Bunge, Serikali wasaka siri za Tundu Lissu

Bunge, Serikali wasaka siri za Tundu Lissu

Huwa najiuliza bila kupata majibu. Huyu Mungu yupo upande wenu tu!?
Huyo jamaa uliyemjibu yeye ametoa mawazo yake. Wewe unamtisha kwamba "Azichunge kauli zake".......utamfanya nini asipozichunga!!!??? Maana hapo Mungu umemuingiza tu, Ila nia yako Ovu ni dhahiri.
Hayo ni mawazo ya kipuuzi kuleta mizaha kwenye maisha ya mtu
 
imekuwa ndio msimamo wa Lissu mwenyewe kitandani, “niko tayari kufa kuliko kutibiwa kwa masharti.”
Mwenye nia njema huwa hatoi masharti ya kumuhudumia mgonjwa ambaye ana uhakika kwa asilimia zote kuwa ni mtu asiyejiweza,kutoa huduma pasipo masharti kwenye majanga kama haya ni njia mojawapo ya kuvuna thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu.

Wakati wananchi wa ndani ya nchi na wananchi wa nchi mbalimbali wanagombania wapelekewe Lissu wakamtibu kwa gharama zao pasipo masharti yoyote,cha kusikitisha ni serekali yenye majukumu ya kubeba gharama kwa raia wake wanapopatwa na majanga kama haya kukataa kutekeleza wajibu wake kwa kisingizio cha kukiukwa masharti.
 
Hii ni habari ya kipuuz.sio serikal wala bunge wanaojua lisu kaumia sehem zipi.Hizi taarifa za risasi mara imempiga miguuni nyingine tumbon mara mikononi nani huwa anazitoa?Maana wananchi wanajua kuna risasi zilimpata miguuni nyingine tumbon na mikononi. Kivipi tena isijulikane?Au mlikua mnawahadaha watu?

Kingine kama wewe ndo mwandishi wa habari basi hii taaruma unaidharirisha sana.Kuna haya hapo ziko katika maudhui moja lkn cha ajabu haya moja iko juu na kuikuta nyingine hadi upite haya mbili.Aya ya kupigwa risasi zaid ya 30 inamaudhui sawa na aya hiyo uliyoelezea siku ya tukio kutoka bungeni.
Taaluma, Unaidhalilisha.
 
Siri za tundu Lissu ziisaidie nn serikali?? Ww chapa kazi achana na umbea umbea
Mpuuzi wewe unajisajili leo leo kutuletea upumbavu wa kuhoji kinachofanyika?! Kama hakuwa threat kwao ni kwa nini walimumiminia risasi kama chatu?! Gebwe we
 
Lissu ni mbunge, bunge Lina haki ya kumtibu na kuratibu matibabu yake. Lawama za serikali bunge lisibebeshwe, ni vizuri uongozi Wa chadema uishauri vizuri familia, matibabu yale ni gharama kubwa, wananchi wenye mapenzi mema nao ni masikini!!

Bunge liruhusiwe kutimiza majukumu yake, hasira zisizidi busara.

Bunge watume hela za matibabu aidha kwenye akounti ya hosiptal au akauti ya chadema kama wengine wanavyofanya hakuna atakae zikataa, ila suala la kuratibu waachie familia na Chadema. Nionavyo mimi tatizo lililoko ni fedha za matibabu tu,
 
Serikali na bunge wanazidi kuumbuka kila kukicha kutokana na ubabe wao usiokuwa na maana.... Na bado, mtaendelea kuumbuka tu.... Mna roho mbaya nyinyi [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Wao wakiumwa aaah utafikri zile hela za baba zao, hilo li ndunga yembe limekataa india nusu mwaka wala hakuna aliyelisema *****, yaani wanaudhi hawa mbwa, unapewa dhamana ya kitu halafu hata hujui ufanye nini
 
