Bunge, Serikali wasaka siri za Tundu Lissu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
USIRI uliotanda kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, anayetibiwa nchini Kenya, unaitesa serikali na uongozi wa Bunge la Tanzania

Taarifa kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zinasema, wakuu wa Bunge na Serikali, mihimili ya dola, wamekuwa wakihaha kutafuta taarifa za kinachoendelea kwenye matibabu ya mwanasiasa huyo na kiongozi mwandamizi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lissu alijeruhiwa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 mwilini katika shambulio lililofanywa Septemba 7 mwaka huu akiwa mjini Dodoma kwa shughuli za Bunge. Tangu hapo, amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital) nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kutokana na kuwapo usiri mkubwa, Bunge liliamua kuitisha kikao maalum na familia ya Lissu ili kupata mwanya wa kufahamu kinachoendelea kuhusu matibabu ya mbunge huyo.

Kikao cha familia ya Lissu na Bunge, kilifanyika Jumatatu wiki hii, kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu wake, Dk. Tulia Ackson, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Hanang, Mary Nagu (CCM).

Wengine waliohudhuria kikao hicho, ni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, Katibu wa Spika, Said Yakoub, Alute Mughwai ambaye ni kaka mkubwa wa Lissu, dada yao mkubwa na mdogo wao aitwae Vicenti.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria wa Chadema, alishambuliwa nje ya nyumba yake eneo la Area D, mjini Dodoma alipowasili akitokea bungeni baada ya kumaliza kipindi cha asubuhi.

MwanaHALISI Online limefahamishwa na vyanzo vya habari kuwa “usiri uliotawala matibabu ya Lissu, umesukuma uongozi wa Bunge kuitisha kikao cha wanafamilia.”

“Bunge na hata serikali wanahaha kupata taarifa za matibabu ya Lissu… ni matokeo ya bunge kujiweka pembeni na jambo hili tokea mwanzo,”

Anasema mtoa taarifa. “Siyo spika wa Bunge wala serikali anayejua Lissu ameumia vipi na anatibiwa sehemu gani ya mwili wake. Hawajui matibabu yake yatachukua muda gani na ni nani hasa anayelipa gharama zake.”

Kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa chama chake kimeamua kuchukua dhamana kuhusu matibabu ya Lissu katika msingi wa kuwa jukumu la kusimamia matibabu ni la kifamilia zaidi, Bunge limejikuta gizani.

“Bunge liliyumba tokea awali… sasa linajaribu kujirejesha kwa nguvu kupitia familia. Lakini mpango huu hauwezi kufanikiwa kwa kuwa familia ya Lissu imebaki na msimamo wa kutopokea fedha kutoka serikalini,” ameeleza mtoa taarifa.

Taarifa ndani ya kikao kati ya uongozi wa Bunge na familia zinasema mkakati wa Bunge kujiweka karibu na Lissu umepata mtihani. Ni kutokana na familia kukataa kutoa taarifa iwapo Chadema haikuwakilishwa kikaoni.

“Chadema haikuhudhuria kikao kile. Sasa familia imegoma kuridhia matakwa ya Bunge,” anaeleza.

Taarifa zinasema mbele ya kikao, Bunge liliwasilisha pendekezo la kutaka kuwa mratibu na mlipaji mkuu wa matibabu ya Lissu. Familia imekataa.

Mmoja wa wanafamilia alinukuliwa akikiambia kikao hicho kwamba wapewe muda wa kujadiliana kuhusu mapendekezo ya Bunge. Wa kujadiliana nao ni uongozi wa juu wa Chadema.

“Kutokana na utata uliogubika na serikali inavyoshambuliwa kwa kushindwa kukamata watuhumiwa, hatuwezi kuridhia lolote hapa,” alinukuliwa mwanafamilia akisema kikaoni.

Familia ya Lissu, kwa mujibu wa taarifa hizo, imeomba muda w amashauriano kwa kuwa imekuwa ndio msimamo wa Lissu mwenyewe kitandani, “niko tayari kufa kuliko kutibiwa kwa masharti.”

Kikao cha familia ya Lissu na uongozi wa Bunge kilifanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:55 asubuhi mpaka saa 7:40 mchana.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amekiri kutofikiwa kwa muafaka katika kikao hicho kuhusu mapendekezo ya Bunge.

“Ni kweli tulikutana na kuzungumza na familia ya Lissu, lakini hatukuweza kufikia mwafaka kutokana na msimamo wa familia. Tumekubaliana kukutana tena wakati mwingine,” alisema.

