Bunge, Serikali wasaka siri za Tundu Lissu

Bunge, Serikali wasaka siri za Tundu Lissu

Heri wewe usiekuwa na kilema leo na unaedhani u mtimilifu, lakini unaijua kesho yako na mapungufu yake kwako?
Ni Lisu aliewaita wanaomsababishia leo awe kitandani na huku wewe ukifulahia?
Lisu hajawa kilema kama wewe unavyoomba iwe,hakuna alie toa taarifa ya ulemavu wa lisu hadi sasa!
Umelaaniwa wewe binaadamu uombae na kufurahia mabaya juu ya binaadam wengine, ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yako.
Kwa kuwa tunaamini ni Mungu aliemnusulu Lisu na uvuri wa mauti ni yeye huyohuyo atamnusulu na kilema,na rehema na utukufu wa bwana utajidhihirisha juu yake.
AMINA.
Mkuu hao watu wa Rwanda tuachane nao Mungu anatenda miujiza.
 
Umesikika vema, una bahati wewe uliyelipia uzima wako
 
Hapana mkuu usimuombee ili afe, ila muombe Mungu wako ampige na kumuadhibu Kama yule aliekuwa mbabe wa zenji ambaye kufa anahitaji kuliko chochote lakin Mungu hataki kumuita,,,Amuombeane mwenzie mabaya hakika mabaya hayo huanzia kwake,,,
Kwenye maombi yangu nina jua jinsi ya kuomba bila shaka mungu wangu atatenda miujiza huyo Troll atapatwa na kiharusi naomba muamini hivyo!!!
 
Siri za tundu Lissu ziisaidie nn serikali?? Ww chapa kazi achana na umbea umbea
 
Huwezi kubali shetani aliyetaka kukuwa, awe mratibu wa matibabu!!! No,no,no. Utakuwa nijinga kukubsli. Serikali na bunge wanataka kuwslaghai wananchi wasiamini kuwa wao ni watuhumiwa.lakini watanzani waneshazigundua hila za kishetani za serikali na bunge.
 
Kama unadhani kuna mtu atapanic kwa upumbavu wako unajidanganya. Umezakiwa mpumbavu, utakuwa fala na utakufa hayawani.
Kiukweli mmepanic. Tatizo lenu kila kitu ni agenda. Na nimeona tayar mmeshahama kwenye hoja.
 
Nakwambia ujue japo masikini.....sitaki kunyanyasikaa....sitaki madharau.....

by msondo ngoma.
 
Lissu ni mbunge, bunge Lina haki ya kumtibu na kuratibu matibabu yake. Lawama za serikali bunge lisibebeshwe, ni vizuri uongozi Wa chadema uishauri vizuri familia, matibabu yale ni gharama kubwa, wananchi wenye mapenzi mema nao ni masikini!!

Bunge liruhusiwe kutimiza majukumu yake, hasira zisizidi busara.
 
USIRI uliotanda kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, anayetibiwa nchini Kenya, unaitesa serikali na uongozi wa Bunge la Tanzania

Taarifa kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zinasema, wakuu wa Bunge na Serikali, mihimili ya dola, wamekuwa wakihaha kutafuta taarifa za kinachoendelea kwenye matibabu ya mwanasiasa huyo na kiongozi mwandamizi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lissu alijeruhiwa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 mwilini katika shambulio lililofanywa Septemba 7 mwaka huu akiwa mjini Dodoma kwa shughuli za Bunge. Tangu hapo, amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital) nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kutokana na kuwapo usiri mkubwa, Bunge liliamua kuitisha kikao maalum na familia ya Lissu ili kupata mwanya wa kufahamu kinachoendelea kuhusu matibabu ya mbunge huyo.

Kikao cha familia ya Lissu na Bunge, kilifanyika Jumatatu wiki hii, kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu wake, Dk. Tulia Ackson, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Hanang, Mary Nagu (CCM).