Matatizo ya roho mbaya ni kuanza kutenda halafu kufikiri hufuata baadae.Watu walikataa kumtibia eti kwasababu utaratibu haukufuatwa.Hivi unaacha kumtibu MTU aliye maututi eti kwaajili ya utaratibu?Je kulikuwa na uhakika gani juu ya waliompiga risasi kutomfuata hospitali?Haohao wakasema wanataka familia ya Lisu iandike barua ili waweze kumtibia Lisu,lakini cha ajabu ktk mazungumzo yao na familia ya Lisu hayajapata muafaka eti kwakuwa chadema hawakuwa na mwakilishi ktk kikao hicho,huku ni kujichanganya maana walioambiwa waandike barua ni familia ya Lisu,sasa chadema ya nini hapa?Kama watanzania wasingechanga hela Lisu angetibiwa na brabra zenu?Si angeshakufa?Sasa mnawasiwasi wa nini? Au baada ya kusikia anaendelea vizuri?Najiuliza sana juu ya hiki kinachoendelea juu ya kumtibia mtu ambaye utaratibu haukufuatwa.Au tuamini kuwa utaratibu haukuvunjwa bali ni utashi tu wa wahusika? Na kama ulivunjwa iweje nao sasa hivi wanataka kuvunja utaratibu kwa kutaka kumtibia?Nini kinafaa hapa,ni kufuata utaratibu au utashi wa mtu?
 
Sijaelewa; why wamwalike James Mbatia na wasimwalike either Mbowe (kwa maana ya mwenyekiti) au kiongozi yeyote wa ju from Chadema ambako mgonjwa ndio hutumika nao badala yake wameenda NCCR-Mageuzi!? Kuna mtu naweza nielewesha hapa!? Mbatia angekua mtu wa Singida I could think, may be because ni home boy wake but Mbatia ni Mchagga wa Vunjo na tena wa chama tofauti na mgonjwa!? Well, ina maana hata yule mbunge wa Singida aliye enda kumjulia hali mgonjwa nae kawavimbia kuwaeleza hali halisi ya mgonjwa!????? Still najiuliza maswali mengi but all in all, damu ya mtu ni mbaya sana.
 
Mungu ni Mwema!!

Get well soon Lisu.

Watesi wako wanaendelea kuweweseka, wamegubikwa na hofu mioyoni mwao, wanasononeka wanatamani Ardhi ipasuke wajichimbie kabla haujaamuka kitandani maana utawavua nguo hadharani
 
Hivi yule aliye lazwa India miezi mitatu wali itana kwenye kikao na familia? Au bado wanafikiria Lissu amefariki? Maana mfu ndie huwekewa vikao.
Mia mia zetu zitamtibu Lissu bila masimango
maisha yapo kasi sana kila kitu kitapita tutasahau!
 
mtu unataka utaratibu kwa mtu aliye mahututi..Ujinga huu..hawakutegemea apone..hawakutegemea wananchi watachanga visenti vyao.wanajikomba.na bado.wataumbuka sna wanahizaya kabisa
 
kikao kimeitishwa kuona jinsi lissu atakavyotibiwa na serikali,lakini kubenea anasema serikali inasaka siri za Lissu!
sasa mchawi kama wewe unataka lisu atibiwe? na jiulize wachawi kama wwwe wako chama gani? alafu jiulize ni chama gani kinaunda serikali?
 
USIRI uliotanda kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, anayetibiwa nchini Kenya, unaitesa serikali na uongozi wa Bunge la Tanzania

Taarifa kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zinasema, wakuu wa Bunge na Serikali, mihimili ya dola, wamekuwa wakihaha kutafuta taarifa za kinachoendelea kwenye matibabu ya mwanasiasa huyo na kiongozi mwandamizi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lissu alijeruhiwa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 mwilini katika shambulio lililofanywa Septemba 7 mwaka huu akiwa mjini Dodoma kwa shughuli za Bunge. Tangu hapo, amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital) nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kutokana na kuwapo usiri mkubwa, Bunge liliamua kuitisha kikao maalum na familia ya Lissu ili kupata mwanya wa kufahamu kinachoendelea kuhusu matibabu ya mbunge huyo.

Kikao cha familia ya Lissu na Bunge, kilifanyika Jumatatu wiki hii, kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu wake, Dk. Tulia Ackson, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Hanang, Mary Nagu (CCM).

Wengine waliohudhuria kikao hicho, ni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, Katibu wa Spika, Said Yakoub, Alute Mughwai ambaye ni kaka mkubwa wa Lissu, dada yao mkubwa na mdogo wao aitwae Vicenti.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria wa Chadema, alishambuliwa nje ya nyumba yake eneo la Area D, mjini Dodoma alipowasili akitokea bungeni baada ya kumaliza kipindi cha asubuhi.