Alipoulizwa ni kipi kimesababisha mkwamo, Mbatia alisema, “ni kutoaminiana.” Upande wa Chadema na familia umeonekana kutokubaliana kuhusu msimamo wa Bunge. Kauli za Bunge na zile za Ummy Mwalimu, zimechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo ufa wa mahusiano kati ya pande hizi mbili.”

Ummy ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, ambaye wiki iliyopita alisikika akitoa msimamo wa serikali kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya Lissu kokote nje ya nchi. Awali, waziri huyo na bunge walinukuliwa wakisema mjini Dodoma kuwa serikali imejiondoa kwenye suala hilo baada ya familia ya Lissu kushikilia kumchukua na kumpatia matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kikao cha familia na Bunge, Alute, kaka wa Lissu, alikiri kutokamilika kwa mazungumzo. Sababu ameitaja kuwa ni kukosekana kiongozi kutoka Chadema.

Alute ambaye kama Lissu, naye ni wakili wa Mahakama Kuu, anayefanyia shughuli zake mkoani Arusha, alisema, “siwezi kusema zaidi ya hayo.”

Anasema, “moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani, mambo tuliyoyajadili yanamuhusu Lissu.”

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kueleza sababu za Chadema kukosa uwakilishi kwenye kikao hicho.
 
Mungu aliye tajiri wa vyote ataendelea kutupa fedha za kumtibu Lissu...who would thought Mange Kimambi peke yake angeweza kuchangisha zaidi ya Sh.Mil.60 akiwa mbali kwa ajili ya kumtibu Lissu? WE ARE FINE NO PROBLEM...the killers should go to hell and burn among the rocks!
 
Serikali na bunge wanazidi kuumbuka kila kukicha kutokana na ubabe wao usiokuwa na maana.... Na bado, mtaendelea kuumbuka tu.... Mna roho mbaya nyinyi [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwani wanakwama nini kukiri u husika wao ili yaishe?
 
Zichunge sana kauli zako mkuu.. Mungu hadhihakiwi!!! Utajikuta pabaya hutoamini
Huwa najiuliza bila kupata majibu. Huyu Mungu yupo upande wenu tu!?
Huyo jamaa uliyemjibu yeye ametoa mawazo yake. Wewe unamtisha kwamba "Azichunge kauli zake".......utamfanya nini asipozichunga!!!??? Maana hapo Mungu umemuingiza tu, Ila nia yako Ovu ni dhahiri.
 
USIRI uliotanda kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, anayetibiwa nchini Kenya, unaitesa serikali na uongozi wa Bunge la Tanzania

Taarifa kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zinasema, wakuu wa Bunge na Serikali, mihimili ya dola, wamekuwa wakihaha kutafuta taarifa za kinachoendelea kwenye matibabu ya mwanasiasa huyo na kiongozi mwandamizi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lissu alijeruhiwa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 mwilini katika shambulio lililofanywa Septemba 7 mwaka huu akiwa mjini Dodoma kwa shughuli za Bunge. Tangu hapo, amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital) nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kutokana na kuwapo usiri mkubwa, Bunge liliamua kuitisha kikao maalum na familia ya Lissu ili kupata mwanya wa kufahamu kinachoendelea kuhusu matibabu ya mbunge huyo.

Kikao cha familia ya Lissu na Bunge, kilifanyika Jumatatu wiki hii, kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu wake, Dk. Tulia Ackson, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Hanang, Mary Nagu (CCM).

Wengine waliohudhuria kikao hicho, ni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, Katibu wa Spika, Said Yakoub, Alute Mughwai ambaye ni kaka mkubwa wa Lissu, dada yao mkubwa na mdogo wao aitwae Vicenti.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria wa Chadema, alishambuliwa nje ya nyumba yake eneo la Area D, mjini Dodoma alipowasili akitokea bungeni baada ya kumaliza kipindi cha asubuhi.

MwanaHALISI Online limefahamishwa na vyanzo vya habari kuwa “usiri uliotawala matibabu ya Lissu, umesukuma uongozi wa Bunge kuitisha kikao cha wanafamilia.”

“Bunge na hata serikali wanahaha kupata taarifa za matibabu ya Lissu… ni matokeo ya bunge kujiweka pembeni na jambo hili tokea mwanzo,”

Anasema mtoa taarifa. “Siyo spika wa Bunge wala serikali anayejua Lissu ameumia vipi na anatibiwa sehemu gani ya mwili wake. Hawajui matibabu yake yatachukua muda gani na ni nani hasa anayelipa gharama zake.”

Kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa chama chake kimeamua kuchukua dhamana kuhusu matibabu ya Lissu katika msingi wa kuwa jukumu la kusimamia matibabu ni la kifamilia zaidi, Bunge limejikuta gizani.

“Bunge liliyumba tokea awali… sasa linajaribu kujirejesha kwa nguvu kupitia familia. Lakini mpango huu hauwezi kufanikiwa kwa kuwa familia ya Lissu imebaki na msimamo wa kutopokea fedha kutoka serikalini,” ameeleza mtoa taarifa.

Taarifa ndani ya kikao kati ya uongozi wa Bunge na familia zinasema mkakati wa Bunge kujiweka karibu na Lissu umepata mtihani. Ni kutokana na familia kukataa kutoa taarifa iwapo Chadema haikuwakilishwa kikaoni.

“Chadema haikuhudhuria kikao kile. Sasa familia imegoma kuridhia matakwa ya Bunge,” anaeleza.

Taarifa zinasema mbele ya kikao, Bunge liliwasilisha pendekezo la kutaka kuwa mratibu na mlipaji mkuu wa matibabu ya Lissu. Familia imekataa.

Mmoja wa wanafamilia alinukuliwa akikiambia kikao hicho kwamba wapewe muda wa kujadiliana kuhusu mapendekezo ya Bunge. Wa kujadiliana nao ni uongozi wa juu wa Chadema.

“Kutokana na utata uliogubika na serikali inavyoshambuliwa kwa kushindwa kukamata watuhumiwa, hatuwezi kuridhia lolote hapa,” alinukuliwa mwanafamilia akisema kikaoni.

Familia ya Lissu, kwa mujibu wa taarifa hizo, imeomba muda w amashauriano kwa kuwa imekuwa ndio msimamo wa Lissu mwenyewe kitandani, “niko tayari kufa kuliko kutibiwa kwa masharti.”

Kikao cha familia ya Lissu na uongozi wa Bunge kilifanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:55 asubuhi mpaka saa 7:40 mchana.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amekiri kutofikiwa kwa muafaka katika kikao hicho kuhusu mapendekezo ya Bunge.

“Ni kweli tulikutana na kuzungumza na familia ya Lissu, lakini hatukuweza kufikia mwafaka kutokana na msimamo wa familia. Tumekubaliana kukutana tena wakati mwingine,” alisema.

Alipoulizwa ni kipi kimesababisha mkwamo, Mbatia alisema, “ni kutoaminiana.” Upande wa Chadema na familia umeonekana kutokubaliana kuhusu msimamo wa Bunge. Kauli za Bunge na zile za Ummy Mwalimu, zimechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo ufa wa mahusiano kati ya pande hizi mbili.”

Ummy ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, ambaye wiki iliyopita alisikika akitoa msimamo wa serikali kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya Lissu kokote nje ya nchi. Awali, waziri huyo na bunge walinukuliwa wakisema mjini Dodoma kuwa serikali imejiondoa kwenye suala hilo baada ya familia ya Lissu kushikilia kumchukua na kumpatia matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kikao cha familia na Bunge, Alute, kaka wa Lissu, alikiri kutokamilika kwa mazungumzo. Sababu ameitaja kuwa ni kukosekana kiongozi kutoka Chadema.

Alute ambaye kama Lissu, naye ni wakili wa Mahakama Kuu, anayefanyia shughuli zake mkoani Arusha, alisema, “siwezi kusema zaidi ya hayo.”

Anasema, “moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani, mambo tuliyoyajadili yanamuhusu Lissu.”

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kueleza sababu za Chadema kukosa uwakilishi kwenye kikao hicho.

Hii ni habari ya kipuuz.sio serikal wala bunge wanaojua lisu kaumia sehem zipi.Hizi taarifa za risasi mara imempiga miguuni nyingine tumbon mara mikononi nani huwa anazitoa?Maana wananchi wanajua kuna risasi zilimpata miguuni nyingine tumbon na mikononi. Kivipi tena isijulikane?Au mlikua mnawahadaha watu?

Kingine kama wewe ndo mwandishi wa habari basi hii taaruma unaidharirisha sana.Kuna haya hapo ziko katika maudhui moja lkn cha ajabu haya moja iko juu na kuikuta nyingine hadi upite haya mbili.Aya ya kupigwa risasi zaid ya 30 inamaudhui sawa na aya hiyo uliyoelezea siku ya tukio kutoka bungeni.
 
Back
Top Bottom