Wengine waliohudhuria kikao hicho, ni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, Katibu wa Spika, Said Yakoub, Alute Mughwai ambaye ni kaka mkubwa wa Lissu, dada yao mkubwa na mdogo wao aitwae Vicenti.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria wa Chadema, alishambuliwa nje ya nyumba yake eneo la Area D, mjini Dodoma alipowasili akitokea bungeni baada ya kumaliza kipindi cha asubuhi.

MwanaHALISI Online limefahamishwa na vyanzo vya habari kuwa “usiri uliotawala matibabu ya Lissu, umesukuma uongozi wa Bunge kuitisha kikao cha wanafamilia.”

“Bunge na hata serikali wanahaha kupata taarifa za matibabu ya Lissu… ni matokeo ya bunge kujiweka pembeni na jambo hili tokea mwanzo,”

Anasema mtoa taarifa. “Siyo spika wa Bunge wala serikali anayejua Lissu ameumia vipi na anatibiwa sehemu gani ya mwili wake. Hawajui matibabu yake yatachukua muda gani na ni nani hasa anayelipa gharama zake.”

Kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa chama chake kimeamua kuchukua dhamana kuhusu matibabu ya Lissu katika msingi wa kuwa jukumu la kusimamia matibabu ni la kifamilia zaidi, Bunge limejikuta gizani.

“Bunge liliyumba tokea awali… sasa linajaribu kujirejesha kwa nguvu kupitia familia. Lakini mpango huu hauwezi kufanikiwa kwa kuwa familia ya Lissu imebaki na msimamo wa kutopokea fedha kutoka serikalini,” ameeleza mtoa taarifa.

Taarifa ndani ya kikao kati ya uongozi wa Bunge na familia zinasema mkakati wa Bunge kujiweka karibu na Lissu umepata mtihani. Ni kutokana na familia kukataa kutoa taarifa iwapo Chadema haikuwakilishwa kikaoni.

“Chadema haikuhudhuria kikao kile. Sasa familia imegoma kuridhia matakwa ya Bunge,” anaeleza.

Taarifa zinasema mbele ya kikao, Bunge liliwasilisha pendekezo la kutaka kuwa mratibu na mlipaji mkuu wa matibabu ya Lissu. Familia imekataa.

Mmoja wa wanafamilia alinukuliwa akikiambia kikao hicho kwamba wapewe muda wa kujadiliana kuhusu mapendekezo ya Bunge. Wa kujadiliana nao ni uongozi wa juu wa Chadema.

“Kutokana na utata uliogubika na serikali inavyoshambuliwa kwa kushindwa kukamata watuhumiwa, hatuwezi kuridhia lolote hapa,” alinukuliwa mwanafamilia akisema kikaoni.

Familia ya Lissu, kwa mujibu wa taarifa hizo, imeomba muda w amashauriano kwa kuwa imekuwa ndio msimamo wa Lissu mwenyewe kitandani, “niko tayari kufa kuliko kutibiwa kwa masharti.”

Kikao cha familia ya Lissu na uongozi wa Bunge kilifanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:55 asubuhi mpaka saa 7:40 mchana.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amekiri kutofikiwa kwa muafaka katika kikao hicho kuhusu mapendekezo ya Bunge.

“Ni kweli tulikutana na kuzungumza na familia ya Lissu, lakini hatukuweza kufikia mwafaka kutokana na msimamo wa familia. Tumekubaliana kukutana tena wakati mwingine,” alisema.

Alipoulizwa ni kipi kimesababisha mkwamo, Mbatia alisema, “ni kutoaminiana.” Upande wa Chadema na familia umeonekana kutokubaliana kuhusu msimamo wa Bunge. Kauli za Bunge na zile za Ummy Mwalimu, zimechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo ufa wa mahusiano kati ya pande hizi mbili.”

Ummy ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, ambaye wiki iliyopita alisikika akitoa msimamo wa serikali kuwa ipo tayari kugharamia matibabu ya Lissu kokote nje ya nchi. Awali, waziri huyo na bunge walinukuliwa wakisema mjini Dodoma kuwa serikali imejiondoa kwenye suala hilo baada ya familia ya Lissu kushikilia kumchukua na kumpatia matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kikao cha familia na Bunge, Alute, kaka wa Lissu, alikiri kutokamilika kwa mazungumzo. Sababu ameitaja kuwa ni kukosekana kiongozi kutoka Chadema.