MwanaHALISI Online limefahamishwa na vyanzo vya habari kuwa “usiri uliotawala matibabu ya Lissu, umesukuma uongozi wa Bunge kuitisha kikao cha wanafamilia.”

“Bunge na hata serikali wanahaha kupata taarifa za matibabu ya Lissu… ni matokeo ya bunge kujiweka pembeni na jambo hili tokea mwanzo,”

Anasema mtoa taarifa. “Siyo spika wa Bunge wala serikali anayejua Lissu ameumia vipi na anatibiwa sehemu gani ya mwili wake. Hawajui matibabu yake yatachukua muda gani na ni nani hasa anayelipa gharama zake.”

Kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa chama chake kimeamua kuchukua dhamana kuhusu matibabu ya Lissu katika msingi wa kuwa jukumu la kusimamia matibabu ni la kifamilia zaidi, Bunge limejikuta gizani.

“Bunge liliyumba tokea awali… sasa linajaribu kujirejesha kwa nguvu kupitia familia. Lakini mpango huu hauwezi kufanikiwa kwa kuwa familia ya Lissu imebaki na msimamo wa kutopokea fedha kutoka serikalini,” ameeleza mtoa taarifa.

Taarifa ndani ya kikao kati ya uongozi wa Bunge na familia zinasema mkakati wa Bunge kujiweka karibu na Lissu umepata mtihani. Ni kutokana na familia kukataa kutoa taarifa iwapo Chadema haikuwakilishwa kikaoni.

“Chadema haikuhudhuria kikao kile. Sasa familia imegoma kuridhia matakwa ya Bunge,” anaeleza.

Taarifa zinasema mbele ya kikao, Bunge liliwasilisha pendekezo la kutaka kuwa mratibu na mlipaji mkuu wa matibabu ya Lissu. Familia imekataa.

Mmoja wa wanafamilia alinukuliwa akikiambia kikao hicho kwamba wapewe muda wa kujadiliana kuhusu mapendekezo ya Bunge. Wa kujadiliana nao ni uongozi wa juu wa Chadema.

“Kutokana na utata uliogubika na serikali inavyoshambuliwa kwa kushindwa kukamata watuhumiwa, hatuwezi kuridhia lolote hapa,” alinukuliwa mwanafamilia akisema kikaoni.

Familia ya Lissu, kwa mujibu wa taarifa hizo, imeomba muda w amashauriano kwa kuwa imekuwa ndio msimamo wa Lissu mwenyewe kitandani, “niko tayari kufa kuliko kutibiwa kwa masharti.”

Kikao cha familia ya Lissu na uongozi wa Bunge kilifanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:55 asubuhi mpaka saa 7:40 mchana.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amekiri kutofikiwa kwa muafaka katika kikao hicho kuhusu mapendekezo ya Bunge.

“Ni kweli tulikutana na kuzungumza na familia ya Lissu, lakini hatukuweza kufikia mwafaka kutokana na msimamo wa familia. Tumekubaliana kukutana tena wakati mwingine,” alisema.

Alipoulizwa ni kipi kimesababisha mkwamo, Mbatia alisema, “ni kutoaminiana.” Upande wa Chadema na familia umeonekana kutokubaliana kuhusu msimamo wa Bunge. Kauli za Bunge na zile za Ummy Mwalimu, zimechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo ufa wa mahusiano kati ya pande hizi mbili.”

Ummy ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, ambaye wiki iliyopita alisikika akitoa msimamo wa serikali kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya Lissu kokote nje ya nchi. Awali, waziri huyo na bunge walinukuliwa wakisema mjini Dodoma kuwa serikali imejiondoa kwenye suala hilo baada ya familia ya Lissu kushikilia kumchukua na kumpatia matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kikao cha familia na Bunge, Alute, kaka wa Lissu, alikiri kutokamilika kwa mazungumzo. Sababu ameitaja kuwa ni kukosekana kiongozi kutoka Chadema.

Alute ambaye kama Lissu, naye ni wakili wa Mahakama Kuu, anayefanyia shughuli zake mkoani Arusha, alisema, “siwezi kusema zaidi ya hayo.”

Anasema, “moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani, mambo tuliyoyajadili yanamuhusu Lissu.”

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kueleza sababu za Chadema kukosa uwakilishi kwenye kikao hicho.
Polisi wameshindwa kuitafuta wala kuitambua silaha iliyotumika! Nini maana ya usajili wa silaha?
 
Back
Top Bottom