekiti kilaza sanz Emmanuel Mwakasaka mbunge wa Tabora mjini, jimbo lake limechoka sana lakini humsikii bungeni kutetea japo hata kidogo, yaani mkuu wa mkoa wa tabora ndo amakuwa mtetezi wa jimbo na mkoa
 
Kwahio mtuhumiwa anakabidhiwa ripoti ili achukue hatua zaidi?


Only in Tanzania!! Ndugai amelalamika kuwa amedhalilishwa na Ndugai hayo huyo anapelekewa ripoti ya kamati yake ili achukue hatua dhidi ya yule aliyemtuhumu!
 
Dah..
Naona jamaa katumia hekima sana kwenda.

Cha ajabu eti taarifa zinasema sio Spika aliyemuita, ila ni kamati ya maadili iliyomuagiza Spika amuite kuhojiwa.
Kinachofuata hapo jamaa ni kuibuka mshindi tu, halafu soon Jiwe anaitisha shughuli ya kitaifa anamualika Assad na kumsifia mambo yanakwisha.

Ndugai ajiangalie sana.
Jiwe si mwanasiasa.
Atamharibia sana political carrier yake, na baadaye Ndugai ataonekana kama Spika aliyevurunda Tanzania.
Hadi sasa ndo spika mvurundaji kuwahi kutokea.
 
kichotokea hapo ni sawa na Kumwita Mwalimu kashasha kuhojiwa na shafih Dauda, Jese john , edoku mwembe ,maestro na maulid kitenge" katika Dawati la michezo kwa Madai ati anawadhalilisha wachambuzi wa soka Tanzania " yani ni Tanzania pekee akili ndogo inaongoza akili kubwa.
 
Back
Top Bottom