econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 22,138
- 32,715
Kwanza nimpe pole Speaker mstaafu kwa yaliyompata. Na hili liwe funzo kwetu kuwa unapokuwa na madaraka usiumize upande mmoja huwezi kujua kesho itakuwaje. Kuna observation nimeipata kutokana na sakata la Ndugai.
1. Kwanza, inaonekana Bunge ni tasisi ya CCM ndio maana hata speaker kwenye barua yake amemnukuu katibu mkuu wa CCM.
2. Pili, wabunge wa CCM wanamlaumu speaker kuenenda tofauti na Mwenyekiti wake wa chama. Kwamba speaker aendane na Mwenyekiti wake la sivyo ajiuzulu. Hivyo kulifanya bunge kuwa taasisi ya CCM. Haya yamesemwa na wabunge wengi akiwemo Msukuma , Lusinde na gwajima
3. Tatu, Speaker alipotoa maoni yake ni Viongozi wa CCM ndio waliomshambulia sana, kiasi cha kumtaka ajiuzulu. Na hata alipoomba msamaha Mwenyekiti wa CCM bado alimpiga vijembe na kumwambia ana stress za 2025. Na kuambiwa Ni adui namba moja.
4. Nne, Rais aliwapongeza wenyeviti wa CCM waliomshambulia ndugai baada ya kutoa hoja yake ya mikopo. Hi inamaanisha wenyeviti wana status ya kumshambulia speaker bila shida.
5. Tano, hata speaker Ndugai mwenyewe alipokuwa kwenye kiti Cha uspika alikitumikia Sana chama Cha CCM zaidi ya mhimili wa bunge. Kwa mfano kwenye awamu ya tano speaker alimuondoa kwenye ubunge Mh Lissu, wakati akiwa bado anaomba kuhakikishiwa usalama akirudi nchini. Wakati ambao spika alitakiwa kusimama na Mh Lissu Kama mbunge chini ya mhimili wake yeye aka mmistreat kisa ni upinzani. Hivi karibuni karuhusu wabunge ambao chama hakikuwapitisha na hakiwatambui na kudai atawakinga hamna wa kuwasumbua. Yani spika anavunja katiba kisa tu kuwafustrate CHADEMA?.
Cha kufanya ili bunge lisiwe taasisi ya CCM.
1. Speaker asidhaminiwe na chama awe mtu huru anayechaguliwa na wabunge. Hi itaondoa allegence kwenye chama na kufuata matakwa ya chama bungeni.
2. Speaker awe ni mtu impartial yani awe mtu asiyeegemea upande wowote. Kanuni za bunge zirekebishwe ili moja ya sababu za kumuondoa speaker iwe pale anapofanya upendeleo.