Alute ambaye kama Lissu, naye ni wakili wa Mahakama Kuu, anayefanyia shughuli zake mkoani Arusha, alisema, “siwezi kusema zaidi ya hayo.”

Anasema, “moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani, mambo tuliyoyajadili yanamuhusu Lissu.”

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kueleza sababu za Chadema kukosa uwakilishi kwenye kikao hicho.
KWANINI WALIMUALIKA MBATIA NA MBOWE??
 
Ernesto Che Guevara wakati akipambana dhidi ya madhila wa ubepari aliwahi kusema...., " I BETTER DIE ON MY FEET THAN STAND ON MY KNEES ".....,

Viva Lissu..
Do wish you a very quick recovery.
Aluta Continua.
 
Tundu Lissu yupi huyu Mlemavu? Wanamuonea.
Yani ktk wapumbavu watatu wa nchi hii wewe ni wa kwanza, na wakikupanga namba mbili, hao wapangaji itabidi watumbuliwe kwa kukosa uadilifu. You're the most hopeless among the extremely hopeless.
 
Tundu Lissu yupi huyu Mlemavu? Wanamuonea.
Maxence Melo Invisible Moderator Paw na wengineo, mtu kama huyu mnamuachaje?

JamiiForums tambueni watu kama hawa hata siku JamiiForums ikipata matatizo au wamiliki weke bahati mbaya wakashindwa kesi zilizoko Mahakamani(Mungu apishie mbali), hawa watu hata nyinyi watakuja kuwakejeli.

Eleweni watu kama hawa huenda wanatamani hata huu mtandao usiwepo kama ambavyo wanafurahia yaliyomkuta Lissu aliekuwa mkosaji wa serikali.

Hawa sio wenzetu kabisa.
 
Huwa najiuliza bila kupata majibu. Huyu Mungu yupo upande wenu tu!?
Huyo jamaa uliyemjibu yeye ametoa mawazo yake. Wewe unamtisha kwamba "Azichunge kauli zake".......utamfanya nini asipozichunga!!!??? Maana hapo Mungu umemuingiza tu, Ila nia yako Ovu ni dhahiri.[/QUOTE

Kiazi kingine
 
Huwa najiuliza bila kupata majibu. Huyu Mungu yupo upande wenu tu!? Maana wachawi na watu WAOVU kutwa Mungu yupo katika NDIMI zao.
Huyo jamaa uliyemjibu yeye ametoa mawazo yake. Wewe unamtisha kwamba "Azichunge kauli zake".......utamfanya nini asipozichunga!!!??? Maana hapo Mungu umemuingiza tu, Ila nia yako Ovu ni dhahiri.
 
Yaani umkane mtoto wako halafu baada ya kuona kuna waliopata uchungu nae wakaamua wamchukue wamhudumie ndo unaanza kujipendekeza?? Halafu Yohana ndo anatuita sisi vilaza na wapumbavu hahaha aisee
 
Maxence Melo Invisible Moderator Paw na wengineo, mtu kama huyu mnamuachaje?

JamiiForums tambueni watu kama hawa hata siku JamiiForums ikipata matatizo au wamiliki weke bahati mbaya wakashindwa kesi zilizoko Mahakamani(Mungu apishie mbali), hawa watu hata nyinyi watakuja kuwakejeli.

Eleweni watu kama hawa huenda wanatamani hata huu mtandao usiwepo kama ambavyo wanafurahia yaliyomkuta Lissu aliekuwa mkosaji wa serikali.

Hawa sio wenzetu kabisa.
Wewe huwa unaachwaje ukitukana watu humu?
Vumilia mitazamo yake. Hajatukana mtu hapo, ameelezea fikra zake.
 
Back
Top Bottom